Zitto: Hata kesi ya Mbowe ni jumba bovu kwa awamu ya 6. IFUTWE!

Zitto: Hata kesi ya Mbowe ni jumba bovu kwa awamu ya 6. IFUTWE!

Huyu mama yenu akija kushtuka ataelewa amezungukwa na wapambe waliojaa unafiki! huku wakimuaminisha maadui wake ni upinzani.

Jiwe alidhani maadui zake ni kina Mbowe ila kumbe waliomzunguka ndio walikua maadui zake wakuu..

Je mshawahi kujiuliza why yule jamaa aliweza kupata access ya medical sensitive medical information ya kuwa Jiwe ana pacemaker?
Mengine uko sahihi. Hiyo ya pacemaker sio kitu nyeti. Nibtaarifa za kawaida kimatibabu hata watoto wake ndugu na marafiki wanajua. Sio jambo la kushangaza
 
Watu wanashauriana mambo mabaya wakiwa watupu kama walivyokuja Duniani halafu wanaanza kulalamika.

Mbowe anapaswa kuachiwa huru,kuombwa msamaha na kulipwa fidia ya kudhalilishwa na kuchafuliwa jina na wana-ccm na serikali yao!
Wahuni waliomwingiza Chaka Magufuli Mama kawashtukia
 
Washabik wa chato wameangushiwa kitu kizoto chenye ncha kali
 
Kesi ya kubumba ya Mbowe inaivua nguo serikali na kwa kweli ni hujuma dhidi ya utawala wake. Kesi hii imewaudhi mno na inawakera watanzania wote, wapinzani na wana CCM na inamweka Rais Samia katika mizani sawa na Fashisti Magufuli. Ni kesi inayoharibu tashwira ya Mahakama, Polisi na Majaji. Hoja iliyowasilishwa karibuni katika Bunge la Ulaya ya kuiponda kesi hii imedhihirisha namna kesi ya kijinga hii inavyoligharimu Taifa! Naungana na Mh. Zitto kwamba Kesi hii ni jumba bovu inayolinufaisha na kulifurahisha genge la kihuni la Mwendazake. Kwa vyovyote vile haina maslahi kwa Taifa wala Utawala wa awamu ya Mama Suluhu.
 
KUANZA UPYA SI UJINGA .
Serikali yake inatokana na ile yenye genge linaloangusha gari bovu. Hawezi kamwe kujitenga na genge hilo.

Hata anapojaribu kujitenga na genge, yale anayoonekana kuyasimamia yeye hata wasiokuwa kwenye genge nao wanaona kama anaanzisha genge jingine lisilokuwa na maslahi ya wananchi.

Kwani amesikiliza wananchi wanasemaje juu ya serikali yake?

Ajikite zaidi kusikiliza upande huo ili apate kujua picha sahihi ya hisia za wananchi juu ya serikali yake.
 
Mama amaenza kutambua ukweli kuwa kesi ya Mbowe ni jumba bovu wanataka adhalilike yeye.

Majaji wa Mwendakuzimu akina Siyani, Liganga na wenzake mmesikia hilo?
Hivi hao ndondocha wanasikiaga? Labda siku zamu yao ikifika ndio watasikia...
 
Mama Hana kifua na nafasi kuhifadhi visasi na roho mbaya, tumsamehe na kumuombea alikuwa na mashinikizo makubwa wafuasi wa mwenda zake.
Hivi Magufuli kama kwl ndy aliyekuwa na visasi?
Hivi mbowe kakamatwa wakati wa Magufuli?

Hivi wale uamsho walitolewa na nani mahabusu?
Na kama waliopo madarakani wanafata ya Magufuli kuna Mambo mangapi ya Magufuli ,, wameyageuka?

Walishindwa nn kutokumkamata mbowe na kumpa kesi ya ugaidi?
Mbowe amematwa na kupewa kesi ya ugaidi kila mtu anafahamu tatizo ni nn?
Tatizo ni kudai katiba mpya,,tena walisema wataitisha maandamano bila kikomo inchi nzima.
Hilo pia sababu ni Magufuli?

Ama kweli marehemu Hana haki..
Atasingiziwa kila kinachotokea hapa Tanzania.
Tuwache siasa za kinafiki,,tuwe wakweli.

Ifike kipindi ukweli usemwe na sio kumsingizia Magufuli kila kukicha..
 
Back
Top Bottom