Ziara ya Rais Samia Nchini Norway baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo, Februari 13, 2024

Ziara ya Rais Samia Nchini Norway baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo, Februari 13, 2024

Afu kuna mjinga 1 Kaja na mada ya CHADEMA wasitishe maandamano kisa kuna msiba wa Lowasa
Huku mkuu wa nchi wala hana habari na huo msiba
 
View attachment 2902967
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo, tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902968
View attachment 2902970
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya mapokezi yake katika Kasri la Kifalme, Oslo nchini Norway tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902976
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Mfalme Harald V wa Norway pamoja na Malkia Sonja mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo kwa ajili ya ziara ya Kitaifa, tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902978
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Mfalme Harald V wa Norway mara baada ya kukabidhiana zawadi katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo, tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902979
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akimpa zawadi Malkia Sonja mara baada ya kuwasili katika Kasri la Kifalme, Norway wakati wa ziara yake ya Kitaifa, tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902980
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima kabla ya kuweka shada la maua katika Mnara wa Kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway, tarehe 13 Februari, 2024.

View attachment 2902981
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu wa Taifa, Oslo nchini Norway, tarehe 13 Februari, 2024.
Naona Mfalme yupo na Malikia , yeye yupo Pekee yake. Protocol ina semaje hapo .
 
Afu anapiga sana misele huyu mama si atulie nyumbani uku.
kiufupi wapinzani huwa hamueleweki mnataka nini, Magu alipokuwa haendi ulaya mkamsema vibaya, huyu anaenda mnamasema vibaya, Mnaboa Sana, hamna hoja, mnaishi Kwa matukio Tu.
 

The Oslo Energy Forum 2024​

Wednesday 14. February​


Creating Action for Transformational Change – business and political views
Opening session by
  • Jonas Gahr Støre, Prime Minister, Norway
  • Samia Suluhu Hassan, President, Tanzania
  • John Kerry, Special Presidential Envoy for Climate, USA
  • Anders Opedal, Chair OEF / President & CEO of Equinor
OSLO ENERGY FORUM 2024

1707927847858.png


United States Special Presidential Envoy for Climate John Kerry speaks during the Oslo Energy Forum, which is held at the Scandic Holmenkollen Park hotel in Oslo, Norway, 14 February 2024. The forum, aiming to encourage a productive discussion on the most critical energy issues and solutions, runs from 13 to 15 February 2024.

Source - Agência de Notícias de Portugal, S.A.
 
14 February 2024
Oslo, Norway

Masuala makuu matatu yanayobeba sekta ya nishati yajadiliwa

Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mkutano wa Nishati Jadidu Clean Energy mjini Oslo Norway akitoa mada,

1707928123760.png

Jukwaa la Nishati la Oslo linaunganisha viongozi katika tasnia inayohusiana na nishati ulimwenguni na biashara zingine na wawakilishi kutoka kwa sekta za nishati ambao ni watunga sera, mamlaka, wadhibiti na taasisi zinazoathiri hali na fursa za mipango kazi ya makampuni.

Masuala makuu matatu katika sekta ya nishati - yaani usalama, uendelevu, na uwezo wa kumudu - yanajadilwa kwa kina kuona changamoto zake katika hali ya kisasa ya kijiografia kuliko hapo awali.

1707928659930.png

Oslo Energy Forum connects leaders in global energy-related industry and other businesses with representatives from authorities, regulators and institutions influencing the companies’ framework conditions and opportunities.

Kwa hisani kubwa ya :
Source - Agência de Notícias de Portugal, S.A.
 
Tunakula mema ya inchi baada ya hapo sisi haooo kizimkazi na pensheni tele kigumu chama chama Cha mapumbavu
 
Mh. Rais Dr. Samia Siuluhu Hassan akiwasili na kupokelewa kwenye kongamano la nishati mjini Oslo Norway

1707930422944.png

Picha :
Kwa hisani kubwa ya :
Source - Agência de Notícias de Portugal, S.A.
 
Na iki ndio anacho weza.
TAIFA halina umeme
TAIFA halina sukari
 
Mwache apigwe na baridi,dar joto Sana.🤣🤣🤣🤣
 
Kwani mizunguko yote hiyo anachokitafuta ni kipi imekua too much sasa
 
kiufupi wapinzani huwa hamueleweki mnataka nini, Magu alipokuwa haendi ulaya mkamsema vibaya, huyu anaenda mnamasema vibaya, Mnaboa Sana, hamna hoja, mnaishi Kwa matukio Tu.
Ndio maana aliwanyoosha….😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
SSH Yupo kwenye vitu anavyovipenda, makongamano, seminars, kukutana na,wafalme, watu mashuhuri, watu maarufu, Viongozi hasa wakubwa duniani. Ni asili yake. Kula bata. Hivi kwanini haendi na mume wake?

Matatizo ya wananchi, matatizo makubwa ya nchi, bajeti, kusoma taarifa muhimu anaona wanamsumbua tu, ngoja nikale bata. Nitawaachia mawaziri. Nikirudi vitu vitakuwa sawa.

Usimwambie asome taarifa kuhusu umeme, maji, nauli, mfumuko wa bei, au atembelee Tanesco, awawajibishe Wizara ya nishati, hana huo muda ila ana muda wa kutembea ulaya, US, Middle east.
 
Kuna mgauni naskia unatajwa takwa sana kwamba ndio upitishwe kama vazi la taifa.....😜
 
Ziara hii imeacha gumzo katika wafuatiliaji wa taarifa za shughuli za kifame (Royal Tours) za wafalme na malkia wa bara la ulaya.

Tanzania imetumia soft power (nguvu isiyoumiza) vizuri kupitia Royal tour hii ya mwaliko wa King Harald V wa Norway
 
Back
Top Bottom