#COVID19 Zitto: Nimepima, nimekutwa na maambukizi ya UVIKO. Naendelea vema

"Chanjo imesaidia kutopata madhara makubwa" - propaganda imeanza hapa..kila la heri
 
Ushauri mzuri, ila ni ngumu kuchanja
 
someone"s medical information is for his either his own use or share with his/her personal doctor. Tuambie basi na mengine unayoumwa kama wewe umeamua kuwa muwazi
 
Wale wote waliokuzunguka wapimwe
 
Hii hatari Sasa, maana juzi umekua kwenye kikao Cha vyama, WENDA wameisha ukwaa wengine mliokua nao

Pole Sana aisee
 
hamia ccm upewe shavu.
 
Huku mtaani watu wengi wnalalama juu ya maumi u ya mwili , mafua, kihozi na mwili kuchoka sijui Kama yaweza kuwa Corona ama no hii transition ya kutoka kwenye jua Kali na joto na kuja kwenye Mvua.
Pole Mkuu.
 
Pole mkuu. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, wewe utakuwa mgonjwa wa kwanza Tanzania ktk wimbi hili la sasa!!
 
nimetafakari kwa mda, kikao kinaendelea kuzungumzia issues za kisiasa nchini.

bwana zitto alimuombea msamaha mtuhumiwa Mbowe mwenyekiti wa chama cha chadema, jambo ambalo lilizua taharuki hasa kwa viongozi wa chadema akiwemo bwana lema na bwana lissu.

jee kweli zitto mgonjwa au kakwepa kujumuishwa kwenye maazimio yatayofikiwa?

jee anataka kujitetea huko mbele ikiwa matarajio hayatakua kama alivyotaraji ?
 
Nisiwe msemaji wake ila nimeamua kumpa benefit of doubt.
 
Unapenda Sana attention Kaka Zitto , Sasa ukiugua mafua tuu unautangazia Umma. Umma wa Watanzania hauna maslahi na kuugua kwako.
 
Kwani wanapoenda kwenye mikutano inayohudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi hawapimwi Corona?
 
Ni kuwatisha wahudhuriaji ili wasitishe mkutano kwa kuwa mmoja wao amekutikana na UVIKO 21
 
Si wa chama tawala wala wa upinzani, wanasiasa wa rangi zote wanashangaza sana.

Ni kuhusu suala la uviko 19. Huku mtaani watu tunaishi maisha yetu bila hofu yoyote ile ya covid. Si kwamba hatuamini kwamba hakuna covid bali tunaamini kama wananchi tuna changamoto za kushughulika nazo zaidi ya covid.

Sasa swali langu la msingi linabaki: hawa jamaa wanamwakilisha nani hasa? Wanamwakilisha mwananchi wa kawaida kutoka Kariakoo au Mwandiga kweli? Hapa nilipo nimetype hii post nikiwa kwenye kijiwe changu cha draft, wote tupo hapa maskless, unvaccinated.

No wonder Magufuli anabaki kuishi katika mioyo ya watanzania, the guy had a lot of common sense. Mtu unaishi Tanzania utatuleteaje slogans za Anthony Fauci wa Maryland? As if hujui hali halisi ya nchi yako na watu wake. Mkoloni alichokifanya kwenye kichwa cha mtu mweusi anakijua yeye mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…