Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto kubali tukukaange kwa mafuta yako,kwanini umuite Mtu neno au jina usilojua maana yake ilhali huyo mtu ana jina lake na unalifahamu? Una mleta mama yako hapa ili upate sympathy? Sisi siyo wajinga ,tuna akili.Hufai kuwa kiongozi,bora ungejitaja kwamba wewe pia ni mlemavu kwakuwa una vidude vya ajabu usoni karibu na macho.Sisi sote tu walemavu,una mdhihaki mtu aliyelazimishwa kuwa mlemavu na mwanadamu mwenzake?
Hivi mtu mlemavu akiitwa mlemavu anakuwa amedhihakiwa?
 
Kwakuwa ameomba radhi, amefanya jambo jema na si vema kuendelea na mjadala huu

Hujafa hujaumbika
 
Sidhani kama alifanya hivyo kwa makusudi ukizingatia Mama yake alikuwa na Ulemavu.., Na Lissu sio Mlemavu naturally....
Ashike Msahafu halafu Aape Wallah wa bila wa tallahi sikuelewa maana ya neno chiba!
Ili Allah Apitishe Hukumu Yake!
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
Unataka kusema zitto alilisahau jina la Lissu? Kwa nn asingemuita tu Lissu kama anavyomuita siku zote?
 
Zitto anashinda twitter na huko neno Chiba linatumika kila siku.

Asitufanye mambwiga bhana!
Hili pia linazua maswali mengi....huenda jamaa hakutegemea kukosolewa hivyo imebidi atafute sababu ya kujitetea.
 
Ashike Msahafu halafu Aape Wallah wa bila wa tallahi sikuelewa maana ya neno chiba!
Ili Allah Apitishe Hukumu Yake!
Dah!...umeenda mbali Sana mkuu...tusifike huko.
 
Kuomba radhi ni swala moja kukubaliwa ni swala jingine.

Viongozi wajifunze kuwajibika pale wanapokosea, Ni aibu kwa kiongozi kariba ya Zitto kutamka maneno kama haya.

Hata CCM pamoja na kebehi zao zote kwa upinzani sijawahi kuwasikia wakimdhihaki Lissu kwa ulemavu wake.
Siasa za nchi hii umeanza kuzijua leo? Waliokuwa wakimuita Mbowe Makengeza ni kina nani?
 
Msanii wa reggae Ras Mtimanyongo amefunga mjadala wa Zitto Kabwe kumwita Tundu Lisu Chiba kwa kusema hilo ni jina la kawaida kabisa halina hata chembe ya kejeli.

Watu wenye miguu isiyolingana urefu hupenda wenyewe kuitwa Bryson au Chiba kwani huwapa umaarufu fulani.

Huwezi tu kuitwa Chiba eti kwa sababu miguu yako hailingani urefu, ni lazima uwe na value fulani " special" kwa jamii hivyo Zitto Kabwe hakukosea kumwita Lisu kama Chiba bali alimpaisha zaidi, anasema ras Mtimanyongo.

Wote Bryson na Soni Chiba walikuwa watu maarufu sana enzi zao, anasisitiza Ras.

Yaaa man Nimefunga mjadala!

Mungu wa mbinguni ibariki Chadema na ACT wazalendo!
 
Unataka kusema zitto alilisahau jina la Lissu? Kwa nn asingemuita tu Lissu kama anavyomuita siku zote?
Usipangie watu majina ya kuwaita watu, Mara kadhaa Lissu alimuita Magufuli Dikteta uchwara, amemuita Zitto ni Yuda.

Zitto pia hakujua Chiba inahusiana na Ulemavu kwa binaadam, hivyo alilitumia akijua ni jina la utani tuu, amejua maana yake ndio sababu ameomba Radhi, Isingekuwa inahusiana na ulemavu ilikuwa ibaki hivyo na hakuna ulazima wa mtajwa atajwe kwa jina lake moja kwa moja, yeye sio Mungu.
 
Msanii wa reggae Ras Mtimanyongo amefunga mjadala wa Zitto Kabwe kumwita Tundu Lisu Chiba kwa kusema hilo ni jina la kawaida kabisa halina hata chembe ya kejeli...
Ras amepiga cha wapi kabla ya kutoa haya maoni yake? Tuanzie hapo...
 
Inasikitisha sana. Hilo jina analijua vizuri maana yake. Yeye mwenyewe mama yake mzazi alikuwa mlemavu wa miguu. Aliwahi hata kuwa Mwenyekiti wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA). Mbona hakumuita mama yake China? Huyu mtu ana laana fulani.
Kwani ni nini maana ya Chiba?
 
Filamu - Champion of Death
Stelingi - Sony Chiba
Zamani sana hiyo kama sikosei ni miaka ya 80s wahenga waliopo hapa watakuwa wanakumbuka.
 
Lissu si mlemavu, anatembea kwa miguu yote na hajapoteza kiungo mkuu wangu.

..Ni mlemavu.

..mguu mmoja ni mfupi na hawezi kuukunja.

..pia mlemavu wa mkono ambao haunyooki.

..huenda Zitto alilenga kumkejeli akiamini sauti za kumuunga mkono zitakuwa kubwa kuliko za kumpinga.

..Ni jambo la bahati mbaya sana Zitto kujihusisha na siasa za namna hii.

..Kwenye siasa it is ok to attack / make fun of your opponents character but not their physical disabilities.

..Mnyika alipomuita Kikwete dhaifu alikuwa akizungumzia aina ya uongozi wa Kikwete.

..Sikuwahi kumsikia Mnyika au mpinzani yeyote akimkejeli Kikwete kwa changamoto ya kiafya iliyopelekea upasuaji.

..Kwa hiyo sikubaliani na mlinganisho wako kwa kauli ya Mnyika kwa Kikwete, au kauli ya Lissu dhidi ya Magufuli, na dhihaka za Zitto dhidi ya ulemavu wa Lissu.

..Nashauri Chadema wamsamehe Zitto Kabwe, lakini wawe makini naye. Zitto is out of control ktk kuitafuta na kuichokonoa Chadema.

Cc Nguruvi3, Fundi Mchundo
 
Back
Top Bottom