Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Uchaguzi 2020 Zitto: Kura yangu nafasi ya Urais nitampigia Tundu Lissu (CHADEMA)

Na Mimi Kura Kwa Lissu!

1. Uhuru- Saivi tunaishi kwa wasiwasi uki- comment tu hata huko twitter kukosoa unaweza kujikuta una kesi ya money laundering....
Hivi wanaompinga Tundu Lissu, haya hawayaoni jamani au nao ni wanufaika na mfumo wa Dhurma na ukandamizaji?
 
Andiko hili limetaka kuniliza kabisa duh ..

Andiko moja la kizalendo Sana

Zitto tunachukua nchi mapema Sana October 28.

Kila dalili zinaonyesha hakuna Mtu wa kumzuia Lissu Labda Mungu pekee....
Hahahaha nakubaliana na wewe kabisa...Kila dalili za mitandaoni zinaonesha Lissu ndiye Rais ajaye ingawa hata kwenye mitandao mambo naona yanabadilika kwa kasi
 
ZITO KABWE INAMAANA MWALI WAKO BENADI MEMBE UMESHAMTOSA MARA HII? MEMBE NDOTO ZAKE ZA KUWA RAIS NA KUMTOA RAISI MAGUFULI ASUBUHI, SASA UMEMUGEUKA??
 
Hahaah! tulukuonya na kukushauri kwaba Membe nje ya CCM ni sawa na Nyuki wa Mashineni, hang'ati ukajibu kwa kejeli ukasema Membe amefukuzwa CCM kwa kumkosoa Mwenyekiti wake na anauzika sio kama Lowassa. Get a strap!
 
Ulituaminisha Membe sasa Unatuaminisha LISSU ...huu ni utapeli wa kisiasa
 
I think You should start using yours as well. Mtego upi? Tell me. Yaani mtego uwe set kwa nafasi ya urais tu ila sio kwa Wabunge au Madiwani?
Wewe ni wa nchi hii au??
Wakati wa EL kuliibuka kauli ya goli la mkono...
Wakati huu wanadai hata kura zikipigwa bado ccm wataunda serikali...
Tumia akili ya ziada kuelewa hizo kauli...
 
Zitto mbona wewe na mgombea wako mnapishana kauli, mnaleta mkanganyiko kwa wanachama wenu na watanzania kwa ujumla, ni kama vile kuna mgogoro ambao haueleweki ndani ya chama chenu na mmeamua kuuweka publicly kwa kupishana kauli
Jaribuni kuwa na kauli moja or either muwaeleweshe watanzania msimamo wenu kama chama ni upi maana haiwezekani chama kinampigia kampeni mgombea wa chadema na mgomea wenu yupo wala hafanyi kampeni and
at the same time amekomaa tu kwamba yeye ndio mgombea halali wa urais na atashinda kwa kimbunga

Hii inasababisha muonekane hampo makini na hamjui mnachokifanya
 
Hiyo barua ya Msajili ya kujieleza kwa nini Maalim alipanda jikwaa moja na Lissu, msiijibu kabisa. Kaukeni tu. Haina mashiko kisheria.
MSIMAMO RASMI WA ACT WAZALENDO KUSHIRIKIANA NA CHADEMA.

Hivyo basi, baada ya maelezo hayo, natangaza rasmi kwa Wanachama, Wafuasi, wapenzi wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa Ujumla, kuwa:

1. Pale kwenye Kata ama Jimbo ambalo ACT Wazalendo tuna Mgombea, tunaomba Muwapigie Kura wagombea wa ACT Wazalendo.

2. Pale ambapo kwenye Kata au Jimbo la Uchaguzi hakuna Mgombea wa ACT Wazalendo, lakini kuna wagombea wengine wa Vyama vya Upinzani, ACT Wazalendo tunawaomba MPIGIE KURA MGOMBEA WA CHAMA CHA UPINZANI mwenye nguvu zaidi ili kutokutawanya Kura.

3. Kwa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe NITAPIGA KURA YANGU kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai LISSU. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda Mgombea wa Chama tawala, amefanya kampeni nchi nzima, mwitikio wa Wananchi kwake ni mkubwa sana, ameeleza kwa ufasaha dhamira yake ya kuleta mabadiliko na sina mashaka na dhamira hiyo, pamoja na anayotaka kuyafanya kama Rais, ni mambo hayo ndiyo yaliyonipa msukumo wa kumpigia Kura Lissu.

Zaidi NINAMUAMINI LISSU kutokana na historia yake ya kupigania Haki za Watu. Ninaomba kila mpenda Haki na Mabadiliko nchini ampigie kura ya URAIS ndugu Tundu Lissu ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Natanguliza Shukran kwenu

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bangwe, Kigoma Mjini
Oktoba 16, 2020
 
ZITTO kajivua uanachama wa ACT WAZALENDO kakiuka katiba kifungu hiki hapa
1603289807414.png
 
Mtajua hamjui mwaka huu. Kinachokuuma wewe ni nini?? Sisi wana ACT tunaungana na Zitto.
Haya sasa wana ACT wenzako huko wanasema Zitto kabwe na Maalim seifu wamekosa sifa za kuwa wanachama wa ACT wamevunja katiba.
 
Haya sasa wana ACT wenzako huko wanasema Zitto kabwe na Maalim seifu wamekosa sifa za kuwa wanachama wa ACT wamevunja katiba.
Hao nao wataangukia pua kama alivuoanguka Lipumba mpka leo anahutubia mawe.😅😅😅
 
Back
Top Bottom