Ziara ya Rais Samia: Watanzania waishio Marekani waandamana kudai Katiba Mpya

Haikuwa sahihi kwa Rais kuwakimbia wananchi hawa wachache kwa kutokomea kupitia mlango wa nyuma wa jengo. Kiongozi bora ni yule anayesikiliza wananchi wake, bila kujali ni wanamuunga mkono au wanampiga, bila kujali wako upande wa chama tawala au nje ya chama tawala, wote hawa ni wanannchi wa Tanzania na kama wanatanzania wanayo haki ya kusikilizwa, si lazima wakubaliwe wanachosema/wanachotaka cha muhimu wasikilizwe.

Rais na wasaidizi wake wanapaswa waanze kujenga utamaduni wa kuwasilikiza wananchi wao hasa wanapokuwa ziarani, wanapaswa watoe majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara, wakishindwa au kukwepa kutoa majibu ni dhahiri kwamba watapata shida sana kuwaongoza wananchi wao wanaowaongoza. Viongozi wanapokwepa kuwasikiliza wananchi wao wanaonesha na kudhihirisha udhaifu mkubwa wa kiuongozi na kiutendaji walionao.
 
Mkuu mpaka akili ziwe sawasawa ndipo unaweza kufanya kitu kama ulichoandika.

Afrika hatukupewa ujasiri wa kuonyesha wazungu kuwa tunaweza ila ujasiri wetu ni wa kuharibu na kuuana tu.
 
sahihi
 
Kweli aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…