Hivi mtu mlemavu akiitwa mlemavu anakuwa amedhihakiwa?Zitto kubali tukukaange kwa mafuta yako,kwanini umuite Mtu neno au jina usilojua maana yake ilhali huyo mtu ana jina lake na unalifahamu? Una mleta mama yako hapa ili upate sympathy? Sisi siyo wajinga ,tuna akili.Hufai kuwa kiongozi,bora ungejitaja kwamba wewe pia ni mlemavu kwakuwa una vidude vya ajabu usoni karibu na macho.Sisi sote tu walemavu,una mdhihaki mtu aliyelazimishwa kuwa mlemavu na mwanadamu mwenzake?
Dah!...NB:
Binafsi naamini kwa weledi na umakini wa Zitto kwenye kujadili, kuchangia na kuanzisha hoja hasa kwenye public platforms ZZK hakuandika kwa bahati mbaya......,Muda utatuambia.......
Ashike Msahafu halafu Aape Wallah wa bila wa tallahi sikuelewa maana ya neno chiba!Sidhani kama alifanya hivyo kwa makusudi ukizingatia Mama yake alikuwa na Ulemavu.., Na Lissu sio Mlemavu naturally....
Unataka kusema zitto alilisahau jina la Lissu? Kwa nn asingemuita tu Lissu kama anavyomuita siku zote?Ameomba radhi! Seems alijua ni jina la utani lakini hakujua linahusishwa na ulemavu. Itakuwa ajabu hili tukitaka kulifanya topic.
Nashauri likomee hapo, kulizungumza zaidi halitamuumiza tu Zitto bali hata ndugu yetu. Mengine tuache yapite.
Hili pia linazua maswali mengi....huenda jamaa hakutegemea kukosolewa hivyo imebidi atafute sababu ya kujitetea.Zitto anashinda twitter na huko neno Chiba linatumika kila siku.
Asitufanye mambwiga bhana!
Yamoto hii ya juzi 2013?? Hilo jina lipo toka miaka ya 90
Dah!...umeenda mbali Sana mkuu...tusifike huko.Ashike Msahafu halafu Aape Wallah wa bila wa tallahi sikuelewa maana ya neno chiba!
Ili Allah Apitishe Hukumu Yake!
Siasa za nchi hii umeanza kuzijua leo? Waliokuwa wakimuita Mbowe Makengeza ni kina nani?Kuomba radhi ni swala moja kukubaliwa ni swala jingine.
Viongozi wajifunze kuwajibika pale wanapokosea, Ni aibu kwa kiongozi kariba ya Zitto kutamka maneno kama haya.
Hata CCM pamoja na kebehi zao zote kwa upinzani sijawahi kuwasikia wakimdhihaki Lissu kwa ulemavu wake.
Usipangie watu majina ya kuwaita watu, Mara kadhaa Lissu alimuita Magufuli Dikteta uchwara, amemuita Zitto ni Yuda.Unataka kusema zitto alilisahau jina la Lissu? Kwa nn asingemuita tu Lissu kama anavyomuita siku zote?
Ras amepiga cha wapi kabla ya kutoa haya maoni yake? Tuanzie hapo...Msanii wa reggae Ras Mtimanyongo amefunga mjadala wa Zitto Kabwe kumwita Tundu Lisu Chiba kwa kusema hilo ni jina la kawaida kabisa halina hata chembe ya kejeli...
Kwani ni nini maana ya Chiba?Inasikitisha sana. Hilo jina analijua vizuri maana yake. Yeye mwenyewe mama yake mzazi alikuwa mlemavu wa miguu. Aliwahi hata kuwa Mwenyekiti wa chama cha walemavu Tanzania (CHAWATA). Mbona hakumuita mama yake China? Huyu mtu ana laana fulani.
Lissu si mlemavu, anatembea kwa miguu yote na hajapoteza kiungo mkuu wangu.
HEBU MUULIZE ZITO LABDA ANALIJUA JIBU LA SWALI LAKO NDIO MAANA AKAOMBA RADHIHivi mtu mlemavu akiitwa mlemavu anakuwa amedhihakiwa?
Ni nini maana ya Chiba? Kwa tafsiri rasmi ya Lugha gani?..Ni mlemavu.
..mguu mmoja ni mfupi na hawezi kuukunja.
..pia mlemavu wa mkono ambao haunyooki...