JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Kumekuwepo na video ambayo imechapishwa na kusambazwa na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii wakidai kuwa inaonesha madhara yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililoikumba Venezuela, ambalo linadaiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 1,450 pamoja na uharibifu mkubwa wa makazi, miundombinu na mali mbalimbali. Katika kufuatilia uhalisia wa madai hayo kwa kutumia nyenzo za kidijitali, ikiwemo utafutaji wa picha kwa kutumia mbinu ya reverse image search, imebainika kuwa video hiyo si ya tukio linalodaiwa kutokea nchini Venezuela. Ufuatiliaji kupitia chombo cha khabari cha ihalas news agency umebainisha kuwa video hiyo ilirekodiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Uturuki mwezi Februari...
Kumekuwepo na graphic inayosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikidai kuwa kuwa na maneno yafuatayo "Kwa nini CHADEMA imemuua dereva wa Heche?" Katika kufuatilia ju ya kile ambacho kimechapishwa imebanika kuwa graphic hiyo inapotosha umma kwa kutoa hitimisho lisiloungwa mkono na ushahidi kuhusu kifo cha aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Suezi Dani Maradufu, ambaye alifariki akiwa katika nyumba ya kulala wageni mkoani Kigoma. Aidha, ufuatiliaji umeonyesha kuwa graphic hiyo imetengenezwa kwa kutumia nembo na muundo unaofanana na wa Jambo TV. Hata hivyo, chombo hicho kwa sasa kimefungiwa kufanya shughuli za utangazaji na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) hivyo taarifa hiyo kubanika kuwa ni potofu Sambamba...
Kumekuwepo Picha inayosambazwa kwenye mitandao ya Facebook, Instagram na X (zamani Twitter) kumuonesha mwanaume wa Zimbabwe aliyekwenda Afrika Kusini mwaka 2009 na kurejea nyumbani baada ya miaka 16 kufuatia mashambulizi dhidi ya wahamiaji (xenophobic attacks), ambapo amekuta nyumba ya familia ikiwa imeharibika na wazazi wake wakiwa wamefariki. Katika kufuatilia zaidi kuhusu picha hiyo kwa kutumia nyenzo za kigijital imebanika kuwa Hakuna taarifa kutoka vyombo vya habari vya kuaminika au rekodi zinazothibitisha tukio hilo au kumtambulisha mtu huyo. Sambamba na hivyo kumeendelea kuwepo na picha nyingi zenye mfanano na hiyo zikichapishwa hapa, hapa, hapa, hapa Ingawa kumekuwa na visa vya wahamiaji wa Zimbabwe kurejea nyumbani kutokana...
kumekuwepo na dai kuwa Salim Ahmed Salim ni Mtanzania pekee aliyekuwa anaandikiana Barua na Marais wa USA. Yeye na George Bush Senior walikuwa marafiki. Kwenye barua hii Utaona Bush akiwa Makamu wa Rais anamwambia Salim kama kuna kitu chochote anachotaka awasaidie watoto wa Salim wanaosoma USA amuambie. Sambamaba na hilo katika moja ya machapisho mengine yanadai kuwa George Bush anamuambia Salim Ahmed Salim “ My mind races back to our UN days and I value our friendship that started back then”.
Wakuu hii taarfa inasambaa sana kupitita mitandao ya kijamii uhalisia wake ni upi? Just 6 days before the World Cup kickoff, N’Golo Kanté’s French wife announced she was filing for divorce, believing that under French law their assets would be split 50/50 regardless of the circumstances. However, during the court proceedings, it was later revealed that Kanté had no assets in France, while his properties and wealth in his home country were registered in the names of his twin children. As it stands, Kanté is now the one entitled to receive a share of her assets. After hearing the outcome, she immediately wanted to call off the divorce, but the verdict had already been passed
Back
Top Bottom