Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Kinachonihuzunisha wala sio hotuba, bali nguvu niliotumia kushawishi jamaa zangu na kusimama foleni kumpigia kura Rais mwenye hotuba za hivi. Bora ningempigia dovutwa.

Mwenyezimungu nisamehe sana katika hili, naomba unipe uhai 2020 ni-appeal kura yangu.
 
Hatimaye mkuu wa kaya naye kaota mchana leo eti Jecha amepewe tuzo KWELI?
Nani asiyejua kuwa Jecha alibadili matokeo?
Sio CCM zanzibar wala Bara wote wanajua ya kuwa Jecha alicheza mchezo mchafu.
Atatunukiwa tuzo ya KUPORA NA KUNYANG'ANYA HAKI ZA Wanzanzibar.
Niko Unguja leo na nimesikia kesho mkuu wa kaya ATAKUWEPO kibanda mahiti kuendeleza ndoto za mchana za ajira kwa vijana,tanzania nchi ya viwanda na kutekeleza agizo la siasa mpaka 2020.
Lakini wazanzibar wengi wamesikitishwa na kauli yake ile ya "CHOKO CHOKO" na wamesema Rais wa jamhuri hapaswi kuzungumza kauli za kuligawa taifa kiasi hiki.
Naona mkuu bado anaendelea kufeli kwa kasi ya mwendokasi katika ahadi yake ya kulifanya taifa hili kuwa moja na kujenga umoja wa kitaifa.
Marais wote waliopita waliweza kumuenzi Nyerere kwa kulinda umoja wa kitaifa.
Ni nyerere pekee aliyeweza kutoa hotuba bila kuandikiwa.
 
Hizi kauli za Rais sio uchochezi kweli? [Kwa kutumia definition za watawala]
 
Naukubali sana utendaji wa Rais wangu Magufuli ,
Ila ananiangusha sehemu moja tu napo ni kwenye hotuba zake , kwa jicho la tatu uwa hazivutii kabisaa, hazifanani na kiwango chake cha elimu
Subiria siku atakapotoa au kuisoma hotuba zake kwa kidhungu, utazipenda. Kiengereza chake ndio kinapendeza, ni lugha mama nambari mbili kwa mkulu.
Kiswahili kinamchanganya kidogo.
Nimeiskiliza hotuba hii aliyoitoa Pemba imenifanya nijiulize kama mkuu ameandikiwa hii hotuba au anafyatua tu na kuchomekea maneno.

Kiongozi wa nchi analipuka kama mwehu! Shame!!
 
Ati na huyu ndio wa kushauriwa na viongozi wa dini! mmh!
 
Mpeni Mungu yaliyo yake Mungu na mpeni kaizari yaliyo yake kaizari! mungu wa mukulu je ni huyu wa isaka na yakobo aliyeumba mbingu na nchi? Nina wasiwasi mukulu ana mungu wake!
 
Mimi kufyatua watoto nimeichukulia siriazi kabisa ninaifanyia kazi maana ule haukuwa utani ile ni kazi ya watu wazima wote
Kwani alisema tufyatue watoto au alisema tufyatuane? Au wewe huoni tofauti ya misemo hiyo miwili?
 
Hii ni hutuba ya Raisi wa Tanzania au mwenyekiti wa CCM? Hii ilikua nafasi nzuri ya kuongea na wapemba Mkulu hakuitumia. Kenda kuongeza mafuta kwenye moto. Ushabiki wa kisiasa umemzidi.
 
Safi Laisi wetu, ila nadhani kuna haja ya kuwa na vigezo vipya vya wagombea urais katika nchi yetu; fluent miongoni mwao. Urais ni tunu ya juu kabisa katika nchi. Mungu ametoa dhamana kubwa kwa viongozi, hivyo tunatarajia mamlaka ya urais isiwe ikitoa kauli ambazo hukwaza watu wengine. Mungu tunusuru oir future is uncertain!
 
Nilipata nafasi ya kusikiliza sehemu ya Mh Rais Magufuli aliyoitoa kisiwani Pemba hivi majuzi. Kwa upande wangu binafsi sikuipenda kwa sababu ilikuwa zaidi ya uchochezi badala ya kuwaunganisha Watanzania. Katika hutuba zake mara kwa mara huwa anasema uchaguzi umemalizika na sasa tufanye kazi lakini yeye mwenyewe alikuwa anawasema Wananchi wa Pemba kwa kutomchagua Prof Mbarawa katika uchaguzi mkuu.Mbali zaidi alidiriki kumsifia mwenyekiti kiti wa Tume ya Uchaguzi ndugu Jecha ilihali kila mtu wa ndani na nje ya Tanzania anajua kwamba CUF walikuwa washindi . Alidiriki hata kusema Jecha apewe nishani bila ya kuwa na aibu kitu ambacho Wazanzibari wenyewe wanajua kwamba wameporwa demokrasia yao . Na hata jumuia za kimataifa hilo linaeleka kwamba demokrasia ilibakwa
Na mbali zaidi alienda mbali na kuwaita watu vichaa . Naanza kuamini kuwa hutuba nyingi za Mh Rais zina walakini .Je hii ndio sababu anayohofia ya kukutana na wanahabari wa kimataifa nje ya nchi ?
Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom