750k(take home) ni mshahara unaweza kumfanya mtu aishi kidogo bila wasi hapa Bongo?

Mbona hiyo ni kubwa sana. Mimi nalipwa 70,000/- kwa mwezi na nina familia, maisha yanaenda.
 
Aiseee maisha kweli yanataka tafakari, yaani mimi 400,000 wiki imekwisha.
Siyo siku wiki tu ata ukitaka kwa siku itaisha na ukitaka kwa mwezi itaisha tu wewe mwenyewe jinsi unavyo panga bajeti zako ukitaka lakini nne imalizike mwezi itawezekana
 
Uko sahihi mtu asiforce kula kuku wakati uwezo wa dagaa.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu hawa-save hata mia na wanapokea kila mwezi.
Akipokea tu mshahara anaenda bar ya karibu anamwagilia moyo tu. Siku 4 tu mshahara kwisha, akili inarudi mahali pake maisha yanaendelea.
Hiyo ndio monthly routine.
Kuna mtu anasoma ujumbe huu anatabasamu tu anatamani ku-like anajisemea maisha ndio hayahaya.
Kwa shida gani ufe halafu huku nyuma watu wanagombania mali zako!
 
Gharama kivipi tena uku umesema mifugo bei rahisi na ugali wa mtama upo na viazi shida ipo wapi kuku bei rahisi ni mwendo wa kubadili mboga tu
 
Hpo inategemea na mkoa na mazingira ya kazi
Kweli,kwa morogoro,mwanza,mbeya,iringa,katavi,kahama na hata dar hiyo pesa inakusongesha vizuri kabisa,ila ukipita kwenye kimji kama cha arusha usishuke kwenye basi,usile hata mshikaki,utakuwa umeilaani hela yako,itaisha ndani ya siku nne,arusha,moshi,bagamoyo,kinondoni() hivi vi mji vina majini hela
 
Bora ukose hela ya Kula lakini usikose hela ya kuweka Akiba πŸ€—

Manake Kuna watu Wana kula hadi Akiba alafu wakikwama kwa kupata tatizo hata la shilingi 30,000 lazima wapige simu kukopa. Hii ni mbaya Sana kwa kweli
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ aloooo
Yan kwamba tunakula hadi akiba
 
Ungeniuliza mahala pengine sio humu jeifu ningekujibu 750k unaishi vizuri tu na pisi kali ungekata
Ila kwa kua umeuliza jukwaani hapa nitajibu
750k ni matumizi ya mafuta tu ya gari yangu
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…