Naona kama wewe ndo ungenyamaza kimya chief, yeye ana haki ya kujitapa.
1. Anatetea kiapo chake cha kulinda Ukraine.
2. Yeye ndo amevamiwa na sio kwamba amevamia.
3. Ukubwa wa jeshi la Urusi mpaka sasa ameweza kuwadhitibiti kwa sehemu Kyiv isichukuliwe.
4. Operation toka siku 3 mpaka sasa umeingia mwezi wa 3, ongera kwake kwa ujasiri huu.
5. Ameshambulia sehemu kadhaa kwa udogo Russia, na amepiga mpaka meli bora kabisa ya kisasa ya Kirusi yenye mifumo ya S300 defence system. Jamaa kajihidi mno.
6. Amedhihirisha kuwa russia wamemtia hasara sababu inaonekana hasara amepata yeye tu ila kumbe hata Russia amepata.
7. Amefanya ulimwengu ujue mrusi kuna mda mikwara mingi kama msukuma aloshinda tatu mzuka milioni 5 kumbe vitendo hamna kitu.
Mwisho kabisa huu ndo uanaume, sio unavamiwa na baunsa unakuwa mnyonge kumtoa mkeo na familia, mwanaume lazima upambane.