2008-2025 JWTZ imezuia mapinduzi ya kijeshi ya Jeshi la Rwanda (RPF) mara 8 ndani ya Burundi

2008-2025 JWTZ imezuia mapinduzi ya kijeshi ya Jeshi la Rwanda (RPF) mara 8 ndani ya Burundi

Watanzania tunaishi sana kwa historia.

Jeshi imara halinunui silaha, jeshi imara ni lile linalotengeneza silaha zake zenyewe.

Ukiwa unanunua silaha, tambua na wenzio wananunua silaha, mkipigana vita mtambue hiyo ni vita baina yenu na wale wanaowauzia silaha.

WaAfrica tuache unyumbu, tusome, tujifunze, tukuze vizazi bora, tupendane, tuache kuwa vibaraka.

Africa hakuna jeshi lenye nguvu, Africa kuna vibaraka tu wa nchi na magenge ya wauza silaha duniani kifupi waAfrica NI wanasesere.
Marekani, Israel, USA, Russia, China hawa wote pamaoja na kutengeneza bado wananunua silaha.
 
Inaonekana hujui mambo mengi ya ukanda huu. Uzuri kwa sasa taarifa ni nyingi fuatilia ujue ni kwa nini.

Nenda pia kasikilize hotuba ya Rais wa Burundi Ndayishimiye aliyoitoa juzi akiwa anahutubia mabalozi Bujumbura.
Burundi kwanza inatakiwa iunganishwe na Rwanda itawaliwe kutokea Kigali, umaskini ni mkubwa sana Burundi.
 
Wewe ni mwongo sana, hiyo ya Nkurunzinza yale Mapinduzi yalifeli kwa sababu ndani ya jeshi la Nkurunziza walikuwemo waliosaliti yale Mapinduzi wakawa upande wa Nkurunziza ata hakukua na dalili ya JWTZ ata 1

Nyinyi kazi yenu ni kubeba mabegi mazito mgongoni na kubeba mbwa wa vita kwenye sherehe zenu tunaona huku

Ni Ruwanda pekee kwa Afrika mashariki ndio wana jeshi bora zaidi pamoja na udogo wa nchi yao nendeni mukawachezee muone, maiti za wanajeshi wenu zinaonekana huko kila siku zikirejeshwa Tz wakila vichapo kutoka kwa M23.,
Jeshi lenu ni weak sana kwa JWTZ.
 
Burundi kwanza inatakiwa iunganishwe na Rwanda itawaliwe kutokea Kigali, umaskini ni mkubwa sana Burundi.
Unaona sasa. Hili ndilo tatizo lenu Rwanda, Hamtaweza kuitawala Burundi ikiwa JWTZ ipo na ni imara. Burundi ni jirani wa kimkakati kwa Tanzania.
 
Usikae ukawaamini waAfrica katika maamuzi yeyote yale, suala la DRC linahitaji akili nyingi kuliendea na sio miguvu, tukienda vibaya pale Goma Ile vita inaweza kusambaa sehemu kubwa EA.

M23 na Rwanda wanahitaji kuhusishwa Sana kwenye kila mazungumzo ya kutatua huu mgogoro, vinginevyo ni kuiingiza kanda yote hii kwenye crisis ambayo hatuwezi kuwa na majibu nayo zaidi ya kwenda tena kwa mabeberu.

DRC ni eneo ambalo lina umafia mwingi sana wa kimataifa unaohusisha WaAfrica wenyewe, Wazungu, Wachina, Wahindi nk, wapo mpaka head of states wa Africa wanaonufaia na DRC.
Unaweza ukafikiri unapigana na M23 au Rwanda ukajikuta unapigana hata na wananchi wako aka Oligarchs wanaonufaika na DRC.
Tishekedi anayelindwa abaki madarakani, Je anadeserve kubaki madarakani kwa manufaa ya WaCongo, amefanya nini Tishekedi kuhakikisha umoja mshikamano wa WaCongo wote, amefanya nini kulifanya jeshi la DRC liwe uwezo wa kulinda mipaka yake?
Amefanya nini Tishekedi kuhakikisha Congo na majirani zake wanaishi pamoja?

SADC wanakwenda DRC kumkomoa PK na M23 au wanakwenda kutatua tatizo la DRC?.
SADC, Munisco, EAC nk wapo DRC kabla ya M23 hawajafika Goma nini walifanya?.
2012, M23 wallikuwepo Goma, mazungumzo yakifanyika wakaondoka Goma, nini kilifanyika baada ya hapo kutatua tatizo?
SADC/EAC wakifika Kigali na kumtoa PK wanaweza kuzifanya Rwanda na Burundi ziwe na amani? wanaweza kurudisha amani ya kudumu DRC?
Acha uoga, total war is coming, mnaleta ukoloni wa kishamba this time m23 wanapotezwa kwenye historia ya dunia

Peace is a cost.
 
Unaona sasa. Hili ndilo tatizo lenu Rwanda, Hamtaweza kuitawala Burundi ikiwa JWTZ ipo na ni imara. Burundi ni jirani wa kimkakati kwa Tanzania.
Burundi ina faida au msaada gani kimkakati kwa Tanzania?
 
Unajiandikia tu km huna kichwa...
Deep states haziendeshwi hivyo duniani pote. Ukiona majaribio ya mapinduzi yanafeli basi hayo ni maandalizi ya kuingia mapinduzi kamili, ref. Syria.
Unataka kunambia JWTZ ni bora kuliko RDF?. Kwa sasa Rwanda ni nchi yenye intelejensia kali kuliko nchi yoyote Central & East Africa na mbaya zaidi imeweka watu wake katika kila serikali kwenye sekta za maamuzi... Anzia ikulu ya Samia, TISS, JWTZ, JKT, POLICE, mashirika yote muhimu yote ya umma pote huko kuna wanyarwanda kibao wamejazana.
We kuweza Rwanda na JWTZ yako?
 
Acha uoga, total war is coming, mnaleta ukoloni wa kishamba this time m23 wanapotezwa kwenye historia ya dunia

Peace is a cost.
European union, U.SA kila mwaka wanatenga bajeti ya kufadhili M23 kupitia Rwanda.
Umeandika nn sasa?
 
Kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka huu 2025, waasi wa kitusi wa Burundi likiwemo kundi la Red Tabara wamekuwa wakifadhiliwa na kupewa mafunzo na Rwanda kwa lengo la kufanya mapinduzi nchini Burundi.

Mara nane zote wamejaribu kupindua serikali ya Burundi kwa nyakati tofauti ila wamekuwa wakishindwa vibaya mno kutokana na msaada wa JWTZ kwa nchi ya Burundi.

Jaribio mojawapo ni lile la kumpindua Nkurunzinza (R.i. p) akiwa Tanzania 🇹🇿, lililofeli vibaya mno na kwa aibu.

JWTZ popote pale itakapotia mkono, RPF haiwezi kufanikiwa na haitakaa ifanikiwe.

Mgogoro wa Congo wa sasa, Rwanda ana back up ya Israel, Qatar, USA & France.

Congo kwa upande wake, wakuu wa vyombo vya ulinzi, na mawaziri wa ulinzi wa nchi zote za SADC Wanakutana kinshasha kwa ajili ya hatua za haraka za kuizuia Rwanda na njama za kumpindua Tshikedi, hawa SADC nchi nyingi zina buck up ya China na Russia.

Ikiwa Rwanda atakataa kuwithdraw jeshi lake kutoka Congo, basi uhenda vita ikafika hadi Kigali.

Mwisho, popote pale JWTZ itakapo tia nguvu, Rwanda haitakaa ifanikiwe kamwe.
Uongo huumbuliwa na facts, France ni mmoja wa maadui wakubwa wa Rwanda. Uongo huu unayabainisha yote uliyoyaandika kuwa null and void.
Screenshot_20250202-113828.jpg
Screenshot_20250202-113906.jpg
 
Marekani, Israel, USA, Russia, China hawa wote pamaoja na kutengeneza bado wananunua silaha.

Wananunua silaha ndogo ndogo, zile sophisticated zinazohitaji high tech na kwa ajili ya kuamua vita huwa wanatengeneza mwenyewe.
 
Tulia ,kamuulize Rais wako kagame.

Na Jiulize juzi ktk speech yake kwenu kwa nini alikwepa kutamka Tanzania ,akaishia kulaumu South africa.
Inawezekana ni kwasababu TZ hakuna mahala tumefanya kitu, maana rais wetu hajatoa tamko lolote lile juu ya kinachoendea Drc, sasa ulitaka aitaje Tz kwa lipi??
 
Unajiandikia tu km huna kichwa...
Deep states haziendeshwi hivyo duniani pote. Ukiona majaribio ya mapinduzi yanafeli basi hayo ni maandalizi ya kuingia mapinduzi kamili, ref. Syria.
Unataka kunambia JWTZ ni bora kuliko RDF?. Kwa sasa Rwanda ni nchi yenye intelejensia kali kuliko nchi yoyote Central & East Africa na mbaya zaidi imeweka watu wake katika kila serikali kwenye sekta za maamuzi... Anzia ikulu ya Samia, TISS, JWTZ, JKT, POLICE, mashirika yote muhimu yote ya umma pote huko kuna wanyarwanda kibao wamejazana.
We kuweza Rwanda na JWTZ yako?
RDF na Rwanda ni weak sana kwa JWTZ Tanzania.

Endelea kujifurahisha na hizo propaganda zenu.

Tanzania hatuna ukabila hata Raia halali wa Tanzania mwenye asili ya Rwanda ana haki ya kuhudumu taaisisi yeyote Tanzania.

Kwa sasa mpango uliopo ni kupitisha operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu wote ni kuwarudisha nchini kwao, mikoa itakayoanza ni Kigoma, Geita, Katavi, Kagera.

Kwahiyo sisi Tanzania hatuwezi kuwabagua Wanyarwanda ila wale ambao hawana uhalali wowote wa kuishi Tanzania watarudishwa.

Hamna ambacho Rwanda yaweza kufanya Tanzania isijue.
 
Kama Congo inataka vita iishe....iwatangaze wanyamlenge ni Wacongo. Waited waasi ikae nao chini.

Wakikataa basi nchi zingine Zitoe msaada wa Kavita. Ninaamini namna bora ya kushinda vita ni kuanza na amani kwanza.
 
Hawa watoto wa elfu 2 hawajui kitu. Huyo mwenetu tumemuonyesha njia hiyo amekulia hapa hapa na akipata shida break ya kwanza ni hapa ndio kwao.Madogo hawajui historia wanapotezwa na hizi PROPAGANDA ambazo tumewafunza sisi🤗🤗🤗
Kagame kakulia Uganda, japo sawa ame train hapa, ila ni mwenyeji wa Uganda
 
Back
Top Bottom