Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Zito ni mjinga sana ni kipi anachokifanya huyu bi tozo ambacho ni tofauti na magufuli .
 
Yani Magufuli alikuwa zero. Anaiba uchaguzi ili ajaze wabunge wamuongezee muda wa kukaa madarakani, halafu anakufa hapo hapo. Mjinga kweli.
Aliyekufa ni mmoja lakini CCM inaendelea kubaki kileleni kwa Nguvu ile ile na utii ule ule kwa Amiri jeshi mkuu mpya
 
Amefarijika nini mnafiki mkubwa huyu zitto kabwe. Walimpa kichwa huyo cag kwamba hawezi timuliwa wakati kazi yenyewe siyo kajipa mwenyewe.
I hope wanasheria wa serikali watakata rufaa.

Hakutakiwa kutimuliwa, ila ubabe ukatumika.
 
Muendelezo wa vita kwa marehemu ndio imefanikisha kuwezekana kutoka hayo maamuzi bila ya hivyo sidhani kama ingewekana, maamuzi hayo yasingetoka Magufuli angekuwa bado yupo madarakani ni kama sasa rais aliye madarakani atavunja katiba na hakuna kitakachofanyika na ndio maana nikasema kilichotokea ni unafki tu ila wenye chuki na marehemu kwao kitu chenye kuwafurahisha.
Nilikuwa sifahamu kwamba kuna Vita Dhidi ya Marehemu....

Hata hivyo, bado nafahamu Rais pekee ambae hana bahati mbaya ya kusemwa semwa nchi ni Mwinyi peke yake!

Mwalimu Nyerere kafanya mambo mengi sana nchi hii, lakini bado hadi kesho anasemangwa, na wala sijawahi kusikia msamiati wa "Vita Dhidi ya Marehemu"

Jakaya kila siku anasemangwa lakini sijawahi kusikia msamiati wa "Vita Dhidi ya Mstaafu Jakaya"!

Kwamba, Rais wa sasa anaweza kuvunja katiba na hakuna kitakachofanyika... INAWEZEKANA KABISA!

Inawezekana kwa sababu SSH anatumia staili ya JK na sio ya JPM!

Bila shaka unakumbuka CHADEMA ya enzi ya JK ilikuwa STRONG kweli kweli... huku Mbowe, kule Slaa, pale kuna Mnyika, Lema nae yupo kibao... bila kumsahau Mdee, na wengine kadhaa!

Unakuta JK anafanya jambo linalopelekea full mapovu toka kwa akina Mnyika! Watafoka sana! Wataongea kadri wapendavyo, baada ya muda wanaitwa Ikulu "wakajadili" kuhusu suala husika!

CHADEMA na Gwanda zao, haoooo Ikulu... Kwavile mgeni lazima akaribishwe kinywaji, usishangae ukakuta unawekewa juicy kwenye glasi na JK mwenyewe!!!

Hapo watacheka, wanafurahi, na mwisho wa yote JK anawaahidi kufanyia kazi malalamiko yao!

Akina Tundu Lissu na ujanja wao wote ule watatoka hapo huku wakiwa wamekenua magego yote 49 lakini inakuwa ndo imetoka hiyo!! Hakua cha kufanyia kazi wala nini...

So, hakuna cha chuki hapo... it's all about how you handle your opponents!!
 
Kati ya watu wamekuwa wa hovyo katika nchi hii waliotokea kumainiwa ni Zitto.... Sasa hivi kawa Hopeless, Useless, Untrustworthy, dubious..... Rotten one.... Written off.... Hajawahi kuwa na uchungu na nchi hii.... Ni mchumia tumbo wakuaminika..... Hovyo kabisa takataka....

Ilaumu mahakama sio Zitto. Zitto alifungua kesi tu, mahakama ikatoa maamuzi dhidi ya Magufuli.
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Zitto ni mdini mtupu ndio maana kutimuliwa assad alivalia njugha na chuki kwa magufuli ilichangiwa na udini. Huko kigoma zipo tuhuma akiwa mbunge alijaa ubaguzi wa kidini.
Baada ya mama kua rais kwa udini akazima moto akawa sio mpinzani.
 
Unamuongelea Mbatia malaya wa siasa?! Ongelea mtu mwingine achana na huyo LGBT
Acha kukurupuka mzee! Hoja kujiuzulu kwa Ndugai nani alipeleka kesi mahakan! Kwanini alishindwa?
 
Wewe
Huna akili. Mamlaka ya uteuzi ndo nini?
Wewe una akili gani kazi ushabiki maandazi.Narudia tena Asad alipaswa ajiuzulu kulinda heshima yake, Rais hawezi kuwa submissive kwa CAG na ashukuru awakumuua,walimuondoa kiungwana.
 
Acha kukurupuka mzee! Hoja kujiuzulu kwa Ndugai nani alipeleka kesi mahakan! Kwanini alishindwa?
Mahakama inapofanya maamuzi kwanza huangalia whether kuna objectivity kwenye madai. Pili huangalia kama mlalamikaji ana masilahi kwenye suala Hilo. Sijui Mbatia aliambiwaje kwenye madai yake. Maana Ndugai alijiuzulu, sasa Mbatia ni nani akaombe judicial review kwa suala ambalo hana masilahi
 
Wewe
Wewe una akili gani kazi ushabiki maandazi.Narudia tena Asad alipaswa ajiuzulu kulinda heshima yake, Rais hawezi kuwa submissive kwa CAG na ashukuru awakumuua,walimuondoa kiungwana.
Unazidi kujionesha kwa kiasi gani huna akili. Eti kumuua? Wapi Rais amepewa mamlaka ya kumuua mtu chizi wewe??
Rais sio Mungu ni binadamu kama wewe aliyepewa mamlaka ya Urais na Katiba ambayo ndo hiyo hiyo imempa kinga huyo huyo CAG kuwa hawezi kuondolewa kwa chuki tu lazima ufuate taratibu zilizowekwa na katiba katika kumuondoa.

Kwa hiyo elewa Rais sio Mungu.
 
Hatimae Mahakama Kuu imethibitisha bila shaka Rais Magufuli na mwenyekiti wa CCM alivunja Katiba ya nchi iliyomuweka madarakani na aliyoapa kuilinda na kuitetea lakini akaivunja kwa kumwondoa CAG kinyume na Katiba.

Najiuliza hivi hakuwa na washauri? Au washauri wake wana uwezo mdogo juu ya Katiba? Je, waliomshauri watachukuliwa hatua gani?

Kuna watu walihoji uwezo mdogo wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali lakini wakapuuza lakini leo yametimia. Akili kubwa imeshinda Magufuli alivunja Katiba ya nchi.

View attachment 2437046
Kwahiyo anarudishwa kuwa CAG au atatakiwa kulipiga Bakora Kaburi lake mpaka Hasira za Kutumbuliwa Kwake ziishe?
 
Udini tuu zito ndo unaomsumbua kunya anye bata,samia alitymia sheria gani kwa ndugai.
 
Back
Top Bottom