Jeshi la Polisi nchini Kenya limesema tuhuma za kutekwa kwa Twaha Mwaipaya, raia wa Tanzania na mwanaharakati, zinahitaji uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
Katika taarifa iliyotolewa Nairobi, Oktoba 27, 2026, polisi wamesema taarifa za awali zinaonesha kuwa Mwaipaya aliripotiwa kuwa katika makazi ya Hilda Newton, huku wakisisitiza kuwa mazingira ya uwepo wake eneo hilo na matukio yaliyotangulia madai ya kutekwa yanahitaji kuchunguzwa kwa umakini.
Soma Pia: Twaha Mwaipaya atekwa na watu 'wasiojulikana' jijini Nairobi, Kenya
Jeshi hilo limeonya dhidi ya kusambaza taarifa za uongo, kuhariri maudhui ya kidijitali kwa nia ya kupotosha au kueneza madai ambayo hayajathibitishwa, likisema hatua hizo zinaweza kusababisha...