Zitto Kabwe asema Kikwete alimwambia CCM hakina muda mrefu madarakani na kumshauri abaki upinzani. Aliahidiwa uwaziri wa fedha iwapo angejiunga CCM

Zitto Kabwe asema Kikwete alimwambia CCM hakina muda mrefu madarakani na kumshauri abaki upinzani. Aliahidiwa uwaziri wa fedha iwapo angejiunga CCM

Hii habari sijui uelewa wangu mdogo!!. Unasema kikwete alimwita na kuahidi kumpa uwaziri akijiunga CCM. Kikwete huyohuyo anamwonya asihamie CCM kwani hakina muda mrefu madarakani. Rudieni kuisoma habari hapo juu. Je Kikwete na Zito walikuwa wamelewa Pombe?
Hakika akili zilikuwa zimewaruka kichwani.
Kwa hiyo ni kwa msingi wa ushauri huo wa Kikwete, Zitto akaanzisha chama haraka ili achukue nafasi ya CCM iliyokuwa mahututi?

Zitto ndani ya CHADEMA ulikuwa ni mradi wa kuiangamiza CHADEMA.
 
Zitto Kabwe amesema mwaka 2012 alipata changamoto chama chake cha wakati huo cha CHADEMA akidai ilikuwa juhudi ya kumzuia kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Zitto amesema kulikuwa na makubaliano baada ya kugombea uchaguzi wa nyuma yake kwamba amuachie kijiti Freeman Mbowe na atampokea miaka mitano ijayo na badala yake miaka miwili kabla aliondolewa nyazifa zote za uongozi Chadema na wapo katika kundi lao walisema waende CCM.

Zitto Kabwe amesema Jakaya Kikwete alimuita na kumwambia ana machaguo mawili kwa kuwa alikuwa anachipukia kwenye siasa, kwanza kujiunga na chama tawala cha CCM na endapo angefanya hivyo angempa uwaziri wa fedha siku inayofata.

Rais mstaafu Kikwete alimpa angalizo Zitto Kabwe kwamba kwa maono yake CCM haitakuwepo madarakani muda mrefu ilhali Zitto bado kijana mdogo na kumshauri kutafuta jukwaa lingine lakini sio la chama tawala.

Zitto amesema kwenye hicho kikao mmoja wa waliokuwepo ni rafiki yake Deo Fulikunjombe naye akamshauri asiende CCM.

Kumbe biashara ya CCM kununua wapinzani ilianza kitambo sana?
 
Watale tulotumia muda wetu kujifunza propaganda hatuoni mpya hapo
 
Tulistuka mapema sana
Ni kama mna roho ya paka.
Kuna msemo unasema paka ana "maisha tisa",... najuwa tafsiri hii si rasmi, lakini nnina hakika naeleweka.
Chama kimepita kwenye misukosuko ya kutisha sana; lakini hofu yangu kubwa ni kwamba mtu asiyekuwa na uwezo kama Samia ndiye anakuja kuwamaliza. Inashangaza sana!
 
Samia aweza kuwa ndio Rais wa mwisho kutokea ccm , hana uwezo wa kumaliza Chadema , vinginevyo atamalizika yeye kama Sizonje
 
Samia aweza kuwa ndio Rais wa mwisho kutokea ccm , hana uwezo wa kumaliza Chadema , vinginevyo atamalizika yeye kama Sizonje
Mmmmh. Mki'survive' safari hii huenda hamtapotea tena.

Sitegemei kamwe kwa kada mwaminifu wa chama kama wewe kuona hatari inayo wanyemelea mapema hivi. Mtakuja kustuka kukisha kucha, na wakati huo 'stori' zitakuwa nyingine kabisa. Kirusi cha Samia tayari kimo damuni mwenu, subirini tu kiwamalize, au kwa bahati tu mwili wa chama chenu kiote usugu dhidi ya kirusi hicho. Lakini siku ndiyo zinayoyoma hizo.
Hili tuliachie hapa mkuu wangu 'Erythro.'
 
Ni kama mna roho ya paka.
Kuna msemo unasema paka ana "maisha tisa",... najuwa tafsiri hii si rasmi, lakini nnina hakika naeleweka.
Chama kimepita kwenye misukosuko ya kutisha sana; lakini hofu yangu kubwa ni kwamba mtu asiyekuwa na uwezo kama Samia ndiye anakuja kuwamaliza. Inashangaza sana!
Hahaha mama akawapumbaza na juisi za ikulu wakawa wanakenua haooo ,,baadae wanashtuka wamepigwa banzi la kisogoni wakigeuka hawaoni mtu ,,,walijua wanapambana na watu wa mwendazake kumbe nao wanatumika tu
 
Mmmmh. Mki'survive' safari hii huenda hamtapotea tena.

Sitegemei kamwe kwa kada mwaminifu wa chama kama wewe kuona hatari inayo wanyemelea mapema hivi. Mtakuja kustuka kukisha kucha, na wakati huo 'stori' zitakuwa nyingine kabisa. Kirusi cha Samia tayari kimo damuni mwenu, subirini tu kiwamalize, au kwa bahati tu mwili wa chama chenu kiote usugu dhidi ya kirusi hicho. Lakini siku ndiyo zinayoyoma hizo.
Hili tuliachie hapa mkuu wangu 'Erythro.'
Mama hana uwezo huo , alichoweza ni kuuza Bandari kwa Wajomba zake
 
Hahaha mama akawapumbaza na juisi za ikulu wakawa wanakenua haooo ,,baadae wanashtuka wamepigwa banzi la kisogoni wakigeuka hawaoni mtu ,,,walijua wanapambana na watu wa mwendazake kumbe nao wanatumika tu
Inabidi kucheka, ingawaje haya ni mambo mazito sana yanayohusu hatma ya taifa letu.
Nimekuelewa jinsi ulivyoliwasilisha hili.
 
Sina sababu ya kubisha Zitto anasema ukweli.

JK is pro talent hata Muhongo, Matarigio na Matindi kawarudisha yeye Tanzania na wengine kadhaa waliokuwa wanapigiwa kelele na jamii ndani ya Tanzania ni talent aliwapa nafasi.

The sad truth japo alikuwa anawapa so called talent nafasi alifanya ivyo kwa milio yao kushinda uwezo wao halisi.

Zitto hana sifa za kuwa waziri wa fedha kuna watu more qualified kumshinda yeye Tanzania wengi tu.
 
Back
Top Bottom