Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Zitto Kabwe: Membe alitupigania dhidi ya tabia Mbaya ya Watu wenye Mamkala kutumia Wahuni kutukana Viongozi wenzao

Mnaofatilia msiba wa Membe nafikiri mnamsikiliza sasa Zitto akimuelezea marehemu Membe.

Zitto badala ya kumuongelea Membe anaushambulia utawala wa Magufuli mpaka kumuita JPM mpuuzi.

Na kwanini wenzake wamepewa dakika mbili ila Zitto kapewa dakika zaidi. Zitto anachafua hali ya hewa...
Weka ushahidi wa video ili tuamini hiki ulichosema hapa.
 
Sifa za kijinga sana,kwa taarifa yako hasimami tena,hasimami tena!
Mkuu vipi kwema lakini?!!

Sijakufuru kwa kuandika kuwa mpendwa wetu ATASIMAMA....

Kwani mimi nikifa nitasimama tena?!!!

Kwani wewe ukifa utasimama tena ?!!! Una Siri ya kusimama tena baada ya kukata kwako roho?!!! tafadhali nipatie siri yako hiyo......
 
Labda kwavile Makonda yupo pia, lakini msibani sio eneo la kusutana.
 
Ukweli usemwe record ya Magufuli imeandika hivyo Duniani na mbinguni ya Membe pia imeandikwa hivi Duniani na mbinguni
 
Namuona Zito hapa na vazi lake jeupe tayari kwenda kuzikwa na Maembe. Kipara nae hatulii kila saa kugeuka nyuma tu kwa kina Lukuvi anafosi tabasamu na kucheka kwingi, hivi hajui kama the next ni dingi yake?
Ooooohh.
 
Ni group la whatsapp la wake wa viongozi hasa wale ambao waume wao wako na post kubwa. Waziri, RC, speaker na kuna wake wa maraisi pia ambao ni walezi wa hilo group.
 
Mbona kaongea vizuri tu sijaskia akiongelea habari za jiwe.
 
Najua tuko kwenye huzuni, ila maneno yako, hata yangejaa pipa, hayawezi kubadili chochote kwa sasa. Too late!
Lolote limhusulo Muumba wetu, hakuna wa kumpangia maana hekima ya Mungu si hekima ya mwanadamu.

Tunaweza kuona tunanena vyema sana, kumbe ikawa ni takataka mbele zake. Tunaweza kumwona mtu akinena takataka, lakini ikawa ni hekima mbele za Mungu.

Lakini pa.oja na hizo hali zote, hatuwezi kuacha kunena, ila yeye ndiye mwamuzi.
 
Zitto Kabwe amewaponda wote walioshabikia upuuzi aliofanyiwa Membe wakati Ule huku wengine wakimchafua kwa magazeti yaliyochapishwa na Mitambo " Vyombo"

Zitto anesema ana Imani wale wote waliomchafua Membe na kumtendea Uovu watajuta na wataenda kuomba radhi kaburini kwake

Source: ITV
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hebu atutolee kelele zake hapa, km anampenda sana marehemu akafukiwe nae.

Atupishee sie
 
Unafanyia reference biblia wakati mwenzake alipokufa alimcheka?
Hayo tunamwachia yeye na Mungu wake. Wanadamu hatujapewa mamlaka ya kuhukumu bali tumepewa utashi wa kumwambia mwanadamu mwenzetu yale yaliyo mema.
 
Kamarada Tegga tunaomba kwa imani....

Hata mimi nikifa ,ndugu zangu wataomba kwa IMANI Ila wewe usiniombee....

Hata wewe ukifa ,ndugu zako wataomba kwa IMANI nami nitakuombea.....
Pole sana. Pole sana. Pole sana. Nimerudia mara tatu, mkuu.
 
Back
Top Bottom