Ziara ya Rais Samia: Watanzania waishio Marekani waandamana kudai Katiba Mpya

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Your browser is not able to display this video.


Kufuatia Ziara ya rais Samia huko Marekani, wananchi waishio huko wameandamana kudai katiba mpya.

Watanzania hao walibeba mabango yenye ujumbe wa Kudai katiba mpya na Wengine kubeba mabango yanayotaka serikali imwachie huru Mwanasheria Peter Madeleka ambaye inasemekana amekamatwa na Polisi lakini hajulikani alipo(Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi)

Pia walivaa T-Shirt zinazotaka haki itendeke kwa Ben Saanane, Azory, Gwanda etc

Hapo juu nimeweka video ya maandamano hayo huko Marekani

Pia soma;


WATANZANIA WAANDAMANA MAREKANI

Baadhi ya Watanzania wamejitokeza nje ya Ubalozi wa Tanzania Nchini #Marekani na kufanya maandamano wakiwasilisha madai mbalimbali

Baadhi ya madai yao waliyoandika kwenye mabango yao ni Mabadiliko ya Katiba na kuachiwa huru kwa Wakili Peter Madeleka pamoja na kufukuzwa Bungeni Wabunge 19 wanaodaiwa kuwa Bungeni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
 
Safi sana.Natamani huo Moto ungeshika kasi mpaka huku nangulukulu ingekuwa poa sana.
 
Watanzania waishio Marekani katika mji wa Washington waliandamana kuelekea kwenye jengo la ubalozi wa Tanzania mahali ambapo Rais Samia alikuwa akiwahutubia Watanzania.



Kwa bahati mbaya wazee wa itifaki waliona mapema kikundi hicho na kuamua kudivert through narrow way into the conference area, inaonekana hakupitia mlango wa kawaida.

Baada ya kuongea mambo kadha wa kadha Rais Samia amesikika akisema, “Nimewaona wanangu nje wakiwa wamevaa t- shirt na wameshika mabango na nimewasalimia”.

Maneno hayo ni tofauti na maneno mtu ambaye amesoma mabango na kuongea.
 
Wakayapambe kwenye nyumba zao.
 
Waambie wakazane kuandamana
 
Hizo puc ni za mda mrefu Peter madeleka ameshatoka kitamvo yuko mtaani
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…