Mahakama imemkuta marehemu na hatia ya kuvunja katiba!
Kwa nini alaumiwe marehemu ilhali hakufanya yeye binafsi bali ni MAMLAKA,ambayo ipo mpaka Sasa?
Sio mara ya kwanza mahakama kujiridhisha kuvunjwa kwa katiba, baada ya hapo adhabu kwa mkosaji ninini, au nafuu(remedy) kwa aliyekosewa(Victim) ni ipi?
Katiba Ndiyo sheria kuu juu ya Sheria zetu zote, kwanini inavunjwa na mahakama inaridhika halafu hakuna adhabu kwa mkosaji. Si unajua aliye vunja sheria zingine huwa ni kifungo na Adhabu zingine za kikatili?
Why anayevunja sheria mama hawajibishwi?
Na mahakama pia imenishangaza, inakubali Assa alifukuzwa kimakosa kwa sababu alipaswa kuhudumu mpaka muda wake wa kustaafu, lakini inakataa kwamba aliyeteuliwa kushika nafasi yake aliteuliwa kimakosa[emoji1787]
Nadhani Sasa tunahitaji sheria ndogo ya kuilinda katiba itakayokuwa na meno kuitetea katiba kwa kuwaadhibu wale (viongozi) wanaoivunja kwa makusudi.
Hii itasaidia kuwadhibiti viongozi wanaodhani kuvaa joho la uongozi ndo Kinga ya wao kufanya watakayo.