Ziara ya Rais kwenye nchi moja (US) kwa zaidi ya siku 5 haina tija. Muda mwingi wapo "idle" hotelini

Ziara ya Rais kwenye nchi moja (US) kwa zaidi ya siku 5 haina tija. Muda mwingi wapo "idle" hotelini

Wewe usiwe bwege, utaitaje IKULU ya magogoni hotel!!
Hakuna shuhuri yeyote ya maana waliyokuwa wanafanya hotelini bali ni kulala na kuzubaa tu!
Sawa muhishimiwa Bwege.Nikuulize swali.Hivi nyumba yenye choo ndani unaweza kuiita choo?
 
Nyie washamba mkifika New York mnashangaa shangaa tu huku Sisi mnatuzuga kuwa mnafanya kazi!! Hiyo asali karibu mtaiharisha siku si nyingi!
Kushangaa mabugando ni muhimu.Tupo makini na snipers.Na asali italambwa hadi muone wivu.Kazaneni kula matobholwa kwa nsansa!😂😂😂😂
 
Ndugu zangu,

Mnamo tarehe 13.04.2022 Rais Samia amekuwa katika ziara nchini Marekani akiambatana na "delegation" kubwa sana ya watumishi wa serikali.

Kama Rais alipaswa aende US kwa mambo ambayo ni "specific " na sio kukaa huko akisubiri matukio.

Kuna udhaifu mkubwa kwa wizara ya mambo ya nje wanaoratibu ziara hizi, Rais anakosa cha kufanya akisubiri matukio ambayo yapo siku za mbele. Wao wanaangalia posho zao na sio tija ya ziara ya Rais.

Siku zaidi ya tano kwa Rais kuzuru nchi moja humfanya kuwa "iddle" muda mwingi asiwe na cha kufanya.

Ni matumaini yangu udhaifu huu utarekebishwa.
Ndio alichopanga na ndio uwezo wake au ndio mpango mzima wao sio mazuzu, they had their schedule before safari, the kind of a person who she is and her crews define everything. Watanzia akili sifuri kama wenye akili wapo wanaogopwa, wanaonewa wivu, hawapo kwenye mfumo, wanabaguliwa etc. Ila overall ranking ya Watanzania ni poor kichwani, madomo zege, mazembe, hayako organized, wivu kila kitu, they don't think for collective good future in all aspects, even their individual they can't think 20-30-40-50 yrs , barely one may come up with a sustainable family welfare. Huo utopolo walioenda nao Marekani wao wapo kwenye shughuli za bata.
 
Mwamba umewaumbua kunguni na viroboto wa mapambio watakuja wengi kupopoma, kudos Mwamba, what a classic observation of national interest. Long live Long live!
 
Du mzee mtoa mada je umetumwa au? Ratiba ya Rais unayo? au unahisi tu? Tuache kutoa hoja zisizo na mashiko hapa.
 
Kama Rais alipaswa aende US kwa mambo

Toka maktaba :

15 April 2022
Washington DC USA

SAFARI YA KIKAZI YA MH. RAIS SAMIA HASSAN, KUTOA MHADHARA WORLD BANK

Rais Samia Suluhu Hassan kutoa mhadhara katika mkutano wa Benki ya Dunia tarehe 23 April 2022 jijini Washington Marekani


President%20Samia%20Suluhu%20Hassan.jpg

Samia Suluhu Hassan​

President of United Republic of Tanzania
Latest or upcoming appearance: April 23, 2022 source : Samia Suluhu Hassan | World Bank Live

Human Capital at the Crossroads: Reversing the Losses, Reclaiming our Future

Putting people first through investing in human capital – the knowledge, skills, and health that people need to achieve their potential – is critical for sustainable, inclusive growth and poverty reduction. The consequences of the COVID-19 pandemic threaten to leave generations behind and exacerbate inequalities. Health impacts, setbacks to nutrition, the early years and learning, job losses and expanding gender gaps must be addressed with urgency.

Countries have stepped up in innovative ways to put people first through building, protecting, and utilizing human capital – with support from the World Bank and partners. However – ambition, innovation, and sustained support are needed to recover human capital losses and strengthen recovery. Investing in people consistently and providing opportunities for all to achieve their potential can yield economic dividends – and help bring greater stability in a challenging global context.


Source : The 2022 World Bank Group Spring Meetings: Strengthening the case for globalism
Source :
 

Wednesday, April 20, 2022

Wisconsin, USA

KAMPUNI YA SC JOHNSON YA MAREKANI KUSAIDIA TANZANIA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Dkt. H. Fisk Johnson Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SC Johnson Family wakati alipotembelea kiwanda kinachotengeneza Viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti Wadudu wanaodhuru waenezao Magonjwa mbalimbali kilichopo katika Mji wa Racine ulioko jimbo la Wisconsin nchini Marekani 19 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan 19 Aprili,2022 ametembelea Kampuni ya SC Johnson (SC Johnson Institute of Insectice Science for Public Health) inayojishughulisha na Utafiti wa Wadudu Dhurifu waenezao Magonjwa katika Mji wa Racine ulioko jimbo la Wisconsin nchini Marekani na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Dkt.Fisk Johnson.

Katika mazungumzo hayo, Rais Samia alieleza kuwa Malaria bado ni changamoto nchini Tanzania na kuwa asilimia 94 ya Watanzania wapo katika hatari ya kupata maambukizi katika kipindi cha mwaka nzima.

Aidha, Rais Samia alieleza jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau ikiwemo kugawa vyandarua bure kwa wajawazito na watoto wa umri ya chini ya miaka 5, kupuliza dawa ukoko ya kuuwa mbu katika Halmashauri zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria, kutoa huduma za uchunguzi na matibabu pamoja na kufanya tafiti na ufuatiliaji wa mbu na wagonjwa wa Malaria.

Hata hivyo Rais Samia alieleza kuwa bado wananchi wa maeneo mbalimbali nchini Tanzania wanakosa huduma za uchunguzi na Matibabu ya Malaria kutokana na kukosekana kwa vituo vya kutoa huduma za Afya pamoja na uchache wa rasilimali za kugharamia mapambano dhidi ya Malaria.

Akiongea katika mazungumzo hayo, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa SC Johnson Dkt. Fisk Johnson alieleza kuwa lengo kuu la kampuni hiyo ni kuboresha maisha ya watu.

Kampuni hiyo ya kifamilia iliyoanzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita imekubali kusaidia Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malaria katika maeneo mbalimbali ikiwemo kusaidia ujenzi wa vituo vya msingi vya kutoa huduma za afya (Zahanati) katika Mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya Malaria.

Vilevile, wameahidi kusaidia kuboresha miundombinu katika chuo cha udhibiti wa wadudu dhurifu waenezao magonjwa kilichopo Muheza, Mkoani Tanga (Muheza Vector control training centre) pamoja na kusaidia uboreshaji wa miundombinu kwa kushirikiana Utaalamu na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) pamoja na Taasisi ya Afya ya Ifakara.

Katika ziara hiyo Mhe.Samia alipata kutembelea kiwanda cha Kampuni hiyo

Source : KAMPUNI YA SC JOHNSON YA MAREKANI KUSAIDIA TANZANIA MAPAMBANO DHIDI YA MALARIA
 

Tuesday, April 19, 2022

RAIS SAMIA SULUHU ATEMBELEA KIWANDA CHA SC JOHNSON FAMILY CHICAGO NCHINI MAREKANI





IMG-20220419-WA0049.jpg
IMG-20220419-WA0047.jpg
IMG-20220419-WA0045.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akitembelea Kiwanda cha SC Johnson Family kinachotengeneza Viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti Wadudu dhurifu waenezao Magonjwa mbalimbali kiliopo katika mji wa Chicago Nchini Marekani leo tarehe 19 Aprili 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiangalia baadhi ya Wadudu wa aina mbalimbali waliodhibitiwa, alipotembelea moja ya Kiwanda cha SC Johnson Family kinachotengeneza Viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti Wadudu dhurifu waenezao Magonjwa mbalimbali kiliopo katika mji wa Chicago Nchini Marekani leo tarehe 19 Aprili 2022.
IMG-20220419-WA0048.jpg
IMG-20220419-WA0044.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Dkt. H. Fisk Johnson Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SC Johnson Family na Ujumbe wake, kabla ya kutembelea Kiwanda cha SC Johnson Family kinachotengeneza Viuatilifu kwa ajili ya kudhibiti Wadudu dhurifu waenezao Magonjwa mbalimbali kiliopo katika mji wa Chicago Nchini Marekani leo tarehe 19 Aprili 2022.
IMG-20220419-WA0042.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akipata maelezo kuhusu namna ya kudhibiti Wadudu dhurifu waenezao Magonjwa mbalimbali, alipotembelea moja ya Kiwanda cha SC Johnson Family kiliopo katika mji wa Chicago Nchini Marekani leo tarehe 19 Aprili 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa na Dkt. H. Fisk Johnson Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SC Johnson Family, wakati alipomtembelea kiwanda cha bidhaa mbalimbali za Viuatilifu kiliopo katika mji wa Chicago Nchini Marekani leo tarehe 19 Aprili 2022.

source : habari na picha kwa hisani kubwa ya : RAIS SAMIA SULUHU ATEMBELEA KIWANDA CHA SC JOHNSON FAMILY CHICAGO NCHINI MAREKANI
 
ZIARA YA KIKAZI YA MH RAIS SAMIA HASSAN NA UJUMBE WAKE UNAOJUMUISHA MAWAZIRI WAENDELEA KUHUDHURIA MIADI MBALIMBALI

Tuesday, April 19, 2022

BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUISAIDIA ZAIDI TANZANIA KUFUFUA UCHUMI




Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (hayupo pichani), wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bi. Sauda Msemo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (hayupo pichani), wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa Tanzania kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (hayupo pichani), wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bi. Sauda Msemo, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem (hayupo pichani), wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Na Benny Mwaipaja, Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuahidi kuisaidia Tanzania kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na madhara ya UVIKO-19 na vita vinavyoendelea baina ya Urusi na Ukraine.

Dkt. Nchemba amesema hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, wakati wa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), inayoendelea Jijini Washington DC, Marekani.

Alimweleza Kiongozi huyo kwamba Tanzania inafanya kila njia kuhakikisha kuwa uchumi wake ulioathiriwa na matukio hayo unarejea katika hali ya kawaida kwa kutafuta rasilimali fedha na kuzielekeza kwenye sekta zitakazochochea ukuaji wa uchumi ikiwemo kilimo, na kuimarisha sekta binafsi.

‘Tumepokea taarifa ya namna Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) linavyokusudia kufufua uchumi wetu kwa kuwekeza kwenye sekta za uzalishaji ikiwemo kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na kuisaidia sekta binafsi hususan wajasiriamali wakiwemo wamachinga” alisema Dkt. Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na wataalam wa Benki ya Dunia, IMF na Benki ya Maendeleo ya Afrika, watakutana ili kupitia maeneo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili utekelezaji wa miradi hiyo ianze mwaka mpya wa fedha 2022/2023.

“Tuna maeneo yanayohitaji uangalizi wa karibu yakiwemo ya mfumuko wa bei, kupanda kwa bei za bidhaa ambayo ni muhimu kwa wananchi wetu na yanahitaji Serikali ipunguze kodi na fidia ya fedha hizo zinatakiwa zipatikane kutoka kwenye vyanzo vingine, kama tunavyoendelea na mijadala hii” Aliongeza Dkt. Nchemba.

Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, anayesimamia nchi za Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika, Dkt. Hafez Ghanem, alipongeza mabadiliko makubwa ya kisera na kiuchumi yanayoendelea nchini Tanzania, ambayo anaamini yatasaidia kukuza uchumi wa nchi na wananchi wake.

Aliahidi kuwa Benki yake itaisaidia Tanzania, Pamoja na nchi nyingine za Afrika kukabiliana na athari za majanga ya ugonjwa wa Uviko na Athari za Vita vya Ukraine na Urusi vilivyosababisha kupanda kwa bei za bidhaa zikiwemo bei za mafuta na vyakula duniani kote.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba yuko nchini Marekani akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa – IMF, ambayo imewakutanisha Magavana wa Taasisi hiyo, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi ambapo dhima kubwa ya mwaka huu ni kuchambua na kutoa mapendekezo ya namna ya kufufua uchumi wa nchi ulioathiriwa na matukio hayo.

Source : habari na picha kwa hisani kubwa: BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUISAIDIA ZAIDI TANZANIA KUFUFUA UCHUMI
 

Tuesday, April 19, 2022

New York city, US

RAIS SAMIA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TEHAMA



Na Benny Mwaipaja, New York
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka watanzania hususan Vijana, kuchangamkia fursa za maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Mhe. Rais ametoa wito huo Mjini New York nchini Marekani, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati alipozindua Mtandao wa NALA (NALA APP) utakaotumiwa na watanzania waishio Marekani kutuma fedha nchini Tanzania kidijitali.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akimpongeza Bw. Benjamin Fernandes ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kidigitali ya NALA, baada ya kuzindua NALA APP inayotumika kutuma fedha kidigitali kutoka nchini Marekani na nchi nyingine duniani, kwa niaba ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, Jijini New York nchini Marekani.

Alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NALA, Raia wa Tanzania, Bw. Benjamin Fernandes na Timu yake, kwa kubuni Application hiyo ambayo itarahisisha utumaji wa fedha kutoka nchini humo kwenda Tanzania hatua ambayo itasissimua uchumi wa nchi na kuharakisha maendeleo ya wananchi watakaofaidika na huduma hiyo.

“Benjamin Fernandes na Timu yako ni miongoni mwa vijana wabunifu waliojikita katika masuala ya teknolojia ambao Serikali inawaunga mkono hususan wakati huu ambapo nchi inajenga uchumi wa kidijitali ambao matokeo yake yanatarajwa kuwa ni kukuza ajira, kuchangia pato la Taifa na kukabiliana na changamoto zote za kiuchumi na kijamii” Alisema Dkt. Nchemba.

Alisema kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi kwenye miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa kujenga mkongo wa Taifa uliounganishwa na nchi nyingine za kiafrika zikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya, Malawi, Uganda na Zambia na hivi karibuni nchi za DRC na Msumbiji zitaunganishwa.

Dkt. Nchemba alitoa wito kwa wawekezaji kwenye sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kuwekeza nchini Tanzania na kufaidi mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo nchi imeweka ili kuvutia mitaji na teknolojia.

Aliahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizoainishwa na uongozi wa Kampuni hiyo katika masuala ya upatikanaji wa leseni za kuendesha shughuli za TEHAMA ili kuwatia moyo vijana wabunifu wawekeze kwenye teknolojia zinazoweza kuchangia ukuaji wa matumizi ya teknolojia katika kuongeza kipato cha wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Nimefahamishwa kwamba Marekani imewekeza karibu dola bilioni 1.5 katika Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Barani Afrika, ninatamani kuona kuwa Tanzania inakuwa ni moja ya nchi zitakazonufaika na uwekezaji huo” Alisisitiza Dkt. Nchemba katika Hotuba yake akimwakilisha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Benjamin Fernandes alisema kuwa Application iliyozinduliwa nchini Marekani, inafanyakazi katika nchini nyingine 9 duniani na aliibuni kwa ajili ya kusaidia utumaji wa fedha kwa nchi za Afrika.

Aidha, Bw. Fernandes aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza masharti ya leseni ya biashara ya mitandao ili kuwawezesha vijana wengi wabunifu wa TEHAMA, kuwekeza nguvu zao kwa kuwa itaongeza ajira na kukuza uchumi wao.
Alifafanua kuwa hivi sasa mtu anayetaka kutoa huduma ya kibunifu analazimika kulipia leseni Benki Kuu ya Tanzania hata bila kuanza kufanyakazi hatua ambayo alisema inawakwaza vijana wengi kutimiza ndoto zao za kujiajiri na kuwaajiri watu wengine
Source : RAIS SAMIA AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA TEHAMA
 
WWe
Ndugu zangu,

Mnamo tarehe 13.04.2022 Rais Samia amekuwa katika ziara nchini Marekani akiambatana na "delegation" kubwa sana ya watumishi wa serikali.

Kama Rais alipaswa aende US kwa mambo ambayo ni "specific " na sio kukaa huko akisubiri matukio.

Kuna udhaifu mkubwa kwa wizara ya mambo ya nje wanaoratibu ziara hizi, Rais anakosa cha kufanya akisubiri matukio ambayo yapo siku za mbele. Wao wanaangalia posho zao na sio tija ya ziara ya Rais.

Siku zaidi ya tano kwa Rais kuzuru nchi moja humfanya kuwa "iddle" muda mwingi asiwe na cha kufanya.

Ni matumaini yangu udhaifu huu utarekebishwa

Ndugu zangu,

Mnamo tarehe 13.04.2022 Rais Samia amekuwa katika ziara nchini Marekani akiambatana na "delegation" kubwa sana ya watumishi wa serikali.

Kama Rais alipaswa aende US kwa mambo ambayo ni "specific " na sio kukaa huko akisubiri matukio.

Kuna udhaifu mkubwa kwa wizara ya mambo ya nje wanaoratibu ziara hizi, Rais anakosa cha kufanya akisubiri matukio ambayo yapo siku za mbele. Wao wanaangalia posho zao na sio tija ya ziara ya Rais.

Siku zaidi ya tano kwa Rais kuzuru nchi moja humfanya kuwa "iddle" muda mwingi asiwe na cha kufanya.

Ni matumaini yangu udhaifu huu utarekebishwa.
Ulipolamba ka Unaibu Waziri ulikuwa huongei! Leo uko bench ndo unajifanya kujua kuwa watu wanalamba posho za Bure! Acha Wivu wewe Bidada.
 
Ndugu zangu,

Mnamo tarehe 13.04.2022 Rais Samia amekuwa katika ziara nchini Marekani akiambatana na "delegation" kubwa sana ya watumishi wa serikali.

Kama Rais alipaswa aende US kwa mambo ambayo ni "specific " na sio kukaa huko akisubiri matukio.

Kuna udhaifu mkubwa kwa wizara ya mambo ya nje wanaoratibu ziara hizi, Rais anakosa cha kufanya akisubiri matukio ambayo yapo siku za mbele. Wao wanaangalia posho zao na sio tija ya ziara ya Rais.

Siku zaidi ya tano kwa Rais kuzuru nchi moja humfanya kuwa "iddle" muda mwingi asiwe na cha kufanya.

Ni matumaini yangu udhaifu huu utarekebishwa.
Tanganyika acheni nongwa JK alikaa ulaya karibu miezi 3 kwa issue ya Tenzi dume wakati mahospitali kiba Tanzania yalikuwa nanafanya hiyo operation kw mafanikio makubwa sana., ni vile mama munanchuki lakini bado atakuwepo
 
Back
Top Bottom