Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Naona bado vita na marehemu inaendelea.

Kwahiyo Prop Assad anarudi kwenye kiti chake kumalizia siku zake.?
Mahakama ya Tanzania imetangaza kumuondoa aliyekuwa mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) Prof Mussa Assad na Magufuli kama KINYUME CHA KATIBA *Lakini mahakama inakataa kutangaza uteuzi wa CAG Charles Kichere kama kinyume cha katiba * Mahakama pia inakataa kumrejesha Assad kama CAG mkuu
 
Naona bado vita na marehemu inaendelea.

Kwahiyo Prop Assad anarudi kwenye kiti chake kumalizia siku zake.?
Mahakama imesema kwasababu Kichere anasifa aendelee....... nadhani kwasasa Mzee akikata rufaa inawezekana akalipwa maslahi yake tangu alipotolewa ofisini
 
Naona bado vita na marehemu inaendelea.

Kwahiyo Prop Assad anarudi kwenye kiti chake kumalizia siku zake.?
Zitto na genge lake Udini unawasumbua sana.

Acheni siasa za kupambana na Ukristo pimbi nyie
Ndio nei ya mchele itashuka?
Ndio bei za mfuta zitashuka?
Ndio mfumuko wa bidhaa uliofikia 200% utashuka?

Nyie nyote mko nje ya hoja...

Yaani kama ingekuwa mko shule na mwalimu kawapa mtihani basi karatasi zenu za majibu zingechorwa mstari wa cross ❌ kubwa na kuandikiwa OUT OF QUESTION na hivyo kuambulia ZERO...

Ndivyo ilivyo sasa. OUT OF CONTEXT...!
 
Hawezi kurudishwa kazini. Kwanza Mahakama haijaagiza arudishwe kazini. Mahakama ilitoa hukumu kuwa kuondolewa CAG ilikuwa kinyume cha Sheria.

Mahakama haikusema kuwa CAG wa sasa hayuko kisheria. Hivyo suala la Prof Assad kurudi kazini HALIPO.

Kwa maoni yangu; Prof Assad na Zitto wameshinda pakubwa kuliko Prof kurudishwa kazini. Amesafishwa jina na hii itakuwa ni MWONGOZO kwa ma Rais wengine wasifanye maamuzi kwa HISIA zao au kwa KUKURUPUKA.
 
Hoja yangu ni kwamba kuna katiba yenye manufaa kwa watawala, kuna katiba yenye maslahi kwa wanasiasa, na kuna katiba yenye maslahi kwa wananchi na maendeleo ya nchi yao kiuchumi na kisiasa.

Sawa, ndio unataka kusema je kwani?
 
Nimekuelewa boss, ila mahakama kusema katiba ilikiukwa na wakati huo huo kushindwa kutengua huo ubatili hapo sio kujikanganya ?....
Pascal Mayalla
Nguruvi3
 

Kwa ujumla mahakama zetu haziko huru, na huu ni ushahidi wa hilo. Hili jambo lilipaswa kutolewa hukumu mapema, lakini limechelewa mpaka limepoteza maana.
 
Mahakama imemkuta marehemu na hatia ya kuvunja katiba!

Kwa nini alaumiwe marehemu ilhali hakufanya yeye binafsi bali ni MAMLAKA,ambayo ipo mpaka Sasa?

Sio mara ya kwanza mahakama kujiridhisha kuvunjwa kwa katiba, baada ya hapo adhabu kwa mkosaji ninini, au nafuu(remedy) kwa aliyekosewa(Victim) ni ipi?

Katiba Ndiyo sheria kuu juu ya Sheria zetu zote, kwanini inavunjwa na mahakama inaridhika halafu hakuna adhabu kwa mkosaji. Si unajua aliye vunja sheria zingine huwa ni kifungo na Adhabu zingine za kikatili?
Why anayevunja sheria mama hawajibishwi?

Na mahakama pia imenishangaza, inakubali Assa alifukuzwa kimakosa kwa sababu alipaswa kuhudumu mpaka muda wake wa kustaafu, lakini inakataa kwamba aliyeteuliwa kushika nafasi yake aliteuliwa kimakosa[emoji1787]

Nadhani Sasa tunahitaji sheria ndogo ya kuilinda katiba itakayokuwa na meno kuitetea katiba kwa kuwaadhibu wale (viongozi) wanaoivunja kwa makusudi.
Hii itasaidia kuwadhibiti viongozi wanaodhani kuvaa joho la uongozi ndo Kinga ya wao kufanya watakayo.
 
Mahakama imekosea. Sheria inasema hivi:

CAG ATATEULIWA NA RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ISIPOKUWA ANAWEZA KUONGEZEWA TENA KIPINDI KISICHOZIDI MIAKA MITANO...
Kwanza hatuna mahakama wala bunge hizi ni idara za CCM tupu, marehemu angekuwa hai na madarakani wangesema alikosea? watanzania wangapi waliuliwa na huo utawala dhalimu na kesi zilipelekwa kwao wakakaa kimya? mi sina imani na mahakama za CCM ni ujinga tupu
 
Kuna justification flani tu inatafutwa Ili kumchafua jembe.

Katiba inavunjwa kilasiku kwa staili tofauti tofauti na huyo zito haendi kushtaki anaangaliatu.
 
Mwendazake haijawahi kuheshimu Katiba unless iwe ishu inaho mfavour.

CAD Assad arudishwe kazini haraka Sana.
 
Ama kweli malipo ni hapahapa duniani.

kumbe mzee wa watu prof. Asad alionewa buree.
mlio pewa mamlaka acheni kuwaonea walio chini yenu ipo siku mtadhalilika.

uonevu kama alio fanyiwa Prof. Asad upo sana unaendelea kwenye taasisi mbalimbali, na wengi wao hawana wa kuwatetea wala hawaonekani, hivyo wanaugulia manyanyaso makubwa na uonevu wanao fanyiwa na walio juu yao.

kwa uonevu na udhalilishaji alio fanyiwa Prof. Asad anayo haki ya kurudishiwa title yake ya kuwa AG au alipwe fidia.
 
Kuna justification flani tu inatafutwa Ili kumchafua jembe.

Katiba inavunjwa kilasiku kwa staili tofauti tofauti na huyo zito haendi kushtaki anaangaliatu.
Nani anavunja? Mtaje

Mwendazake alikuwa mshenzi tuu na dikteta uchwara.
 
Mkuu anzisha Mahakama yako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…