#COVID19 Zitto: Nimepima, nimekutwa na maambukizi ya UVIKO. Naendelea vema

#COVID19 Zitto: Nimepima, nimekutwa na maambukizi ya UVIKO. Naendelea vema

"Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa" - propaganda imeanza hapa..kila la heri
 
Juzi ulikuwa kwenye kikao,uliugua lini,ulizidiwa lini? Umepata nafuu lini?

Umemaliza kutumika kwenye issue ya Mbowe,umeamua kutumika Kama dalali wa Corona?

JPM alishatuondolea hofu,kawatishe wa kwenu Kigoma,sisi Corona ni mafua ya kawaida.
Neema ya Bwana yatosha.
someone"s medical information is for his either his own use or share with his/her personal doctor. Tuambie basi na mengine unayoumwa kama wewe umeamua kuwa muwazi
 
Wale wote waliokuzunguka wapimwe
 
Jana nimepima nikakukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu lakini nimekutwa positive.

Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa. Nimekaa eneo tengwa (isolation) ili kutoambukiza wengine mpaka hapo nitakapopima tena.

Nawaomba muendelee kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na kujiepusha na mikusanyiko.

Corona bado ipo, chukua tahadhari na walinde wengine.
Hii hatari Sasa, maana juzi umekua kwenye kikao Cha vyama, WENDA wameisha ukwaa wengine mliokua nao

Pole Sana aisee
 
Jana nimepima nikakukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu lakini nimekutwa positive.

Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa. Nimekaa eneo tengwa (isolation) ili kutoambukiza wengine mpaka hapo nitakapopima tena.

Nawaomba muendelee kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na kujiepusha na mikusanyiko.

Corona bado ipo, chukua tahadhari na walinde wengine.
hamia ccm upewe shavu.
 
Huku mtaani watu wengi wnalalama juu ya maumi u ya mwili , mafua, kihozi na mwili kuchoka sijui Kama yaweza kuwa Corona ama no hii transition ya kutoka kwenye jua Kali na joto na kuja kwenye Mvua.
Pole Mkuu.
 
Pole mkuu. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, wewe utakuwa mgonjwa wa kwanza Tanzania ktk wimbi hili la sasa!!
Jana nimepima nikakukutwa na virusi vya Korona (COVID 19). Sina maumivu yoyote mpaka sasa zaidi ya mafua tu lakini nimekutwa positive.

Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa. Nimekaa eneo tengwa (isolation) ili kutoambukiza wengine mpaka hapo nitakapopima tena.

Nawaomba muendelee kuchukua tahadhari kwa kuvaa barakoa, kunawa maji tiririka na kujiepusha na mikusanyiko.

Corona bado ipo, chukua tahadhari na walinde wengine.
 
nimetafakari kwa mda, kikao kinaendelea kuzungumzia issues za kisiasa nchini.

bwana zitto alimuombea msamaha mtuhumiwa Mbowe mwenyekiti wa chama cha chadema, jambo ambalo lilizua taharuki hasa kwa viongozi wa chadema akiwemo bwana lema na bwana lissu.

jee kweli zitto mgonjwa au kakwepa kujumuishwa kwenye maazimio yatayofikiwa?

jee anataka kujitetea huko mbele ikiwa matarajio hayatakua kama alivyotaraji ?
 
Nisiwe msemaji wake ila nimeamua kumpa benefit of doubt.
 
Unapenda Sana attention Kaka Zitto , Sasa ukiugua mafua tuu unautangazia Umma. Umma wa Watanzania hauna maslahi na kuugua kwako.
 
Kwani wanapoenda kwenye mikutano inayohudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi hawapimwi Corona?
 
Ni kuwatisha wahudhuriaji ili wasitishe mkutano kwa kuwa mmoja wao amekutikana na UVIKO 21
 
Si wa chama tawala wala wa upinzani, wanasiasa wa rangi zote wanashangaza sana.

Ni kuhusu suala la uviko 19. Huku mtaani watu tunaishi maisha yetu bila hofu yoyote ile ya covid. Si kwamba hatuamini kwamba hakuna covid bali tunaamini kama wananchi tuna changamoto za kushughulika nazo zaidi ya covid.

Sasa swali langu la msingi linabaki: hawa jamaa wanamwakilisha nani hasa? Wanamwakilisha mwananchi wa kawaida kutoka Kariakoo au Mwandiga kweli? Hapa nilipo nimetype hii post nikiwa kwenye kijiwe changu cha draft, wote tupo hapa maskless, unvaccinated.

No wonder Magufuli anabaki kuishi katika mioyo ya watanzania, the guy had a lot of common sense. Mtu unaishi Tanzania utatuleteaje slogans za Anthony Fauci wa Maryland? As if hujui hali halisi ya nchi yako na watu wake. Mkoloni alichokifanya kwenye kichwa cha mtu mweusi anakijua yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom