PreGE2025 Zitto Kabwe: Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, Karibuni ACT Wazalendo

PreGE2025 Zitto Kabwe: Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, Karibuni ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mkuu mbona una kichwa kigumu hivyo?? CDM haina tamaa wala uroho wa madaraka. Wanachafanya hivi sasa na kupigania mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi. Utakaowasaidia hata hao wenye tamaa ya madaraka kwenye vyama vyao, kuweka usawa kwenye ushindani.
Mimi sipendi matusi. Nipinge kwa hoja lakini sio kwa kuniita kichwa kigumu. Vyama karibu vyote vya upinzani vinataka mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi isipokuwa hawakubaliani na strategy ya CDM. Badala ya kututukana tuambieni mtawashurutisha vipi CCM wafanye mabadiliko mkiwa peke yenu? Na mtafanya nini kama tutafika 2030 bila reforms?

Amandla...
 
Ni kupoteza muda tu! Act wazalendo haiwezi kushinda hata kiti kimoja kwa kanuni hizi za uchaguzi!
Tatizo lenu ni kuwa mnadhani uchaguzi unafanyika bara tu. Kuna mwaka ACT-WAZALENDO walinyimwa ushindi kwa figisu figisu katika uchaguzi maalam Zanzibar wakakiwasha mpaka mgombea wa CCM aliyetangazwa mshindi akajiuzuru. Hamna namna ACT-WAZALENDO itakosa wabunge na wawakilishi Zanzibar. Hata CCM wanajua hilo.

Amandla...
 
Chama pekee cha upinzani chenye uhakika wa kuwa na wabunge baada ya uchaguzi bila upendeleo ni ACT-WAZALENDO. Watapata wabunge kutokana kukubalika kwao Pemba na sehemu za Unguja. Wanachohitaji ni kuongeza wabunge wa kutosha kutoka Bara ambapo CDM wana mvuto zaidi. CDM wamewapa hiyo nafasi kwa kucheza vibaya karata zao. Na wanazidi kujiharibia kwa namna wanavyo wasimanga wanachama wao wanaotofautiana nao kimkakati.

Wanachofanya ACT-WAZALENDO ni kama walivyofanya CDM kwa kumuunga mkono mgombea wa urais Zanzibar badala ya wa kwao. Kama nakumbuka vizuri kuna wakati mgombea mwenza wa urais wa CDM alitoka ACT-WAZALENDO.

Amandla...
Kama kuna kitu cdm wanajivunia ni kuwa na wafuasi wanaojitambua. Wengi wa wanaohama cdm ni waenda kusaka vyeo. Lakini eti wafuasi wahame kwenda kuwapigia kura walioamua kushiriki uchaguzi utakuwa unajidanganya.
 
Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo. Ukweli ni kwamba hata kama wafuasi wote wa CDM watasusia uchaguzi, mshindi atatangazwa na ndie atashika nafasi. Hamna suala la quorum kwenye uchaguzi. Mkiwaachia wapiga kura wa CCM na ACT-WAZALENDO wapige kura peke yao, wagombea wao ndio wataingia Bungeni. Mnaojidanganya ni nyinyi mnaodhani kususia kwenu kutakuwa na impact yeyote nje ya Clubhouse.

Kwani sasa hivi kwenye chaguzi walizoshiriki wana wabunge gani? Hata hivyo hilo bunge lina impact gani hadi useme wasipopata wabunge watakosa impact?
 
Mimi sipendi matusi. Nipinge kwa hoja lakini sio kwa kuniita kichwa kigumu. Vyama karibu vyote vya upinzani vinataka mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi isipokuwa hawakubaliani na strategy ya CDM. Badala ya kututukana tuambieni mtawashurutisha vipi CCM wafanye mabadiliko mkiwa peke yenu? Na mtafanya nini kama tutafika 2030 bila reforms?

Amandla...
Mimi sipendi matusi. Nipinge kwa hoja lakini sio kwa kuniita kichwa kigumu. Vyama karibu vyote vya upinzani vinataka mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi isipokuwa hawakubaliani na strategy ya CDM. Badala ya kututukana tuambieni mtawashurutisha vipi CCM wafanye mabadiliko mkiwa peke yenu? Na mtafanya nini kama tutafika 2030 bila reforms?

Amandla...
Cdm haihitaji kubembeleza chama chochote kujiunga nacho kwenye kutaka mabadiliko. Wanachotakiwa ni wananchi kuwaelewa tu. Sasa chama kama SAU, JAHAZI Asili unataka ujiinge nacho upate nini? Umewahi kuwaona hata wakifanya mkutano wa hadhara. Kama kuna mahali cdm watachemka ni kutaka kuwa na umoja na hayo matawi ya ccm.
 
Uzuri wale njaa 55+covid19 wote ni ccm na Act nao ni ccm sass wataamua nani apewe jimbo. Huku chadema tunaendelea kukabia juu na NRNE.
 
Cdm haihitaji kubembeleza chama chochote kujiunga nacho kwenye kutaka mabadiliko. Wanachotakiwa ni wananchi kuwaelewa tu. Sasa chama kama SAU, JAHAZI Asili unataka ujiinge nacho upate nini? Umewahi kuwaona hata wakifanya mkutano wa hadhara. Kama kuna mahali cdm watachemka ni kutaka kuwa na umoja na hayo matawi ya ccm.
Shida ndio hiyo. Mnajiona kuwa mnajua kuliko wananchi. Hicho kiburi ndio kinachowafanya muone kuwa mna haki ya kuburuza wanachama wote wa CDM mkisahau kuwa mgombea wenu alipata 51.5% za kura na mshindani wake alipata 48.2%. Badala ya kutambua kuwa karibu nusu ya wawakilishi wa wanachama walikuwa na imani na Mbowe nyinyi mnaendelea kumfanyia yeye na wafuasi wake figisu figisu.

Ukiangalia kuwa hamna chama kinachowaunga mkono, mkijumlisha karibu nusu ya wawakilishi wa wanachama wa Chadema nao hawakuwakubali ni dhahiri kuwa asilimia kubwa ya raia hawaungi mkono strategy yenu. Lakini ukweli utajulikana hivi karibuni.

Amandla...
 
"Kwa wale Wanasiasa ambao wanataka kufanya siasa lakini milango imefungwa kwenye vyama vyao, wasivunje madirisha wala nyumba! KARIBU ACT Wazalendo tufanye Siasa.

Tunaweza kuleta mageuzi tukiwa mchezoni. Uchaguzi ni jukwaa la kuelimisha na kuamsha umma (mobilization). Uchaguzi ni jukwaa la kuionyesha dunia tunachopigania (exposing the flaws)."

Zitto KabweView attachment 3306274
Ditto ni chawa na mchmia tumbo siku zote na yuko n atakufa hivyo
 
Kwani sasa hivi kwenye chaguzi walizoshiriki wana wabunge gani? Hata hivyo hilo bunge lina impact gani hadi useme wasipopata wabunge watakosa impact?
Unasema Bunge halina impact wakati Spika wa Bunge hilo hilo amewapigia kifua Covid-19 na hamkuweza kumlazimisha kumtimua. Ni Bunge hilo hilo ndio lililopotisha sheria ya mabadiliko makubwa katika Tume ya Uchaguzi kwa kuongeza neno "huru". Katika kumbukumbu za Bunge linalomaliza muda wake ACT-WAZALENDO ina wabunge wanne, CUF ina mbunge mmoja na CDM ina wabunge 20. Hiyo ndio halisi.

Amandla...
 
Lissu aliishasema kuwa mazungumzo yameanza na baadhi ya hao mnaowaita Covid-19. Kwa hiyo nae ni msaliti?

Amandla...
Ndio amesema unajua ni wangapi? Na unajua yataisha lini? Una hakika gani kama watakubaliwa?
 
Back
Top Bottom