Zitto Kabwe: Diaspora hawatumi pesa nyumbani, kazi yao ni kukesha Clubhouse

Zitto na yeye Mbona anajionyesha ni mjinga sana?

Kenya ina Diaspora zaidi ya milioni tatu. Tanzania ina Diaspora laki tano.

Kweli anataka watu milioni tatu watume pesa nyumbani sawa na laki tano?

Wakenya waliruhusiwa Kusafiri na kusoma nje miaka mingi sana. Watanzania hata kupata passport ilikuwa mpaka upate scholarship ya serikali.

Pia Watanzania waliaminishwa miaka na miaka kwamba ukiishi nje wewe sio mzalendo. Wakaanza kuogopa hata kwenda nchi jirani. Hao Wachache walioenda ndio sasa mnataka kukamua mpaka damu?

Wakenya Diaspora wamepewa uraia pacha, Watanzania ni chenga kila siku.

Zitto, I hope Unajua mahesabu. Watu milioni tatu pesa wanazotuma nyumbani haziwezi kufanana na za watu laki tano.
 
Zitto Kabwe kwanza anajua ugumu wa kupata passport nchi hii??

Hiyo passport inavyopatikana kwa mbinde kama hisani na maswali chungu nzima unaweza tamani kutuma pesa kweli ukiwa huko ughaibuni??
 
K Kwa kweli
 
Hoja kama hii inaonesha udogo wa mawazo ya Zitto.

Badala ya kuipigia lelele serikali iruhusu dual citizenship kama Kenya watu wapate uhuru wa kuchangia kwa njia zote, hali na mali, anaongozwa na akili fupi ya kuangalia pesa na kuingilia uhuru wa watu kujieleza tu.

Kiongozi wa upinzani anawanyanyapaa watu kutumia haki yao ya kibinadamu kujieleza mitandaoni kweli?

Huyu ni mpinzani au msaidizi wa kitengo cha usalama wa taifa anaziba watu midomo wasiongee?
 
Mapema mwaka huu 2024 nilishuhudia mteja mmoja benki "akigogora" kwa sauti sana na Teller kisha manager. Kisa alizuiliwa "ku-withdraw" fedha alizotumiwa akitakiwa aeleze anazipeleka wapi.
 
Wakenya walianza kusafiri kwenda nje tangu miaka ya 70 so Mkenya anaposafiri kwenda nje anakuwa na connection tayari,tofauti na mtanzania ukienda nje unaanza mwenyewe from zero hadi uje kusimama it takes long time haiwezi kuwa sawa.
 
hii nchi kila kitu ni uozo tu,....kuna wakati nilihiitaji sana SKRILL,...nilihangaika mpaka nikanyoosha mikono juušŸ™ŒšŸ™Œ
 
hii nchi kila kitu ni uozo tu,....kuna wakati nilihiitaji sana SKRILL,...nilihangaika mpaka nikanyoosha mikono juušŸ™ŒšŸ™Œ
Ulitaka kufungua akaunti mkuu? Mbona ni rahisi mkuu sema itabidi ufoji proof of address maana template wanayotaka huwezi kuipata tanzania so huwa tunazifoj.
 

Unachosema ni kweli.

Nilikaa na mshua mmoja alikuwa anafanya kazi East African Community ya mwanzo.

Anasema katika community wenzao Waganda na Wakenya walikuwa wanapeana mipango ya kwenda nje kusoma na kufanya kazi.

Upande wa Tanzania ilikuwa mtu akitaka kufanya kazi au kusoma nje anaonekana yeye si mzalendo.
 
Diaspora nao wangekuwa bize na maisha yao badala ya kupiga siasa mtandaoni. Kuhusu kutuma hela hapo ni jambo lingine linalohitaji umakini. Wabongo wengi tuna changamoto ya uaminifu. Watu walichangia Join the Chain ya CHADEMA bila kujua wanachangia hela za kujenga hekalu la Mbowe na baadhi ya chawa wake.
 
Ulitaka kufungua akaunti mkuu? Mbona ni rahisi mkuu sema itabidi ufoji proof of address maana template wanayotaka huwezi kuipata tanzania so huwa tunazifoj.
duuh!,...aise mi nilichoka🤧🤧
mpaka nikaamua Nitumie crypto coins tu...
 
duuh!,...aise mi nilichoka🤧🤧
mpaka nikaamua Nitumie crypto coins tu...
Kwa Tanzania Skrill, Wise, Payoneer walau ni rahisi kuziverify. Wise ni straight forward kabisa. Hizi mbili zitahitaji uedit bank statement au utility bill kwa kuongeza physical address
 
Kwa hiyo wao ni diaspora wa Nchi gani?
 
Kwa Tanzania Skrill, Wise, Payoneer walau ni rahisi kuziverify. Wise ni straight forward kabisa. Hizi mbili zitahitaji uedit bank statement au utility bill kwa kuongeza physical address
ok Asante sana MKUU,...
 
Wanatuma sana tuu sema ni wachache Kwa sababu Watanzania hawapendi kusafiri
 
Mfumo upo ila Watanzania hawapendi kutoka Nje ya Nchi na tafiti zinaonesha hivyo
 
naunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…