JamiiCheck - Tanzania

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

VVU/UKIMWI vinasalia kuwa janga kuu la afya ya Umma duniani, janga lililogunduliwa zaidi ya miaka 40 iliyopita likiwa limechukua uhai wa watu zaidi ya milioni 40.4 huku maambukizi yakiendelea katika nchi zote duniani. Hadi kufukia mwishoni mwa mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa watu milioni 39.0 wanaoishi na VVU, theluthi mbili kati yao (milioni 25.6) wakipatikana barani Afrika. Pia, mwaka 2022 pekee, watu 630 000 walipoteza maisha kutokana na sababu zinazohusiana na VVU na watu milioni 1.3 walipata VVU.
Nadhani wengi tumetizama movie ya Titanic, ikielezea penzi la vijana wawili na pia kuzama kwa meli hiyo. Inasemekana ina uhalisia kiasi fulani na tukio la kweli la kuzama kwa meli hiyo mwaka 1912. Jambo la kutafakarisha, imekuwa ikidaiwa kuwa aliyekuwa kapteni mkuu wa Meli hiyo Edward John Smith kabla ya kung'oa nanga alisikika akisema kuwa ''Hata Mungu Mwenyewe asingeweza kuzamisha hii meli'' - ( "Even God himself couldn't sink this ship") Kauli hiyo inayodaiwa kutamkwa na Kapteni wa TITANIC, imetafsiriwa na wengi kama chukizo kubwa kwa Mwenyezi Mungu hivyo kupelekea kuwaadhibu maelfu ya watu waliokuwa kwenye meli hiyo. Edward John Smith Meli ya Titanic
Hii dunia ina vitu vya ajabu sana na vya kushangaza. Kuna historia baadhi unaweza unaweza kushangazwa nazo mojawapo ikiwa hii niliyopata kusimuliwa. Msitu wa Nyumbanitu una historia nyingi za kushangaza. Msitu huu upo katika Wilaya ya Wanging'ombe mkoa wa Njombe. Msitu huu nimepata kusimuliwa kuwa endapo mwanamke atakuwa kwenye siku zake basi hatoruhusiwa kuingia katika msitu huo, Ikiwa atakaidi basi akiingia kwenye huo msitu ndio utakuwa mwisho wake wa kuonekana maana atapotea mazima. Nadhani hili jambo mnaona linavyostaajibisha. Najiuliza huu msitu una nguvu na miujiza gani mpaka uweze kuwatendea hivyo dada zetu.
Kevin Carter alikuwa ni mpiga picha, sasa katika kazi zake alifanikiwa kufika Sudan na alikuta eneo fulani nchini Sudan likikabiliwa na njaa kali sana. Wakati anaendelea kuchukua matukio katika picha, alikutana na mtoto dhoofu mwenye utapiamlo aliyekuwa akikabiliwa na njaa kali pamoja na kiu, cha kusikitisha zaidi nyuma ya mtoto huyo dhoofu kulikuwa na ndege hatari aina ya TAI akimuwinda huyo mtoto ili kujipatia kitoweo. Inadaiwa Kevin Carter alipiga picha na kusepa. Inasemekana huko nyuma mtoto yule kutokana na kuwa dhoofu aliweza kuuawa kirahisi na TAI yule. Inasemekana picha ile ya Kevin Carter ilipata umaarufu sana mpaka kupata tuzo ya Pulitzer iliyoanzishwa na Joseph Pulitzer. Inadaiwa Kevin Carter umaarufu aliopata...
Miaka kadhaa nyuma niliwahi kusikia mwanamke mmoja nchini Uganda kajifungua watoto wawili (mapacha) wenye baba tofauti, hali hii ilinishangaza sana. Hali kama hii iliripotiwa pia Septemba 9, 2022 kwenye jarida la CNBC ambapo mwanamama mmoja kutoka Minerois, Brazil alithibitika kuwa na ujauzito wa mapacha ambao baada ya kupimwa DNA zao ilibainika kuwa walikuwa wa baba tofauti. Kisayansi, ni kweli kuwa jambo hili linaweza kutokea? Kama jibu ni ndio, linatokeaje?
Kijana wa miaka 29 aliushangaza ulimwengu kwa kitendo cha kikatili kisichokuwa na chembe ya utu. Inadaiwa baada ya kumpindua na kumuua Rais aliyekuwa madarakani William Tolbert, Samuel Doe alihakikisha anamaliza mizizi ya mtangulizi wake kwa kuua viongozi wote waandamizi. Inadaiwa Aprili 22, 1980 viongozi 13 walifikishwa ufukweni mwa bahari ya Atlantic nchini humo, wanaume hao 13 walikuwa nusu uchi ambapo walifyatuliwa risasi na vikosi vya Rais Samuel Doe. Kati ya waliouawa ni pamoja na Frank E. Tolbert ambaye alikuwa Kaka yake na rais Tolbert, na Rais wa Bunge la seneti. Picha: hali ilivyokuwa siku ya mauaji Muosha huoshwa, Rais Samuel Doe naye alikuja kupinduliwa na kuuawa kikatili sana na waasi.
Salaam ndugu zangu, Nimepata taarifa kwamba Shirikisho la soka nchini Zanzibari limeweka ugumu kwa wachezaji wa Tanzania Bara na itawasajili kama Wageni. Taarifa hii imeandikwa: Bodi inayosimamia Ligi kuu ya Zanzibar (PBZ) imepitisha kanuni mpya za Usajili kuwa Klabu yoyote itakayomsaini mchezaji kutoka Tanzania bara ataingizwa kwenye system kama Mchezaji wa kigeni kwa maana lazima akatiwe Kibali cha kuishi Zanzibar ambacho kina gharimu pesa za kitanzania laki 5. Pia kwenye klabu Moja hawatakiwi kuzidi wachezaji 9 Kwa ligi ngazi ya Mkoa Mchezaji kutoka Tanzania bara atakatiwa kibali cha kuishi na kufanya kazi kwa msimu. Mmoja ambacho kita gharimu Pesa za kitanzania Laki 3. Kwa upande wa Tanzania Bara, mchezaji akisajiliwa kutoka...
Covid-19 ni janga ambalo lilitikisa ulimwengu kuanzia mwaka 2019. Virusi vya korona ni jamii kubwa ya virusi vinavyojulikana kusababisha magonjwa yanayoanzia homa ya kawaida hadi homa kali kama vile Homa Kali ya Upumuaji ya Mashariki ya Kati (MERS) na Homa Kali ya Mfumo wa Upumuaji (SARS). Virusi hivyo kwa mara ya kwanza viligunduliwa 2019 huko Wuhan, China. Uzi huu utapitia baadhi ya nadharia zilizoibuka wakati huo pamoja na fafanuzi za kitalamu za nadharia hizo.
Salaam Ndugu zangu, katik pitapita zangu mitandaoni hasahasa kwenye mjadala unaomuhusu Dkt Slaa nimekuwa nikikutana na clip fupi ya Sekunde zipatazo 15 ikimuonesha anatamka kuhusu kupindua Serikali. Kwa namna Clip hiyo ilivyokatwa nashindwa kuelewa muktadha wa kauli hiyo. Naombeni mtusaidie kutafuta ukweli wa tukio hilo au Interview hiyo kwa kirefu zaidi. Clip niliyokutana nayo na inayosambaa ni hii hapa chini: Picha: Dkt Slaa Video 1: Kipande (clip) inachosambaa kwenye mitandao ya kijamii Video 2: Sehemu ya kipande cha Dkt. Slaa kwa urefu zaidi Chanzo: Star TV
Kuna tafiti za hivi karibuni zimethibitisha kwamba hata wanaume hupata hedhi, ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika. Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi, mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana. Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana silaha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli Nitoe wito kwa serikali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya. USSR
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…