Zumaridi aviponza Vyombo vya Habari. TCRA yatoa onyo na kuvitaka kusimamia misingi ya utoaji habari

Embu tuambie wewe mbinguni papoje?

Una uthibitisho Gani kwamba aliyoyaongea huyo Zumaridi ni ya kweli au ya uongo?

Mbona mnadanganywa na kina mwamposa joe Davy gwajima kwamba wanafufua wafu kuponya magonjwa Kwa maji ya upako Kuna anayewazuieni kuamini hayo?

Why kumwandama huyo mama kwani kavunja Sheria ipi ya nchi hii?

Au Kwa kuwa anaongea msiyopenda kuyasikia? Kila mtu aheshimu Imani ya mwenzake
 
Mwambie Millard Ayo na timu yake aache kukurupuka kuhangaika kutafuta content ambazo hazina maana kwenye kwasababu ya kutafuta hela za laana... pesa za aibu zinafedhehesha...
Pesa za laana Kwa mujibu wa Sheria ipi ya nchi hii? Au mnafikiri Tanzania ni nchi ya kidini?
 
Yaani abaki chini ya uangalizi kafanya kisa Gani?
 
Kama ni hivyo Imani zote zipigwe marufuku la sivyo ni kumuonea tu huyo mama maana hata Imani yako wewe Kuna wanaoona ni ya kijinga kama wewe unavyoona za wenzako ni za kiwenda wazimu
 
Mambo ya kiimani tuyaache kama yalivyo
Mfano wakristo wanaamini kuwa Yesu ni Mungu na alisulubishwa msalabani, Kwa hiyo wazuiwe au wakamatwe Kwa kuwa waislamu hawaamini hivyo? Kila mtu aamini anachoamini, maana mjuzi wa yote ni Mungu
 
Chizi Kwa kuwa anaongea msiyopenda kuyasikia au?

Yule mnayesema alipaa kwenda mbinguni mna uhakika Gani kama alipaa? Au mna uhakika Gani kwamba alisulubiwa na akafufuka? Maana hata hayo ni mambo yasiyokuwa na uthibitisho ila yanahubiriwa kila siku na hakuna anayekuzuia mwacheni mama wa watu ahubiri anachoamini yeye
 
hawa TCRA hawajitambui, hasa huy waziri anayeoongoza wizara hii.

Nchi ina ujinga sana hii
 
Simkubali Zumarid lakini serikali kuingilia sio sawa. Mambo ya imani na mbiguni ni mambo ya kufikirika. Sio tangible
Serkali kuingilia mambo ya ZumAridi ni makosa na inatakiwa ijue kuwa serkali haina dini. Zumaridi anahubiri yanayofuatwa na waumini wake. Hao waumini wanaamini na wana imani na uhalisia wa mahubiri ya Zumaridi, kama Wakristu au Waislamu walivyo na imani ya mahubiri ya wahubiri wao.

Wafuasi wa dhehebu ndiyo wanajuwa ukweli. Serkali haijui wala haitakiwi kujuwa dhehebu lipi ni la kweli na linahubiri ukweli kwa sababu siyo kazi yake. Kwa TCRA kuanza kuwasema wafuasi wa Zumaridi tayari umechukuwa upande. Sasa sijui itachukuwa upande upi, wa wakristu au wailslamu, wa shia au sunni, wa katoliki au anglikana. Unaonaje ikichukuwa upande wa dini asilia.

Serkali mpaka sasa inashindwa kuleta maji safi kwa wananchi, dawa hazippo za kutosha, mabwana shamba wamesambazwa vijijini lakini hawafani kazi. Ng'ombe wanakufa ovyo kwa kukosa majosho ambayo yangepunguza magonjwa. Vijiji karibu vyote barabara zake hazipitiki. Kwa nini serkali ijishughulishe na "none issues"? Au insaogopa nguvu za imani katika uchaguzi ujao. Sasa hivi serkali imejiingiza kwenye dini na kuzivuta karibu na kuzitumia kupumbaza watu kudai haki. Naona uoga unaanza hasa kwa zilie dini zenye ufuasi mkali ambazo bado hazijakamatwa na serkali. CHADEMA iliishatiwa mfukoni na haifurukuti. Hotuba nyingi za CHADEMA hazina makombora ya wizi wa serkali tena. Hii ni sababu kwenye muafaka au makubaliano wameambiwa kuongelea hayo bila ushahidi ni marufuku, sasa wamebaki kutwanga maji kwa kinu. HONGERA MBOWE, MFUKO WAKO UMEJAA NA CHADEMA IMEHASIWA.
 
Heri nusu shali kuliko Shari Zima.

Hao wengine ni Mungu anajua ila kufuru kama ya Zumaridi lazima ipingwe .
Na ya Mwamposa je! Mbona aliitwa bungeni sijui kufanya nini huku wakijuwa kila siku anadanganya juu ya uponyaji wake. Je, Mwamposa anaweza kutoa ushahidi wowote wa alieyemponya?
 
TCRA wamekuwa influenced ?

Kila mtu anajua Yule Zumaridi mgonjwa...

Wao wanaamini zile memes?
Wanatishika na memes??
TCRA wapo sahihi na tena wamechelewa.

kwa haraka haraka zumaridi ni psychopath, hana tofauti na kibwetere. mara nyingi watu kama hawa huwa wanapata wafuasi wengi wenye akili za "kisaikopasi" kama wao.

ni sahihi kabisa kwa TCRA kuvionya vyombo vya habari hususani online media kuhusu kuwafanyia mahojiano watu aina ya zumaridi.

focus pekee ya online media za kibongo ni kupata content za kupost youtube ili kuvutia viewers bila kujari madhara yanayoweza kupatikana kwenye content hizo.

ndio maana ukitazama mahojiano mengi yanayopostiwa youtube kwa kupitia online media,ni ujinga mtupu.
 
Kama Chizi Mwamposa anapewa "airtime" kwa nini Chizi Zumaridi asipewe airtime"? Wote hao machizi tu. Pia machizi wa dini nyingine za kikristu na kiislaamu hupewa airitime, kwa nini chizi Zumaridi anyimwe?
 
Hizo "memes" zinazosambazwa ni kweli huyo Zumaridi kayanena hayo au ni watu tu wanatengeneza!!???
 
Mambo ya kiimani tuyaache kama yalivyo
Mfano wakristo wanaamini kuwa Yesu ni Mungu na alisulubishwa msalabani, Kwa hiyo wazuiwe au wakamatwe Kwa kuwa waislamu hawaamini hivyo? Kila mtu aamini anachoamini, maana mjuzi wa yote ni Mungu
Nakubaliana na wewe. Kama mtu anaamini kuwa Zumaridi ni Mungu kwa nini tumsumbue? Ana tofauti gani na wale wanaoamini jua ni Mungu au Ng'ombe anastahili kuabudiwa.

Amandla..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…