Mshahara ni budget...ukipokea 750k kwa mwezi matumizi yako hayatakiwi yapindukie 15000 kwa siku. Utafanyaje ili ukutoshe? Hakikisha kwanza unaweka shehena ya nafaka ndani, nunua unga kg 10, mchele kg 10 ,ngano kg 10, sukari kg 5, maharage kg 7-10 na mafuta ya kupikia atleast 5litre na gesi inategemea na ujazo ila ule mtungi wa elfu 55-60 unakutosha kumaliza mwezi-miezi miwili.
Mbogamboga jitahidi uwe unapitia sokoni kununua maana kuna unafuu kiasi, ukipata sado zako mbili za viazi, Dagaa kg 2-3, vitunguu kg 2-3, viazi vitamu au ndizi mbichi. Hapa bajeti ya kula mwezi mzima humalizi laki na 20 ikiwa una familia ya mke na watoto 2-3.
Jitahidi kukaa maeneo ambayo ni karibu na kazi! Sio unafanya kazi posta halafu unaishi mpiji magoe ndani ndani huko...nauli tu kwa siku unamaliza zaidi ya 6,000. Ishi sehemu ambayo utatumia gharama ndogo ya sh 500 kwenda na 500 kurudi. Epukana na kupenda sana kutumia bodaboda kwani zinacost. Usiishi maisha ya kujinyima sana kwa wiki jitahidi ule hats nyama mara 2. Epukana na anasa za ulevi wa pombe,kamari na wanawake. Hapo utaona jinsi utakavyosave zaidi ya 300k kila mwezi.
Kama ni bachela jitahidi sana uwe na life skills kama kujua kupika, kuosha vyombo,kufua nguo zako n.k utasave pesa nyingi sana unazoenda kuzipotezea migahawani.
Kama umepanga chumba kimoja basi jitahidi kodi isizidi 50k kama ni vyumba viwili isipindukie 100k kwa mwezi