Zanzibar: Mwanaume afikishwa Mahakamani kwa kukata viuno hadharani

Zanzibar: Mwanaume afikishwa Mahakamani kwa kukata viuno hadharani

Sasa kidume unakataje viuno?

Ujue vitu vingine hivi mtailaumu serikali bure tu
 
Mila na desturi zetu halis "OG" ni kutembea uchi. Ni ujuha kuongoza nchi kwa mila na desturi, hayo mambo ni ya Kitaliban.
Kuna vitu vilivyokuwa vinafanywa miaka ya zamani nikwasababu tu ya zama za ujinga za kipindi hicho na sio desturi

Sio kila jambo la kale ni desturi, angalia na mazingira walikuwa na option ya kufanya kinyume na hapo au walilazimika kufanya hivyo kwasababu hawakuwa na option
 
Zanzibar ni nchi ya kiislamu?

===
Maulid Hussein Abdallah maarufu kama Mauzinde (29) amefikishwa Mahakama ya Mwanzo katika Kijiji cha Mwera Wilaya ya Magharibi Unguja Kisiwani Zanzibar, kwa tuhuma ya kukata viuno hadharani.

Kijana huyo mkazi wa Rahaleo anatuhumiwa kutenda kosa hilo huko Kibole, Wilaya ya Kati, Kusini Unguja saa 11 jioni, ambapo mshitakiwa akiwa amevalia mtandio alicheza kwa kukata kiuno mbele ya hadhara jambo ambalo ni kosa kisheria.

Mshitakiwa huyo amepinga mashtaka hayo na kuiomba Mahakama kumpa dhamana kwa kuwa yupo kituo cha polisi siku nyingi.

Amri ya kupelekwa rumande imetolewa na Hakimu Safia Waziri, baada ya mshitakiwa kushindwa kutekeleza masharti ya dhamana ambayo yalimtaka kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya TZS 100,000 pamoja na barua zikiambatana na kopi ya kitambulisho cha Mzanzibar.

Mshitakiwa baada ya kushindwa kutekeleza masharti hayo, mahakama ilimuamuriwa kwenda rumande hadi Aprili 25, 2022 kwa ajili ya kuanza kusikilizwa ushahidi.

Source: Swahilitimes
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mwisho wa siku nchi lazima ichangamke, huyo ndugu yetu alikua kwenye harakati za kuchangamsha nchi sema tu mambo yame muendea kombo.
 
Huyo mkata kiuno angepelekwa kwenye mahakama ya kadhi ili adhabu stahiki, pumvafu kabisa
 
Back
Top Bottom