Pre GE2025 Zitto: Tumepata Taarifa Nondo yuko Kituo cha polisi Gogoni, Tumefika tumekuta gari inabadilishwa Plate namba

Pre GE2025 Zitto: Tumepata Taarifa Nondo yuko Kituo cha polisi Gogoni, Tumefika tumekuta gari inabadilishwa Plate namba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tumejulishwa kuwa Mwenyekiti wa Vijana Taifa Ngome ya Vijana, Abdul Nondo amefichwa kituo cha polisi Gogoni, Kibamba Dar es Salaam.

Tumefika Kituoni, ingawa Polisi wamekataa, tumekuta Landcruiser iliyotumika kumteka Nondo ikiwa inabadilishwa number plates. (kutoka zile za IST zilizotangazwa na Msemaji wa polisi na kuwekwa zingine).

Soma Pia: Kuelekea 2025 - News Alert: - Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli

Picha chini ndio gari iliyomteka Nondo ikiwa Kituo cha Polisi Gogoni, Kibamba.
View attachment 3166701

Polisi ni dhahiri mpo na Nondo, tafadhali mwacheni huru akiwa mzima wa afya BILA HATA MCHUBUKO! Tafadhali Tafadhali Tafadhali!
This is too much or we have to wait to take the actions against all police in all over the country.
 
Watu kama hawa ni wakuwapuuza
Kuwapuuza tu haitoshi Inabidi kuwambia kwamba hawana mchango wowote!
Tunataka watu wajihusishe na siasa Ili kuhanikiza sera ambazo ni rafiki kwa maendeleo ya watu wote katika nchi..

Tunataka vijana wataokua sehemu ya maamuzi Ili kubadili mifumo na sera zinazosababisha ukosefu wa Ajira, huduma mbaya na duni za afya, matumizi mabaya ya fedha za umma, elimu isyomuwezesha mtu kujikwamua kimaisha! Hatuwataki watu wajihusishe na siasa kama sehemu ya kupata umaarufu na kujilimbikizia utajiri!
 
Police wanakuwa kama genge la wahuni. Sasa wananchi watapata wapi msaada?
Msaada upi Mzee unaotarajia,naamin wanaofanya vitendo Hv ni wachache sana na wameachwa waendelee,ktk Maandiko matakatifu hakuna sehemu mwanamke anatajwa kama kiongozi hakuna na haitatokea Tanzania tumekanyaga mavi na hayo mavi yatatutesa sana.
 
Huyu dogo aliwahi jiteka lakini.

Alikuwa na kesi Iringa pale mahakama ya wilaya.

Kajinga flani hivi.
 
Kabisa Zitto ni noma !!Kwa Zitto ukiona Nondo amepotea ujue hicho kituo takriban polisi watano watakufa au kupata ulemavu .

Zitto ni habari nyingine achana n yule mwamba
Acheni kumpa mtu sifa za kipumbavu tunajadili mambo ya msingi sana hapa halafu mtu mjinga anasema Zitto ni noma,tujadili situation hii ndani ya Taifa letu na kwa umoja wetu tuone tunafanya nini kukomesha utekaji unaofanywa na vichaa,maana sababu ya kuteka ni ya kipumbavu tu.
 
Halafu
mi nashauri vijana waachane na siasa tu maana wanageuzwa mbuzi wa kafara na wakuu wa vyama vyao,kwanza tanzania upinzani hakuna haiwezekani kinatawala chama kimoja miaka nenda rudi,hakuna cha demokrasia ni udikteta tu
Nani afanye siasa
 
Acha unaa ,hujui kama ile kesi alishinda,baada ya polisi kushindwa kuithibitishia mahakama,tusiwe wapuuzi kwa maisha na haki Za wenzetu zinaznyang’anywa kwa nguvu
Hakushinda.

Kaongo hako kajamaa.

Anyways siasa zina mambo mengi ikiwa ni pamoja na public sympathy.

Mimi huwezi nidanganya bwana mdogo maana huwa ninafahamu mambo from the ground.
 
Bila kuwindana na hawa wapumbavu tutateseka sana
Maandazi ya MUNGU hayauzwi wakitokea mbele yangu siku hio nitakuja na kikapu changu kimejaa maandazi Mafwele atasimulia gari lake lilichofanywa na maandazi ya MUNGU
 
Acha upuuzi wako hapa huyo Mama shetani kabisa alafu umemuweka kwenye Avatar kabisa na huenda na wewe leo ulikuwa kanisan huku kwenye Avatar yako umemuweka shetani wa kike
Nyie vijana wa JF mambo leo muwe na adabu japo kidogo,tunamfahamu zitto junior kwa muda mrefu humu jukwaani na misimamo yake kuhusu haki,unapata wapi ujasiri wa kumkosea heshima namna hii?
 
Back
Top Bottom