Zitto: Hata kesi ya Mbowe ni jumba bovu kwa awamu ya 6. IFUTWE!

Magufuli hakwepi lawama za kesi ya Mbowe. Wenzake na Mbowe wako ndani tangu 2018
 
Zitto ni. tatizo sana, ameshasahau kama aliwahi kubishana na MMM twitter kuhusu hii kesi akidai alipanga mipango miovu na Mbowe.
Zitto ni mjumbe katuletea ujumbe kwani ameshajua yatakayojiri ..
Sisi tusubirie majibu kutoka kwa Mama
 
Kesi ya Mbowe iliwndaliwa na jini jiwe. Sukuma gang ndiyo wameamua kumkqmata awamu ya 6
Walioamua kumkamata wakina nani?
Unajuwa kama system inafata order kutoka juu.?

Nani aliamrisha mbowe akamatwe na kupewa kesi ya ugaidi wakati Magufuli ni marehemu?

Tuache unafki..
 
Wanatapatapa Sana japo huyu jamaa wanajaribu kumchafua ila falsafa zake ni kaa la Moto Sana na uzuri yeye alikuwa anasema kila kitu musimamo yake inajulikana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli hakwepi lawama za kesi ya Mbowe. Wenzake na Mbowe wako ndani tangu 2018
Wale uamsho walipewa kesi ya ugaidi na kukaa ndani miaka 9.

Je nao ni Magufuli ndy aliyewapa kesi?
Kumbe mambo ya Kupeana kesi za ugaidi yalikuwapo hata kabla ya Magufuli.

Na tumeshuhudia yamerudi tena mara tu baada ya kufa Magufuli.
Lakini sababu za unafiki wa wanasiasa hawalizungumzi hilo.

Wao wameshupaza shingo na kumpaka matope Magufuli.
Rip my President.
Rip Magufuli.
 
Na tumeshuhudia yamerudi tena mara tu baada ya kufa Magufuli.
Tunasema hakuna aliyepewa kesi ya ugaidi awamu ya Samia. Akina Mbowe wameandaliwa hiyo kesi na jini jiwe. Umeelewa we sukuma gang?
 
Ukweli ni kwamba Hawa wanasiasa uchwara wanamshambulia Magufuli kwa sababu bado ni tishio kwao anapambana nao yuko kaburini huyu jamaa alikuwa mwamba si mchezo

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Hili neno "AWAMU YA 6" ni lugha tu ya KISIASA na ni MWAMVULI wa kujifichia ili kuepuka JOTO KALI la kisiasa na kukwepa UWAJIBIKAJI. Serikali ya sasa INAMALIZIA ile miaka 5 ya Hayati JPM, lkn Viongozi ni WALE WALE! Tuache PROPAGANDA zisizo na MASHIKO. Kukubali MAKOSA siyo UDHAIFU.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Awamu zipo. Awamu ya 5 ilikuwa chini ya dikteta Magufuli ambaye ameliibia Sana taifa hili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…