Zanzibar turudishe heshima yetu, tuige mfano mzuri wa Qatar, pombe ipigwe marufuku kabisa

Zanzibar turudishe heshima yetu, tuige mfano mzuri wa Qatar, pombe ipigwe marufuku kabisa

Kutembea uchi na kuzini hovyo ndio tabia za stone age, mwanadamu alipostaarabika ndio akaanza kuvaa kwa stara na kufunga ndoa
Unajua maana ya neno USTA-ARABU na neno KUST-ARABIKA????Mdogo wangu????NA STONE AGE UNAZINGUMIZIA YA UPANDE UPI DUNIANI????MAANA DUNIA KUBWA MDOGO WANGU
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wewe kama hunywi pombe au huli mbususu acha wengine wazichakate,usilazimishe tabia zenu za stone age kwa watu wastaarabu, au sepa kaishi na wenzako wa Talebans mkatane mikono vizuri
 
Nchi ya Qatar imenivutia sana kwa kuwa na msimamo mzuri dhidi ya uozo wa kimagharibi wa pombe, ngono, ushoga etc

Zanzibar ni nchi nzuri ya kistaarabu sana lakini naona kuna uozo unaongezeka kwa kasi kubwa.

Nyimbo na video za uchi, unywaji pombe, kuvaa vivazi vya nusu uchi hadharani n.k.

Ni muda sasa wa Zanzibar kuweka heshima ya ustaarabu wetu tupige marufuku bar zote na TV zinazopiga nyimbo za nusu uchi.

Kabla ujawaza bia, Anza kwanza na kuwatoa wale watu wa pale ccm hall
 
Mchele mtatoa wapi na viazi vya chips alafu nimesahau na umeme.
bado na lengine bajeti ya serikali inayotoka bara pamoja na waajiliwa znz kuja bara.
Kabla ya April 1964 vyakula tulikuwa tunatoa wapi? Na hata kama tunatoa bara si tunanunua kwa fedha zetu kama biashara nyingine?
 
Nchi ya Qatar imenivutia sana kwa kuwa na msimamo mzuri dhidi ya uozo wa kimagharibi wa pombe, ngono, ushoga etc

Zanzibar ni nchi nzuri ya kistaarabu sana lakini naona kuna uozo unaongezeka kwa kasi kubwa.

Nyimbo na video za uchi, unywaji pombe, kuvaa vivazi vya nusu uchi hadharani n.k.

Ni muda sasa wa Zanzibar kuweka heshima ya ustaarabu wetu tupige marufuku bar zote na TV zinazopiga nyimbo za nusu uchi.
Leo hii uko Dini ilikoanzia wamefuta kodi ya Pombe na akuna tena police kusumbuwa walevi
 
Attachments

  • 746F3612-67DB-4F1F-A942-573832EA889A.png
    746F3612-67DB-4F1F-A942-573832EA889A.png
    301.5 KB · Views: 5
Nchi ya Qatar imenivutia sana kwa kuwa na msimamo mzuri dhidi ya uozo wa kimagharibi wa pombe, ngono, ushoga etc

Zanzibar ni nchi nzuri ya kistaarabu sana lakini naona kuna uozo unaongezeka kwa kasi kubwa.

Nyimbo na video za uchi, unywaji pombe, kuvaa vivazi vya nusu uchi hadharani n.k.

Ni muda sasa wa Zanzibar kuweka heshima ya ustaarabu wetu tupige marufuku bar zote na TV zinazopiga nyimbo za nusu uchi.
Mkifanya hivyo, Zanzibar itakuwa kama Saudia.

Saudia sheria inazuia biashara ya pombe, lakini Saudia ndiyo inayoongoza Duniani kwa kununua mitambo ya kutengenezea pombe majumbani. Ukishuka tu kwenye ndege pale King Khalid International airport unafuatwa na watu, unaulizwa kama unataka pombe ili wakuletee hotelini. Yaani uwatajie hoteli utakayofikia halafu wakuletee pombe.

Masuala ya imani aachiwe mtu mwenyewe, isipokuwa yale yenye kuwaathiri na watu wengine, hayo ndiyo yapigwe marufuku au yatengewe maeneo maalum.

Pombe inamwathiri mtumiaji mwenyewe, lakini vitu kama sigara, hata usiyevuta unaathirika kama unakuwepo kwenye mazingira ya wavutaji.
 
Kufuata maagizo ya Allah na utalii ni kipi cha muhimu zaidi?
Tofautisha unafiki na ucha Mungu.

Nilienda Zanzibar kwa mapumziko. Nikamlipa kijana Mzanzibari kwaajili ya kunizungusha mjini. Cha ajabu, akaanza kuniuliza kama nataka mwanamke ili anitafutie. Nikamdodosa mengi kuhusiana na hilo, akasema vijana wengi wamekuwa wakifanya hiyo kazi na inawasaidia wao na mabinti maana watalii wanatoa pesa nzuri!! Sikuwa na huo mpango na wala siyo jambo nililolifikiria hata wakati napanga safari yangu. Lakini hayo yapo huko Zanzibar. Je, na huo ni miongoni mwa tamaduni mnazotaka kuzilinda?

Wewe kama hunywi pombe kwa sababu ya imani yako, hutahukumiwa kwa sababu wapo wanaokunywa.

Tupo tunaoamini kuwa majini ni mashetani, lakini wapo wanaoamini majini ni viumbe safi vya kumsaidia mwanadamu. Mimi ninayeamini majini ni mashetani, sitahukumiwa kwa sababu walikuwepo waliokuwa wakiyategemea na kuyaheshimu majini.
 
Back
Top Bottom