Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Mnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.

Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.

Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
Zitto anajuwa ukweli maana pia inasemekana ni team X majasusi bana ujuwe hili tukio lakutisha sana amezima kama mshumaa ni ghafla...
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Mhe. Bernard Kamillius Membe, Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika Viwanja vya Karimjee - Dares Salaam leo tarehe 14 Mei, 2023



Saa 4:00 Asubuhi
Viongozi Mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri Mkuu wameanza kuwasili

Saa 5:45 Asubuhi
Mwili wa Marehemu Bernard Membe umewasili Karimjee ukiwa umebebwa kwenye gari Maalum la kubebea Maiti.

Saa 6:00 Mchana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan anawasili.

Rais Samia amekwenda moja kwa moja kusaini kitabu cha Maombolezo kilichoandaliwa, kisha kusalimia na kuwapa pole wafiwa.

Saa 6:05 Mchana
Dua na Sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Dini kisha salamu za viongozi wa Kiserikali na Kisiasa wamekaribishwa kutoa salamu zao.

Zitto Kabwe anazungumza; Amemuelezea Bernard Membe kama Mwanasiasa mkomavu aliyepambana kulinda heshima yake dhidi ya watu waoga walioshindwa kumkabili kwa hoja, ambapo walituma mtu kumshambulia kwa tuhuma mbalimbali.

Amesema Ushindi wake katika kesi ile utazika utamaduni huu mbaya wa kushambulia na kuchafua watu.

View attachment 2621369
Zitto Kabwe
Aidha, amemsifu kwa kusimama imara katika nyakati ngumu ambazo taifa lilipitia, nyakati ambazo watu wengi waliogopa kuisimamia kweli.

Amemshukuru kwa kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambapo aliwapa mafunzo na kuamsha ari ya kufanya kazi kwa bidii.

“Umetimiza wajibu, upumzike pema Membe… Tangulia BM, umeacha simanzi kubwa kwa watanzania. Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Upumzike pema mzee wangu Membe” Zitto Kabwe

Daniel Chongolo (Katibu Mkuu CCM) anazungumza; Amesema Chama cha Mapinduzi kimepokea kwa Masikitiko na Mshituko mkubwa kifo chake.
El Commandante BCM ni gogo.....hakuwa mtu wa kukurupuka....vijana tujifunze.....

Ameondoka akiwa na nishani ya VITA VYA KUMNG'OA NDULI IDD AMIN.....

Ameondoka akiwa na nishani mbili ZA USHUJAA kutoka serikali ya TANZANIA NA COMORO baada ya kufanikisha DEMOKRASIA NCHINI COMORO.....

Resty easy Comrade BCM[emoji120]
 
Sasa wale mnaotulaumu kushangilia misiba nafkr mmejionea , basi anzeni kuwashauri wenzenu ndo mje kwetu sasa , vinginevyo twende hv hv mdogo mdogo , ukifiwa mdogo mdogo unaenda kuchimba shimo unafukia then unarudi kilingeni kusikilizia
 
Zitto Kabwe amewaponda wote walioshabikia upuuzi aliofanyiwa Membe wakati Ule huku wengine wakimchafua kwa magazeti yaliyochapishwa na Mitambo " Vyombo"

Zitto anesema ana Imani wale wote waliomchafua Membe na kumtendea Uovu watajuta na wataenda kuomba radhi kaburini kwake

Source: ITV
Avae Sanda, kule Rondo wameshachimba pale pembeni
 
Nafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Nyongo imekwenda na upepo

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafuatilia kuaga mwili wa Hayati Bernard Membe kwenye runinga. Nimeipenda hotuba ya Zitto Kabwe maana hajamng'unya maneno katema nyongo kwa kusema ukweli. Tuwe wakweli kwa kusema ukweli na siyo kurembaremba hata pale ambapo mambo hayakwenda vizuri.
Zitto amezungumza bila unafiki, ndivyo inatakiwa risala kutolewa.
 
Back
Top Bottom