750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Haha
Kuna wale wa kujenga ni uoga wa maisha


Hivi ni kweli? Au ni mtu tu anajifariji baada ya kujijua hana pesa za kutosha [emoji1787]
Kuna jamaa nafanya nae kazi yy huwa anasema hukuja kuipendezesha dunia kwa kujenga yy kula bata tuu akizishika
 
Humu ndani kila mtu boss! Yaani laki saba iwe mkononi isikutosshe kwa mwezi? Labda uwe unaishi kama Drake

Sent from my TECNO CD7 using JamiiForums mobile app
Ukiingiza kwenye anasa ni pesa kidogo sana iyo,pesa ni matumizi yako tu hakuna pesa nyingi isioisha kwenye matumizi

Mimi nmewahi kutumia 17M ndani ya masaa 3 tu,Ingia Hardware uone
 
Mkuu humu kuna mafogo hatari.

Uzuri wa humu muosha magari anamtukana boss wake, muuza vitunguu sokoni anavimba kuwa anafanya kazi UN Geneva.

Uamuzi ni wako uwe nani humu.

#fakeituntillyoumakeit#
Hakika umenena!
 
Hakuna hela ndogo, chukua hiyo kazi nakupa akili hapa.

Kama huna kazi nyingine, chukua hiyo kazi haraka, ukipata tu nakupa akili, kopa haraka, uwe unakatwa mkopo kama laki 250,000 hv, kwa miaka 7, roughly utapata 18 au 20 Mil.

Hiyo 18 au 20 Mil, gawa mil 15, hiyo mil 15 zamisha kwenye biashara unayojua vizuri ndogo ndogo kama 3 hv za mil 5 biashara moja
Mil 5 nyingine na mil 5 biashara nyingine, kila jioni unazipitia..

Mfano wa biashara za 5 mil,
1: Tigopesa 1 mil, mpesa 1 mil, airtel money 1 mil za kuanzia + kodi hiyo 5 mil inatosha kuanzia sana
2: Biashara ya chakula kizuri Dar cha mtaani, supu, chapati, wali nyama, maharage, ugali nyama tafuta location yenye watu kibao, weka mtu muaminifu wapo, within 6 months utashangaa, kikubwa usimamizi, weka mtu makini na watu wapo
3: Station za kuonyesha mpira, nunua TV 2 za mil 2 hisense na DSTV decoder, na location nzuri, kiingilio 500 kwa kichwa kwa mechi, siku ya mechi 2 unaweza pata hadi laki na zaidi sehemu nzuri..

4: Biashara ya genge la mboga mboga, matunda, viazi, ndizi, nyanya, vitunguu, hii inalipa sana.. Na kuna watu wanafanya deliveries kwenye magenge unajipanga tu kwa Dar.

Hizo ni mifano tu, ila biashara ndogo ndogo zote hizo tatu huwezi anguka, na anzisha kwa wakati mmoja zote, mtu asikutishe, inawezekana.

Mil 3 au 5 iliyobakia weka bank, usiguse kabisa, ikae standby, ukibanwa kabisa unachukua kidogo ikuokoe, mfano ukiumwa, au tatizo gumu limekupata labda ghafla.

Sijamaliza, ukipata kazi sehemu nyingine say within a year or so inalipa labda take home 1 mil unahama na unahamisha bank details zako na unazidi kupanda juu..

Baada ya miaka 2 nitafute, utalipa deni lote na utaona neema duniani, hakuna hela ndogo, tatizo uwezo wa kuizalisha zaidi hiyo hela ndio tatizo na kuzalisha fedha inategemea na mazingira unayoishi na uwezo wako, kila mazingira ni tofauti na tumia akili zaidi.

Kila la kheri.
 
Kweli siku hizi mwanza maisha yanakuwa expensive sana, kuanzia nyumba za kupanga bei kubwa kama za Dar tuu ingawa wenye nyumba wanajenga nyumba nzuri sana, misosi bei kubwa.

Maji ya kunywa yanayouzwa 600 Dar kwa mwanza ni 1000. Cha urahisi kule ni usafiri tuu
Ni Dar pekee maji huuzwa bei ndogo na ndo maana Jambo kashindwa onekana huku.
 
Kuna mengi mno ya kujifunza kwenye huu uzi ideas ni kubwa kwelikweli
 
Ukiingiza kwenye anasa ni pesa kidogo sana iyo,pesa ni matumizi yako tu hakuna pesa nyingi isioisha kwenye matumizi

Mimi nmewahi kutumia 17M ndani ya masaa 3 tu,Ingia Hardware uone
Jamii forum jaman kama hadithi kumbe ndio maisha yenyewe
 
Back
Top Bottom