Zitto, hii ndiyo timu ya kupitia masuala ya Tume Huru ya Uchaguzi uliyotegemea au wamekuchakachua?

Zitto, hii ndiyo timu ya kupitia masuala ya Tume Huru ya Uchaguzi uliyotegemea au wamekuchakachua?

Chadema hamkushiriki mkutano, acheni walioshiriki waunde timu inayowafaa. Kelele za nini. Nyie tazameni tu ,train ndiyo inaondoka hivyo bila nyie. Akili za kuambiwa na Lissu muwe mnachanganya na zenu.

CDM hawahitaji wala kuona wivu kutokuwepo kwenye hiyo tume, wanachotaka ni tume huru ya uchaguzi, na uchaguzi uwe huru kweli. Ikitokea ikawa hivyo, uandae dawa za pressure za kutosha, maana utaona ulichokuwa hupendi kukiona.
 
Mkutano wa Mutungi na vyama? Kuwa serious! Umeyasahau aliyowafanyia wapinzani huyo Mutungi wa maji. Katiba ni yetu wananchi, msipotaka tutaidai kwa maandamano. Hatutaki kunyukana kama Kenya, Malawi, Zambia lakini mkitulazimisha, tutanyukana.
Please remain within the context of the issue.. Chadema wamealikwa wawe sehemu ya mkutano, wamekataa, lakini hapo hapo wanataka wafanye maamuzi ya yanayoendelea ndani ya kikao hicho hicho wao wakiwa nje..Hakuna uhusiano na swali unalouliza.
 
Wadau nimeisoma orodha ya Wajumbe wa KAMATI iliyoundwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Sitarajii Kuona JIPYA Kwani Wajumbe wote ni MAKADA wa CCM na Wameteuliwa Kuitengenezea CCM Mazingira Mazuri
Kwa kuwa Watanzania tunajua CHAMA cha UPINZANI ni CHADEMA TU ndio maana ZITTO na Kundi lake Wameridhia hiyo KAMATI kwani ACT ni sehemu ya CCM
JamiiForums1958521821.jpg

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Chadema hamkushiriki mkutano, acheni walioshiriki waunde timu inayowafaa. Kelele za nini. Nyie tazameni tu ,train ndiyo inaondoka hivyo bila nyie. Akili za kuambiwa na Lissu muwe mnachanganya na zenu.
Uliishazoea kuweka TUME yenu ili ushindishwe. Miaka yazidi kwenda lakini wewe hukui kutwa kulilia mbeleko.
 
janja janja wanayoifanya haitawasaidia kitu bt ndo inawatia kitanzini, saivi watu wapo serious huwezi kuwahadaa kitoto vile.
 
Wasijaribu kutuletea UTOTO, hakuna Tume huru hapo.
Tume huru inapaswa kuwa na sifa hizi;

1. Vyama vya siasa vipendekeze angalau majina ya Wajumbe wawili wawili.
2. Taasisi za kidini zipendekeze zenyewe majina ya Wawakilishi wao
3. Mashirika ya kutetea haki za binadamu na utawala bora yapendekeze yenyewe wawakilishi wao huko.
4. Vyama vya wafanyakazi, wakulima, wanafunzi, NGOs n.k vipendekeze wawakilishi wao vyenyewe.
5. Wajumbe wapigiane kura na kuchaguana wenyewe huko ili kupata viongozi wao (Rais asihusike kuchagulia viongozi).
 
Naomba kumuuliza Mhe. Zitto kama ameshiriki kuunda hii timu iliyotajwa na Msajili au Msajili Kwa namna alivyoona inafaa ndiye kaja na wajumbe wake? Mwenyekiti wa timu hii kweli tunaamini ni mtu wakumleta kwenye hoja nyeti wakati alishatoa kauli mbili tofauti juu ya uchaguzi uliopita? Ana kauli ya baada ya uchaguzi na baada yakuingia awamu wa sita.

Huyu Mwenyekiti wa amani wa Dar es salaam tunaamini anatuvusha na Makamu wake?

Wawajilishi wa vyama vya siasa ndo Hawa? Wawalishi wa Asasi za kiraia nafasi hazina majina means awakushirikishwa wateue watu?

Nataka Kuanza kuamini katiba mpya ni ngumu kupatikana Kwa namna agenda zinavyowekwa meza kuu
Zitto ANATUMIKA IPASAVYO SIO MPINZANI

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Wasijaribu kutuletea UTOTO, hakuna Tume huru hapo.
Tume huru inapaswa kuwa na sifa hizi;

1. Vyama vya siasa vipendekeze angalau majina ya Wajumbe wawili wawili.
2. Taasisi za kidini zipendekeze zenyewe majina ya Wawakilishi wao
3. Mashirika ya kutetea haki za binadamu na utawala bora yapendekeze yenyewe wawakilishi wao huko.
4. Vyama vya wafanyakazi, wakulima, wanafunzi, NGOs n.k vipendekeze wawakilishi wao vyenyewe.
5. Wajumbe wapigiane kura na kuchaguana wenyewe huko ili kupata viongozi wao (Rais asihusike kuchagulia viongozi).
Kwani MHESHIMIWA POLEPOLE anasemaje kuhusu hili ??
 
Eti kwa vile hawakuhudhuria ndio wasihoji, CCM na ACT wanataka kujimilikisha mchakato wa tume huru wakati inajulikana wazi walio initiate vuguvugu la KatibaMpya na @tumehuru ni Chadema.
Siasa ni mahesabu. Kwa hili crediti ni CCM na ACT. After all ndiyo vyama vikubwa nchini Tanzania. Chadema ni chama chenye mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa. Si mbaya akawaacha vyama vyenye uwakilishi mkubwa wa wananchi wakapanga mambo ya kitaifa kwa niaba yao. Ndiyo democracy by representation inavyotaka.
 
Mkutano wa Mutungi na vyama? Kuwa serious! Umeyasahau aliyowafanyia wapinzani huyo Mutungi wa maji. Katiba ni yetu wananchi, msipotaka tutaidai kwa maandamano. Hatutaki kunyukana kama Kenya, Malawi, Zambia lakini mkitulazimisha, tutanyukana.
Unajirurahisha. Labda kunyukana kwenye Club house ya Maria na siyo Tanzania
 
Na kwanini wasihoji, wanaotakiwa kuhoji ni wale tu waliohudhuria? Kwani posho za wajumbe zinalipwa na CCM au ACT si wanalipwa kwa kodi za wananchi. Hivi wanafunzi waliwakilishwa na nani wakulima je kwahiyo wasihoji.

Masuala ya uchaguzi ni ya kitaifa mtu yeyote hata kama hana chama na hakuwakilishwa ana haki ya kuhoji chochote.
Tunatumia democracy by representation. Vyama vya siasa hivyo vikubwa nchini CCM, ACT na CUF vinawakikisha vyama vya siasa, wengine tutawakilishwa kupitia wawakilishi wa dini, asasi za kiraia, wasomi na wawakikishi wengine. Chadema tulieni, mnawakilishwa na vyama vilivyo juu yenu. Mlipewa nafasi ya upendeleo mkadanganywa na Lissu mkasusa. Swallow the pain
 
CDM hawahitaji wala kuona wivu kutokuwepo kwenye hiyo tume, wanachotaka ni tume huru ya uchaguzi, na uchaguzi uwe huru kweli. Ikitokea ikawa hivyo, uandae dawa za pressure za kutosha, maana utaona ulichokuwa hupendi kukiona.
Tafsiri ya tume huru kwako ni ipi mpaka umuone lema akiwa mjumbe .akili za wapi nyie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom