Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Mahakama Kuu, Masjala Kuu imebainisha kwamba uamuzi wa kuondolewa katika utumishi wa umma kwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ulikiuka Katiba.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu, Dk Benhajj Masoud (kiongozi wa jopo), Juliana Masabo na Edwini Kakolaki, kufuatia kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Profesa Assad aliteuliwa kushika wadhifa huo na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Novemba 5, 2014 na alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi Novemba 4, 2019 baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipomteua Charles Kichere kushika wadhifa huo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Serikali mwaka 2019 ilieleza kuwa Profesa Assad kipindi chake kilimalizika Novemba 4, 2019.

Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muda wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.
Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muwa wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 8 ya mwaka 2020, Zitto akiwakilishwa na mawakili Dk Rugemeleza Nshala na Nyaronyo Kichere, alikuwa akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad na kuteuliwa kwa Kichere kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi.

Alidai kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008 kinachoweka mihula miwili ya miaka mitano ya utumishi wa CAG, ambacho ndicho kilichotumika kuondolewa kwa Profesa Assad, kinakinzana na masharti ya Katiba.

Zitto alidai kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba ambayo inaeleza kuwa CAG atatumikia wadhifa huo mpaka umri wake wa kustaafu, yaani miaka 60 kikatiba au miaka 65 kisheria, sawa na kifungu 62(a) cha sheria hiyo kinavyoeleza.

Hivyo, alikuwa akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi, ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba na kwamba kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kutimiza umri wa kustaafu ni batili na pia uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya ni batili.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyosomwa jana ilikubaliana na hoja za Zitto kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi kuweka mihula ya miaka mitano mitano ya utumishi wa CAG ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba Ibara hiyo ya 44 ambacho kinaendana na Katiba.

Mahakama hiyo imesema kuwa wakati kifungu hicho kinaweka mihula ya utumishi wa CAG, Katiba inazungumzia umri wa kustaafu na si mihula.

Hivyo, Mahakama imesema kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kulikuwa ni batili.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imekataa maombi ya Zitto kutamka kuwa uteuzi wa Kichere ni batili, badala yake imesema kuwa uteuzi wake ni halali kwa kuwa aliteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu hukumu hiyo, Wakili Nshala amesema imeacha utata baada ya kukubali kuwa kuifungu hicho cha sheria kinachoweka mihula badala ya umri ni batili na kwamba Profesa Assad aliondolewa kinyume cha Katiba lakini ikasema kuwa uteuzi wa Kichere ni halali.

Zitto katika taarifa yake kwa umma akizungumzia kipengele hicho amesema kuwa amewaelekeza mawakili wake kukata rufaa Mahakama ya Rufani kwa lengo la kubatilisha uteuzi wa Kichere.

Wakili Nshala alisema kuwa wako tayari kwa maelekezo ya mteja wao, Zitto kukata rufaa Mahakama ya Rufani katika kipengele hicho ili kupata ufafanuzi zaidi.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniface Luhende alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia uamuzi huo, hakuweza kupatikana kwa kuwa simu yake haikuwa hewani.
Kwa hiyo kilichokiuka Katiba ni Sheria Namba 11 ya Mwaka 2008 na wala siyo Rais. Magufuli alitumia kifungu hicho kumtoa Prof. Kumbe tatizo ni watunga Sheria ambao walitunga kifungu batili. Mahakama imekifuta ili kisiendelee kuvunja Katiba
 
Are you sure of this?

Hii case imepewa namba 8/2022 maana yake imefunguliwa Samia akiwa madarakani, ulichoandika hapo juu kuwa ilifunguliwa Magufuli akiwa madarakani sio kweli.

Simply, Zitto alisubiri mpaka mama yake aingie madarakani ndio akafungue hiyo kesi, ndio maana sasa namtaka kama kweli Zitto sio mnafiki, kuna kesi nyingine Samia anavunja Katiba kwa kuzuia mikutano ya kisiasa, na yeye akiwa kama mdau, hivyo pia namshauri akamshtaki Samia.
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba hiyo kesi imefunguliwa miezi 4 iliyopita, na leo imetolewa hukumu?!

Hivi ulishawahi kujiuliza ikiwa inawezekana ikawa ni typing error na hivyo kuamua kuchunguza ili ufahamu exactly kesi ilifunguliwa lini?!
 
Kwa hiyo wote hawastahili kutuongoza maana woote wanatumia Akili za kuambiwa na wazungu!

Sijawahi Ona kiongozi wa upinzani mwenye hoja wa kizazi hiki tangu walipoondoka kina prof Baregu na Dk Slaa!

Hawa wa sasa ni makapi tupu!

Ebu fikiria taasisi Makini unaweza Mpa mtu kama Pambalu kuongoza hub ya chama yaani vijana?

Au hao CCM-Asali na wapaka Mikororogo wenye uteuzi wa kutia Shaka?

Tunaongozwa pande zote na opportunist tupu!

Woote wezi tupu!

Ila umamluki ni janga zaidi.

Mwanzo ulikuja na hoja za bendera fuata upepo, nilipokuambia kuhusu chama kilichoingia mikataba ya hatari dhidi ya nchi hii, ndio ukafikia hitimisho hili!
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu. Jee tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake? Apana Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu maono yao yalitafautiana sana.
Uko sahihi kabisa
 
Umeelewa lakini? Kilichopo ni mgongano kati ya Sheria na Katiba! Katiba inatamka kuwa mkaguzi mkuu atatumikia mpaka afikishe miaka 60 ndipo astaafu lakini sheria ya ukaguzi inatoa mwanya kuwa mkaguzi mkuu atakuwa na vipindi viwili vya utumishi katika kiti chake, yaani miaka 5 ya kwanza then ikimpendeza Rais atamteua tena, kwaiyo Magufuli aliutumia mwanya wa sheria ambayo inafafanunua Katiba, wakati uo Zitto alienda Mahamani kupinga kifungu hicho cha Sheria na kwa mujibu wa Sheria zetu, sheria yoyote inayokinzana na Katiba basi kifungu hicho ni batili.

Sheria za namna hii tunazonyingi sana katika Taifa letu! Ata lile la Ndugai kulazimishwa kujiuzulu ni sawa tu na ili la Assad sapo wanaoamua wanaangalia upepo kuwa sasahivi Magufuli hayupo basi hakuna cha kuhofia, ila now Samia yupo ndiye alitefanya Ndugai atoke basi ili haliwezi kukubaliwa kule!
Unaweza sema bora Magufuli alitumia mwanya wa kisheria kukinzana na Katiba ila Samia hakutumia lolote kwa Ndugai zaidi ya power aliyonayo.
Umedadavua vyema sana. Kwa kifupi ni kwamba Kifungu hicho cha sheria ndicho kilikuwa kinavunja Katiba na wala siyo Magufuli alivunja Katiba. Mahakama imeona hivyo na imekifuta. Magufuli alitumia kigungu kilichotungwa na Bunge ambacho kilikuwa kinyume na Katiba. Bunge lilitunga sheria inayokinzana na Katiba na hivyo leo imekuwa declared null and void na kufutwa lakini siyo null and void ab initio!!
 
Shida ni kwamba, wanaoitaji katiba mpya ni Olmsted 2% ya watanzania wote

So utapambana kuongea mambo ya katiba mpya and hakuna mtu atakuelewa

As long as mtu mambo yake yanaenda sawa, no problem

Hata katiba ya sasa ni watu wachache ndio wanaijua

Nani kakuambia kitu ili kibadilike lazima kila mtu akijue? Hizo katiba zilizoandikwa huko nyuma, wananchi wote walikuwa wameeIewa zilizokuwa hapo awali? Au ni mambo ya bendera fuata upepo?
 
Guys,

Naomba nielimishwe,,,

Hivi hawa watu inaoelekea ni Wafuasi wa JPM ni kipi kinawafanya watokwe povu kuhusu hii hukumu?!

What am I missing?!
 
Zitto na genge lake Udini unawasumbua sana. Acheni siasa za kupambana na Ukristo pimbi nyie
Wewe ndio pimbi kuu!
Udini kiaje? Ni wazi magufuli hakufuata katiba kwenye issue ya Assad.
 
Inawezekana kabisa marehemu JPM alivunja katiba, lakini, wewe Zitto tunakujua.
Umejaa roho ya visasi sana wewe. Una nyongo mbaya sana na marehemu sababu tu alikunyoosha na ubunge ukakosa.
Sasa hivi unajipendekeza kwa shangazi yako kisa dini zenu zinafanana huoni madudu ya shangazi.
Wengi wa Watanzania hawakupendi sababu ya siasa zako za hovyo hovyo.
 
Kati ya watu wamekuwa wa hovyo katika nchi hii waliotokea kumainiwa ni Zitto.... Sasa hivi kawa Hopeless, Useless, Untrustworthy, dubious..... Rotten one.... Written off.... Hajawahi kuwa na uchungu na nchi hii.... Ni mchumia tumbo wakuaminika..... Hovyo kabisa takataka....
 
Kwahiyo unaamini kabisa kwamba hiyo kesi imefunguliwa miezi 4 iliyopita, na leo imetolewa hukumu?!

Hivi ulishawahi kujiuliza ikiwa inawezekana ikawa ni typing error na hivyo kuamua kuchunguza ili ufahamu exactly kesi ilifunguliwa lini?!
Hata sioni ubachojaribu kukitetea hapa.

Case no. inatumika kuonesha mwaka kesi ilipofunguliwa, hiyo imeandikwa no 8 of 2022 sijui ndio unataka kubisha na kuita typing error, basi nipe namba ya kesi yako na mwaka wake tuione.
 
Shauri lilifunguliwa Magufuli akiwa hai, ila naona mahakama iliamua kupiga danadana kwa hofu, maana hakuna ambaye anafahamu yule bwana angamtenda nini jaji ambaye angeamua kutoa uamuzi sahihi.
We jamaa hebu ishi kwenye uhalisia, unataka kuniambia sasa hivi mahakama zinaweza kutoa hukumu kama hiyo kwa Samia hivi sasa?
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Taarifa kama hizi zinazidi kutufundisha kua kua na Taasisi imara ni muhimu sana kuliko kua ba mtu mmoja mmoja ambao ni imara.

Angekuepo JPM report hii msingeisikia.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Huyu jamaa alinyimwa posho na JPM...anashindana naye daily lkn bado anashindwa...ifikie hatua amuache mzee wa watu apumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom