PreGE2025 Zitto Kabwe: Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, Karibuni ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
"Kwa wale Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, wasivunje madirisha wala nyumba! KARIBU ACT Wazalendo tufanye Siasa.

Tunaweza kuleta mageuzi tukiwa mchezoni. Uchaguzi ni jukwaa la kuelimisha na kuamsha umma (mobilization). Uchaguzi ni jukwaa la kuionyesha dunia tunachopigania (exposing the flaws)."

Zitto KabweView attachment 3306274
COVID 19 waende huko Watapata fursa.
 
Shida ndio hiyo. Mnajiona kuwa mnajua kuliko wananchi. Hicho kiburi ndio kinachowafanya muone kuwa mna haki ya kuburuza wanachama wote wa CDM mkisahau kuwa mgombea wenu alipata 51.5% za kura na mshindani wake alipata 48.2%. Badala ya kutambua kuwa karibu nusu ya wawakilishi wa wanachama walikuwa na imani na Mbowe nyinyi mnaendelea kumfanyia yeye na wafuasi wake figisu figisu.

Ukiangalia kuwa hamna chama kinachowaunga mkono, mkijumlisha karibu nusu ya wawakilishi wa wanachama wa Chadema nao hawakuwakubali ni dhahiri kuwa asilimia kubwa ya raia hawaungi mkono strategy yenu. Lakini ukweli utajulikana hivi karibuni.

Amandla...
Huhitaji kuungwa mkono na vyama vingi unapokuwa na hoja za msingi. Historia ya hivyo vyama unavyotaka viwaunge mkono cdm inafahamika. Rais sio vyama boss, raia wanaounga mkono hoja za cdm wanajitosheleza, cdm haihitaji kumlazisha yoyote akibaliane na hoja yao. Ila mradi ni hoja za msingi hiyo inatosha.
 
Unasema Bunge halina impact wakati Spika wa Bunge hilo hilo amewapigia kifua Covid-19 na hamkuweza kumlazimisha kumtimua. Ni Bunge hilo hilo ndio lililopotisha sheria ya mabadiliko makubwa katika Tume ya Uchaguzi kwa kuongeza neno "huru". Katika kumbukumbu za Bunge linalomaliza muda wake ACT-WAZALENDO ina wabunge wanne, CUF ina mbunge mmoja na CDM ina wabunge 20. Hiyo ndio halisi.

Amandla...
Hapo umetaja impact ama wingi? kukomoa sio impact boss.
 
"Kwa wale Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, wasivunje madirisha wala nyumba! KARIBU ACT Wazalendo tufanye Siasa.

Tunaweza kuleta mageuzi tukiwa mchezoni. Uchaguzi ni jukwaa la kuelimisha na kuamsha umma (mobilization). Uchaguzi ni jukwaa la kuionyesha dunia tunachopigania (exposing the flaws)."

Zitto KabweView attachment 3306274
Hapa kisiwa cha kusadikika wajanja wanafaidi sana keki ya taifwa.
 
Hapo umetaja impact ama wingi? kukomoa sio impact boss.
Impact inaweza kuwa negative au positive. Uwepo wa Covid-19 una impact kubwa katika uhalisia wa siasa za Tanzania. Sidhani kama lengo lilikuwa ni kuikomoa CDM. Lengo lilikuwa ni kulipa Bunge uhalali ambao bila Covid-19 usingekuwepo. Walichotaka ni wabunge wa upinzani na hawakujali wanatoka wapi. Kwa wakati ule ni CDM peke yake ndio ingeweza kuwatoa na wakakubalika kitaratibu. Na walifanikiwa.

Hata wasingekuwepo bado siasa za Tanzania zingekuwana impact hiyo hiyo. Usitake kufanya uwepo wao umesaidia mahusiano ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
 
"Kwa wale Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, wasivunje madirisha wala nyumba! KARIBU ACT Wazalendo tufanye Siasa.

Tunaweza kuleta mageuzi tukiwa mchezoni. Uchaguzi ni jukwaa la kuelimisha na kuamsha umma (mobilization). Uchaguzi ni jukwaa la kuionyesha dunia tunachopigania (exposing the flaws)."

Zitto KabweView attachment 3306274
Jiwe limerushwa gizani.
 
Hata wasingekuwepo bado siasa za Tanzania zingekuwana impact hiyo hiyo. Usitake kufanya uwepo wao umesaidia mahusiano ya Tanzania na jumuiya ya kimataifa.
Wasingekuwepo Bunge lisingeweza ku operate kama kanuni zinavyotaka. Kuna kamati za bunge ambazo ni lazima ziwe na uwakilishi kutoka vyama vya upinzani. Nadhani kuna kamati ambazo mwenyekiti wake anatakiwa atoke vyama vya upinzani. Wabunge kutoka upinzani waliotangazwa kushinda wasingetosha. Uwepo wa Covid-19 uliliwezesha kamati za bunge kutimiza masharti hayo. Aidha, uwepo wao umeiwezesha serikali kujinadi kuwa ni bunge lake ni la kidemokrasia maana lina wabunge wa upinzani.

Narudia tena, hata wasingekuwepo hayo yangeendelea boss. Serekali inajinadi ni ya kidemokrasia maana wabunge wa upinzani wapo ndani ya bunge! Kwamba hao wanaoambiwa hawaujui ukweli hadi wasubiri kuambiwa na serekali? Kwamba hao wanaombiwa wako huko makwao hawaujui ukweli, hadi wasubiri kupelekewa taarifa na serekali?
 
Hivi huyu jamaa,ukimtoa kwenye siasa,anaweza kufanya shughuli gani?
Career politicians.
 
Narudia tena, hata wasingekuwepo hayo yangeendelea boss. Serekali inajinadi ni ya kidemokrasia maana wabunge wa upinzani wapo ndani ya bunge! Kwamba hao wanaoambiwa hawaujui ukweli hadi wasubiri kuambiwa na serekali? Kwamba hao wanaombiwa wako huko makwao hawaujui ukweli, hadi wasubiri kupelekewa taarifa na serekali?
Hawasubiri kuambiwa na serikali lakini wanashuhudia kuwa kuna wabunge wa upinzani. Unadhani hao mnaotaka kuwapelekea hizo petition hawajui kinacho endelea nchini? Hao wote mnaotaka wawapigie kifua wana wawakilishi wao nchini. Ukweli ni kuwa interest yao zaidi ni utulivu na amani, sio haki. Hayo ya haki ni ya wakina Amnesty International. Mataifa ya magharibi yanachotaka ni pasitokee machafuko ya aina yeyote ili waweze kuendelea kufanya biashara na nchi isiwe source ya wakimbizi. Ndio maana wanawaangalia tu viongozi wa Uganda, Rwanda, Saudi Arabia n.k. Wanajua wakina Halima waliingia vipi Bungeni lakini hawako tayari kuingilia kati waziwazi.

Naona tuishie hapa maana naona tunazungumza lugha tofauti na kukubaliana chochote.

Amandla...
 
Wamevurugwa wengi Mzee Mbowe pia inasemekana alitaka kugombea jimbo lake la Hai !!!!

sasa sijui nayeye anapiga esabu ya kuamia ACT!!!
Msiba mzito kaleta yule muuni wa Belgium !!!!!!
 
Back
Top Bottom