Hakuna hela ndogo, chukua hiyo kazi nakupa akili hapa.
Kama huna kazi nyingine, chukua hiyo kazi haraka, ukipata tu nakupa akili, kopa haraka, uwe unakatwa mkopo kama laki 250,000 hv, kwa miaka 7, roughly utapata 18 au 20 Mil.
Hiyo 18 au 20 Mil, gawa mil 15, hiyo mil 15 zamisha kwenye biashara unayojua vizuri ndogo ndogo kama 3 hv za mil 5 biashara moja
Mil 5 nyingine na mil 5 biashara nyingine, kila jioni unazipitia..
Mfano wa biashara za 5 mil,
1: Tigopesa 1 mil, mpesa 1 mil, airtel money 1 mil za kuanzia + kodi hiyo 5 mil inatosha kuanzia sana
2: Biashara ya chakula kizuri Dar cha mtaani, supu, chapati, wali nyama, maharage, ugali nyama tafuta location yenye watu kibao, weka mtu muaminifu wapo, within 6 months utashangaa, kikubwa usimamizi, weka mtu makini na watu wapo
3: Station za kuonyesha mpira, nunua TV 2 za mil 2 hisense na DSTV decoder, na location nzuri, kiingilio 500 kwa kichwa kwa mechi, siku ya mechi 2 unaweza pata hadi laki na zaidi sehemu nzuri..
4: Biashara ya genge la mboga mboga, matunda, viazi, ndizi, nyanya, vitunguu, hii inalipa sana.. Na kuna watu wanafanya deliveries kwenye magenge unajipanga tu kwa Dar.
Hizo ni mifano tu, ila biashara ndogo ndogo zote hizo tatu huwezi anguka, na anzisha kwa wakati mmoja zote, mtu asikutishe, inawezekana.
Mil 3 au 5 iliyobakia weka bank, usiguse kabisa, ikae standby, ukibanwa kabisa unachukua kidogo ikuokoe, mfano ukiumwa, au tatizo gumu limekupata labda ghafla.
Sijamaliza, ukipata kazi sehemu nyingine say within a year or so inalipa labda take home 1 mil unahama na unahamisha bank details zako na unazidi kupanda juu..
Baada ya miaka 2 nitafute, utalipa deni lote na utaona neema duniani, hakuna hela ndogo, tatizo uwezo wa kuizalisha zaidi hiyo hela ndio tatizo na kuzalisha fedha inategemea na mazingira unayoishi na uwezo wako, kila mazingira ni tofauti na tumia akili zaidi.
Kila la kheri.