Mwanadiplomasia Mahiri
JF-Expert Member
- Nov 4, 2019
- 491
- 1,907
Wewe sir elton john...huyo aliyekuwa anamtukana Membe alikuwa anatumwa na kulindwa na nani?Si kweli.
Kamshambulia aliyekuwa akimtukana mtandaoni.
Wapi kamtaja JPM?
ACHA UPOTOSHAJI WA KITOTO.
Kenge wewe
Zitto anajuwa ukweli maana pia inasemekana ni team X majasusi bana ujuwe hili tukio lakutisha sana amezima kama mshumaa ni ghafla...Mnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.
Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.
Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
El Commandante BCM ni gogo.....hakuwa mtu wa kukurupuka....vijana tujifunze.....Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023
Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili
Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.
Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.
Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.
Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.
Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo walituma mtu kumshambulia kwa tuhuma mbalimbali.
Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.
View attachment 2621369
Zitto KabweAidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.
Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.
“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe
Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
Ionee aibu nafsi yako mkuu....Tunaomba picha kama kweli kachomoka
Asiyekufa ni Mwenyezi Mungu tu......"Kachero mbobevu" aliyekufa kwa ugonjwa wa kifua.
[emoji120]Pumzika kwa amani Membe
Kwa hiyo ni kuamua kuununua ugomvi wa hao wanasiasa?. Safari bado ni ndefu kwetu sisi watanzania.Hawa wanasiasa ndio wa kwanza. Walimfanyia michezo marehemu. Wakasema maneno ambayo wazi yalikuwa ni kufuru.
Dunia hii haina mwenyewe. Mungu ndio mmiliki wake
Avae Sanda, kule Rondo wameshachimba pale pembeniZitto Kabwe amewaponda wote walioshabikia upuuzi aliofanyiwa Membe wakati Ule huku wengine wakimchafua kwa magazeti yaliyochapishwa na Mitambo " Vyombo"
Zitto anesema ana Imani wale wote waliomchafua Membe na kumtendea Uovu watajuta na wataenda kuomba radhi kaburini kwake
Source: ITV
Nawe pia utakufa kama nitakavyokufa mimi.....ionee aibu nafsi yako UNAYOIDHALILISHA hapa......Kapigwa moja tu
Aaaaaamin [emoji120]
Aaamin [emoji120]RIP BCM na RIP le mutuz
😂anafikiri nchi inaendeshwa kwa migebuka
Hakuna barakoa kama ni COVID-19Kuna tetesi wasaidizi wake walimtaka asihudhurie kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi na yeye ameng'ang'ania.
Huenda leo akaja na barakoa.
Nyongo imekwenda na upepoNafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Zitto amezungumza bila unafiki, ndivyo inatakiwa risala kutolewa.Nafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Mkuu "two wrongs doesn't make one right"......