Ziara ya Rais Samia: Watanzania waishio Marekani waandamana kudai Katiba Mpya

Ziara ya Rais Samia: Watanzania waishio Marekani waandamana kudai Katiba Mpya

Lost opportunity. Angesimama na kuongea nao ili athibitishie ulimwengu kuwa ni muumini wa uhuru wa kutoa mawazo kama sehemu ya demokrasia. Aidha, ingekuwa ishara kuwa yeye ni tofauti na waliomtangulia.

Amandla....
Kukaa mno ugenini hayo pia ni madhara na doa kwa Amiri jeshi mkuu.
Siku nyingine pangeni ratiba za kipresidential
 
Ni baadhi ya Watanzania tena wachache siyo Watanzania wanaoishi Marekani. Weka usahihi wa taarifa yako. Si umesema wengine walikuwa ndani Rais akiwahutubia! Ni haki yao ila . muhimu ni; mambo ya Tanzania yataamuliwa Tanzania siyo Washington wala 10 Downing street.[emoji120][emoji120][emoji120]
Kama ni hivyo, mbona raisi anahangaika kuongelea mambo ya Tanzania huko Marekani?
 
Safi sana diaspora, mawaziri Mwigulu Nchemba, Pindi Chana na maofisa wengine wa serikali wameona kwa macho yao wenyewe mabango na sauti za kudai katiba mpya.

Pongezi kwa diaspora kwa kuwakilisha wananchi wengi wanaoandamana ndani ya mioyo yao kudai katiba hapa JF, mitandaoni na ktk makongamano ya ndani.
 
Kesho katika taasisi tajwa ya the Wilson Center , mheshimiwa Rais atakuwepo kujibu masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa, demokrasia, afya, elimu Tanzania




Upcoming schedule for

Monday
April 25, 2022
11:00am – 11:45am ET

A New Day for U.S.-Tanzania Relations: A Conversation with H.E. Samia Suluhu Hassan, President of the Republic of Tanzania​

1650798590581.png

A Conversation with H.E. Samia Suluhu Hassan, President of the Republic of Tanzania. President Samia will share her vision for Tanzania and U.S.-Tanzania relations, and sit in conversation with Ambassador Mark Green, President and CEO of the Wilson Center and former U.S. Ambassador to Tanzania from 2007-2009, to discuss key challenges and opportunities for the future of U.S.-Tanzania relations in various spheres.

The Africa Program works to address the most critical issues facing Africa and U.S.-Africa relations, build mutually beneficial U.S.-Africa relations, and enhance knowledge and understanding about Africa in the United States. The Program achieves its mission through in-depth research and analyses, including our Africa Up Close blog, public discussion, working groups, and briefings that bring together policymakers, practitioners, and subject matter experts to analyze and offer practical options for tackling key challenges in Africa and in U.S.-Africa relations.

source : Africa Program
 
24 April 2022
Washington DC
Marekani

RAIS SAMIA ATIMUA MBIO KUWAKWEPA WATANZANIA MAREKANI



Source : TanAfrika TV
 
Kama ni hivyo, mbona raisi anahangaika kuongelea mambo ya Tanzania huko Marekani?
Rais ameenda kuzungumzia international trade; kwa kunadi fursa zetu za utalii na uwekezaji vitu ambavyo ni tofauti na political sovereignty. 🙏🙏🙏
 
Kikundi cha watu 10..hata hawana athari kabisa
Wewe unataka athari gani? Ya kuteka na kupoteza watu? Wao wanafikisha ujumbe, wewe unataka athari (sijui ni hasi au chanya).
 
Watanzania waishio Marekani katika mji wa Washington waliandamana kuelekea kwenye jengo la ubalozi wa Tanzania mahali ambapo Rais Samia alikuwa akiwahutubia Watanzania.

View attachment 2198353
View attachment 2198354
Kwa bahati mbaya wazee wa itifaki waliona mapema kikundi hicho na kuamua kudivert through narrow way into the conference area, inaonekana hakupitia mlango wa kawaida.

Baada ya kuongea mambo kadha wa kadha Rais Samia amesikika akisema, “Nimewaona wanangu nje wakiwa wamevaa t- shirt na wameshika mabango na nimewasalimia”.

Maneno hayo ni tofauti na maneno mtu ambaye amesoma mabango na kuongea.

..hiyo ilikuwa ni bonge ya FURSA kwa Maza ila ameshindwa kuitumia.


..Maza alitakiwa apite mbele ya hao waandamanaji na asome mabango na hata kuteta nao kidogo.

..angefanya hivyo hata mabeberu nao wangeunga mkono kwamba Maza anaupiga mwingi kwamba ana uvumilivu wa kisiasa.

..kitendo cha Maza kupitia mlango wa uani kilikuwa na ushauri mbaya. Uani kuna mambo mengi, Maza angeweza kupata ajali.
 
Kukaa mno ugenini hayo pia ni madhara na doa kwa Amiri jeshi mkuu.
Siku nyingine pangeni ratiba za kipresidential
Ratiba za kipresidential ndio zikoje na zinahusika vipi kwenye hili?

Amandla...
 
Hili jambo ni muendelezo wa kutaka ushindi wa asilimia 100 katika kila jambo. Kwa imani hiyo utajiaminisha kuwa hakuna raia wenzako wenye mawazo tofauti na yako yanayostahili kusikilizwa!

Amandla...
 
View attachment 2198349

Kufuatia Ziara ya rais Samia huko Marekani, wananchi waishio huko wameandamana kudai katiba mpya.

Watanzania hao walibeba mabango yenye ujumbe wa Kudai katiba mpya na Wengine kubeba mabango yanayotaka serikali imwachie huru Mwanasheria Peter Madeleka ambaye inasemekana amekamatwa na Polisi lakini hajulikani alipo(Jeshi la Polisi halijatoa taarifa rasmi)

Pia walivaa T-Shirt zinazotaka haki itendeke kwa Ben Saanane, Azory, Gwanda etc

Hapo juu nimeweka video ya maandamano hayo huko Marekani
 
Back
Top Bottom