Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Zitto Kabwe amdhihaki Tundu Lissu kwa kumuita CHIBA. Aomba radhi baada ya kulalamikiwa

Kuomba radhi ni swala moja kukubaliwa ni swala jingine.

Viongozi wajifunze kuwajibika pale wanapokosea, Ni aibu kwa kiongozi kariba ya Zitto kutamka maneno kama haya.

Hata CCM pamoja na kebehi zao zote kwa upinzani sijawahi kuwasikia wakimdhihaki Lissu kwa ulemavu wake.
Siku zote anayeomba radhi ni mtu strong.
 
Inawezekana attacks anazopewa Zitto siku za karibuni zimemvuruga ameamua kufunguka kwa namna aliyofanya, atibue makusudi kisha aombe radhi.

Lakini pia inawezekana sababu aliyoitoa Zitto binafsi ni ya kweli, hakujua maana halisi ya hilo neno hasa ukizingatia neno lenyewe ni moja kati ya yale yanayozuka mitaani kila kukicha.

Hivyo basi, kwa upande wangu naona bora nikubaliane na sababu ya Zitto kwamba hakujua maana ya hilo neno, kwani kistaarabu mtu akikukosea halafu usipoikubali samahani yake ni wewe mkosewaji ndie utakuwa na matatizo, sio yeye mkosaji.
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako.

Hii ndiyo Tweet aliyoandika Twitter wakati akijibu hoja ya mdau


Baada ya kulalamikiwa na wadau, Zitto Kabwe aliomba msamaha na kudai kuwa hakuwa anajua maana ya neno ''CHIBA'' kama linamaanisha mlemavu, bali alijua ni maneno ya vijana tu

Nukuu
Kwa kweli sikufahamu kama jina Chiba linahusiana na ulemavu. Nilidhani ni majina ya Vijana ya kutaniana. Mama yangu mzazi alikuwa mlemavu kamwe siwezi kutweza ulemavu wa Mtu. Naomba radhi sana Kwa hili. Hakika Sio Sawa. Uzee umeingia tunapitwa na majina ya mtaani. Mniwie radhi

Amemuita chiba baada ya Lisu kupata shida aache uongo haka kajamaa kanapenda kuonekana smart kuliko wengine...angekua amemuita Chiba kabla ya tatizo tungesema kachapia haelewi maana ya chiba ila hili anajua alichofanya.
 
Zitto ni wakuja kama walivyo wengi

Hata wengi wanaomshutumu Zitto nao hawakuwa wanajua maana ya Chiba au hata sasa hawajui maana ya Chiba

Sio kila mlemavu anaitwa Chiba

Chiba ni Mlemavu mwenye Mguu mmoja mfupi

Kigogo ndio hupenda kumtusi Lissu kwa jina hilo


Inawezekana ni kweli Zitto hakujua maana ya neno Chiba ila naamini alijua ni jina la Kejeli

Tujifunze kuwa Waungwana na hata Bw. Mtume S.a.w ametukataza kuitana kwa majina ya kejeli na kebehi
 
Zitto sasa amevuka mpaka na shime ndugu Tundu usimchekee tena hasa kwa hatua hiyo ya kukudhalilisha kwa kilema chako...
Haiwezekani asijue neno CHIBA(CHIBASON) wakati ni neno la kitaa toke 'nineteen seventies', anasemaje ni terms za vijana wakati tangu akiwa mtoto hilo neno lilikuwa likitumika.

CHIBA kwa maana mguu mmoja ndiyo umelemaa au ni mfupi zaidi ya mwingine.
 
Kama kawaida ya Chadema tayari mmepata sera hapo.

Wazee wa matukio daima.
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
Shukrani sana kwa busara zako, lakini hawatokuelewa
 
Keshaomba radhi
Hujafa hujaumbika!

Kwa jinsi Zitto Kabwe alivyo siyo busara kumkejeli mwenzake kwani naye ana hitalafu nyingi tu mwilini mwake, ajiheshimu.

Labda kama hakusema ila wanamsingizia.

Kiuhalisia Chiba ni mtu aliyezaliwa akiwa na miguu isiyolingana.
 
Mbona hata mamake zito kabwe na yeye alikuwa soni chiba?
 
Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.

Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
Upo sawa ila maana yake anajua ndo maana kamuiata ni neno la kitambo tu
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] [emoji444]ewe chiba we chiba ebu acha magongo ngongongo[emoji444]
 
Back
Top Bottom