Usikae ukawaamini waAfrica katika maamuzi yeyote yale, suala la DRC linahitaji akili nyingi kuliendea na sio miguvu, tukienda vibaya pale Goma Ile vita inaweza kusambaa sehemu kubwa EA.
M23 na Rwanda wanahitaji kuhusishwa Sana kwenye kila mazungumzo ya kutatua huu mgogoro, vinginevyo ni kuiingiza kanda yote hii kwenye crisis ambayo hatuwezi kuwa na majibu nayo zaidi ya kwenda tena kwa mabeberu.
DRC ni eneo ambalo lina umafia mwingi sana wa kimataifa unaohusisha WaAfrica wenyewe, Wazungu, Wachina, Wahindi nk, wapo mpaka head of states wa Africa wanaonufaia na DRC.
Unaweza ukafikiri unapigana na M23 au Rwanda ukajikuta unapigana hata na wananchi wako aka Oligarchs wanaonufaika na DRC.
Tishekedi anayelindwa abaki madarakani, Je anadeserve kubaki madarakani kwa manufaa ya WaCongo, amefanya nini Tishekedi kuhakikisha umoja mshikamano wa WaCongo wote, amefanya nini kulifanya jeshi la DRC liwe uwezo wa kulinda mipaka yake?
Amefanya nini Tishekedi kuhakikisha Congo na majirani zake wanaishi pamoja?
SADC wanakwenda DRC kumkomoa PK na M23 au wanakwenda kutatua tatizo la DRC?.
SADC, Munisco, EAC nk wapo DRC kabla ya M23 hawajafika Goma nini walifanya?.
2012, M23 wallikuwepo Goma, mazungumzo yakifanyika wakaondoka Goma, nini kilifanyika baada ya hapo kutatua tatizo?
SADC/EAC wakifika Kigali na kumtoa PK wanaweza kuzifanya Rwanda na Burundi ziwe na amani? wanaweza kurudisha amani ya kudumu DRC?