Zitto usipoacha uzushi Karma itakucharaza kama inavyowacharaza CHADEMA

Zitto usipoacha uzushi Karma itakucharaza kama inavyowacharaza CHADEMA

Salamu,

Nimesoma alichoandika jana usiku Zitto Kabwe kwa lugha mbili; Kiswahili kuwafikishia ujumbe nyumbu wenzake na Kiingereza kuwafikishia ujumbe mabwana zake nje ya nchi anaoamini watamsaidia kuingia Ikulu kutimiza dhamira hake ya kuliangamiza Taifa la Tanzania. Kashindwa kabla hajaanza.

Kama kawaida WAMBEA na wanamkakati wenzake wote wakadakia uzushi wa kutekwa kwa Prof Assad. Kigogo akapost kama alivyopost Zitto utadhani wako nyumba moja na wanatumia laptop moja.Maria Sarungi akapost na wapambe wao kama akina Aidan Eyakuze wakalike.

Post hizo zikatumwa kwa Mabalozi. Punde Prof Assad mwenyewe amekanusha na baadhi ya hawa wazandiki macho yamewatoka na baadhi wamefuta post.

Sikilizeni, hawa hawajakosea. Ni mkakati waliofundishwa na waliopewa kwa ulaghai wa Kisultan Mangungo kuwa watasaidiwa kuingia Ikulu siku zijazo!! Pumbavu hawa. Tanzania ilipofika itachagua wazalendo na sio wauza lindi kama Zitto Kabwe.

Zitto Kabwe ni bahati mbaya sana ametoka kuwa kijana aliyetamani kuingia Ikulu kwa hoja sasa amekuwa wakala wa mabeberu anayetaka kuingia Ikulu kwa vioja vya kuwa wakala wa kulinda maslahi ya watu wa nje. Ashakwama. Watanzania wameona raha ya kuwa na viongozi wazalendo; sasa nchi inakwenda.

Endeleeni kuwaangalia, watazusha mengi mwisho huu wa mwaka na watatunga uongo mwingi, wakiamini wataiteteresha jamii, maskini we, Wako wao na nyumbu wenzao, watanzania wenye akili wako katika maisha yao, wanaendelea kufurahia amani na utulivu na wanakuka sikukuu zao kwa amani.

Zitto ameingia rasmi katika kundi la vijana wanaoangamia kwa kukosa maarifa. Maskini.

Sasa nilimsikia juzi eti anadai akamatwe yeye, nadhani anachokitaka atakipata, maana Tanzania lazima ibaki.

Pole yake sana. Aendako.Atafika tu. Soon. Si kataka mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAHAHA.PNG

ASSAD kakanusha kama unaamini ile ya ASSAD ni kweli basi na hii ya meko ni ya ukweli shida si muone ki tick hicho?
 
maramla,
Nadhani ni sawa tuu sababu hata nyinyiemu m'mebaki madarakani kwa vioja, sasa na wapinzani wakitumia njia ya kihuni kuingia magogoni msipige kelele kama vile imeingia sana, shubaamiti...
 
Hofu ya nini sasa! Kama ni taarifa ya uzushi si muikanushe kupitia msemaji wa serikali au vyombo vyenu rasmi! na wakati huo huo mkitolea na ufafanuzi wa taharuki inayoletwa na watu wasiojulika!

Yaani tayari mnamugopa Zitto Kabwe kama ilivyo kwa Membe! Kwani hiyo Ikulu mtaishi milele! Si itafikia wakati mtawaachia na wengine kama ilivyotokea kwa watangulizi wenu!
 
assad kakanusha kama msemaji wa mzee meko alivyokanusha,kama mnakubali ile tweet ni ya assad basi na hii ni ya meko sababu zote zina verified tick
HAHAHA.PNG
 
Kutamani kuingia ikulu sio dhambi,ndo siasa hizo,hata Kama zito anatamani kuingia ikulu,haina maana kuwa atamshinda jpm ,Mimi sioni tatizo la mtu kutamani kuwa rais .
Ama kuhusu suala la Assad,dunia ya Sasa la hii mitandao huwezi kukwepa uvumi,maana anaweza anzisha mtu yeyote na kabla haujawa verified ukasambaa ,hii ipo dunia yote kwasasa,labda Cha kufanya tuzime internet
 
Wasijulikana ni waki na nani?

Sasa kama wanaoteka watu ni kama majambazi na hakuna anaewajua ,nani amkamate Zitto?
Unataka kutuaminisha kuwa lengo la Zitto ni kuwachafua watu wasiojulikana? Kwahiyo wasiojulikana wamesingiziwa?

Kwahiyo wewe hao wasiojulikana unawafahamu hata uje hapa jukwaani kuwatetea? Wamekutuma? Au wewe unamaslahi nao hao watekaji?

Zitto katimiza wajibu wake,mmezima Bunge,Vyombo vya habari kwa sasa vimekuwa dhaifu,wanaotusaidi na kututetea ni aki na Zitto.

Siku hizi ukitekwa au kunyakuliwa inabidi Zitto ajulishwe kabla hujafungwa kwenye kiroba na kutupwa Baharini
 
Aisee.... na wewe ni mmojawapo wa wasiojulikana.?? Maana conclusion yako inaashiria hilo..
 
Assad alitekwa na baada ya kelele za raiya wakamuachia.

Unataka Zitto akamatwe kwa kosa gani labda kwa mfano????

Sent using Jamii Forums mobile app

Huyo Assad alitekwa na nani???!!! Na huyo Zitto aliposema Rais wetu ni ahututi alikuwa sahihi???!!! Mimi binafsi naamini wapo watanzania wanaotumiwa vibaya na baadhi ya nchi za nje katika kuihujumu Tanzania...ipo video moja ambapo Uhuru Kenyatta Rais wa Kenya anatumia maneno makali mno kwa watu wa aina hii....
 
Chadema walimvua uanachama kwasababu kulikuwa na connection za siri chadema kuvuja , kwenye harakati za chadema hakuwahi kuwa mstari wa mbele , viongozi wa chadema wa ngazi za juu walipitia dhoruba nyingi ila yeye hajawahi kuguswa.

Huyu jamaa ana mission maalum ndo maana hata sasa hakamatwi ingawa anawaaminisha watu kuwa yupo sahihi ila ni mtu wa mission zake na watu wa upande wa pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taja missions zake tatu takatifu na sisi tufahamu
 
don-oba,

Ndugu yangu kunyamazisha watu hakuna anae weza kabisa na likifanikiwa hilo litatengeneza hatari kubwa zaidi kwa wale wanaodhani wanaweza kunyamazisha.

Mwenyezi Mungu na ukuu wake wote ameruhusu viumbe vyake kumuuliza na pia wapo wanao mtilia shaka zaidi wengine wanasema hayupo lakini bado ameendelea kuwapa stahiki sawa, mbua,maji,jua na ulinzi.

Huwezi lazimisha mtu akupende lakini pia huwezi lazimisha mtu akusifie.
Do your part
 
Back
Top Bottom