Aache kazi private anakolipwa 1.6m au aende government atakapolipwa laki 7.6?

Wife kapata kazi serikalini huko,mshahara ni TGS D ambayo ni sawa na laki 7.6, kwa sasa anafanya kazi private sector ambako mshahara ni 1.6m gross.

Kampuni anayofanyia ina pressure za hapa na pale ila kuna a lot of incentives kama bima ya afya ya Jubilee,holidays allowance na nyingine nyingi.

So right now yuko dilemma, aache hapo private au aende government?
Jibu liko wazi private ya nchi hii siyo sehemu ya kufanya kazi. Anaweza kukaa na huo mshahara hata miaka 10 bila nyogeza wakati huyo wa laki 7.6 wakati huo atakuwa ameshaupita huo mshahara wa 1.6M. Lingine kuondolewa kazini kupo njenje. Ukifanya kazi serikalini unajisikia unaifanyia kazi nchi yako siyo kumtumikia mtu binafsi. Huyo mke wako km atajiendeleza kielimu kuna fursa nyingi sana ya kupangiwa majukumu mengine makubwa yenye maslahi makubwa zaidi.
 
Watoto wa mjini watakushauri abaki hapo hapo private eti kisa 1.6 ila anaweza kujikuta miaka kumi mshahara ndo huo huo na ndo hadi hiyo kampuni iwepo. Ila serikalini anapanda daraja, mikopo ya hapa na pale, security ndo usiseme, hata mshahara utapanda tu. Na hana pa kufukuziwa ni mwendo wa reshuffle tu.

Aende serikalini hatojutia.
Watu wa serikali na serikali yenu 😂
 
Wife kapata kazi serikalini huko,mshahara ni TGS D ambayo ni sawa na laki 7.6, kwa sasa anafanya kazi private sector ambako mshahara ni 1.6m gross.

Kampuni anayofanyia ina pressure za hapa na pale ila kuna a lot of incentives kama bima ya afya ya Jubilee,holidays allowance na nyingine nyingi.

So right now yuko dilemma, aache hapo private au aende government?

Mimi Niko serikalini
Ila nikipata ajira private inayolipa mara mbili ya mshahara na hizo incentives kama za mkeo NAONDOKA..!!

#YNWA
 
Aliomba kazi serikalini ilihali anajua anakazi hapo private sasa Mungu si athumani katimiza haja ya moyo wake, aende tuu serikalini, kama alikua anataka io 1.6M asingehangaika kufanya interviews za serikalini
 
😂😂😂 hivi ni 35/45?
35 ajira nyingi za serikali hazikuhusu, ndio maana unambiwa pambana kama unamini kwenye ajira ya kuajiriwa uingie serikalini, ukifika serikalini unanza kijichagulia wapi ufanye kazi , yaani ukifika umri flani uanza kutana na usiwe na miaka 35, private unalipwa salary kubwa unajisahau halafu umri umenda unambiwa wawekezaji wameamua kufunga mradi au kaja boss mpya na structure za mishahara mipya unambiwa kama hutaki sepa, mara uambiwe utafanya kazi 7 days of week , unajikuta duniani ulikuja kuteseka
 
Wife kapata kazi serikalini huko,mshahara ni TGS D ambayo ni sawa na laki 7.6, kwa sasa anafanya kazi private sector ambako mshahara ni 1.6m gross.

Kampuni anayofanyia ina pressure za hapa na pale ila kuna a lot of incentives kama bima ya afya ya Jubilee,holidays allowance na nyingine nyingi.

So right now yuko dilemma, aache hapo private au aende government?

Job security vs profit
 
Aliomba kazi serikalini ilihali anajua anakazi hapo private sasa Mungu si athumani katimiza haja ya moyo wake, aende tuu serikalini, kama alikua anataka io 1.6M asingehangaika kufanya interviews za serikalini
Iko hivi,serikalini kuna kitu kinaitwa data base, unafanya interview kwa ajili ya taasisi flani, ukifanikiwa kufika oral na kama ulifanya vizuri but due to limited slots unawekwa kwenye hiyo database then ikitokea nafasi ya kada yako unapewa wewe.
Kwa case ya wife, ni mhasibu by profession,alifanya interview psrs mwajiri akiwa ni Bunge la Tanzania, maslahi ya huko nadhani unayajua,so kwa kipindi kile alifanikiwa kufika oral ila hakuipata ile kazi,so hivi karibuni kuna majina yametoka na lake limo wamelichukua kutoka data base anatakiwa kurepot kwenye taasisi flani ambayo mshahara wao ni hiyo tgs D.
Umeelewa?
 
35 ajira nyingi za serikali hazikuhusu, ndio maana unambiwa pambana kama unamini kwenye ajira ya kuajiriwa uingie serikalini, ukifika serikalini unanza kijichagulia wapi ufanye kazi , yaani ukifika umri flani uanza kutana na usiwe na miaka 35, private unalipwa salary kubwa unajisahau halafu umri umenda unambiwa wawekezaji wameamua kufunga mradi au kaja boss mpya na structure za mishahara mipya unambiwa kama hutaki sepa, mara uambiwe utafanya kazi 7 days of week , unajikuta duniani ulikuja kuteseka
Huwa mnapata faida gani kuongea uongo?
 
Attachments

  • Screenshot_20230209-172943_Adobe Acrobat.jpg
    Screenshot_20230209-172943_Adobe Acrobat.jpg
    149 KB · Views: 21
Sio 45?

Saweni
Ngoja tuendelee kumchekea muhindi
ukiwa na fursa ya kupata kazi serikalini do it aisee, salary ni nini eti , mimi mwalimu wa government kwa mwaka nina likizo april siku 14, june siku 30, september siku 14, december siku 30, plus weekend zote, natoroka karibu kila siku , ninafundisha mikondo miwili , kila mkondo una vipindi vitatu per week so ni dk 40 * 3 kwa kila mkondo , halafu nipo TGTS E ,hizo pesa za private ache nipate mtaani
 
Unajisifu kutoroka aiseee 😝
 
Back
Top Bottom