Aache kazi private anakolipwa 1.6m au aende government atakapolipwa laki 7.6?

Aache kazi private anakolipwa 1.6m au aende government atakapolipwa laki 7.6?

Kama ni wife mwambie aende serikalini, KWA maana ya ishu ya security na kustaafu benefits. Hata serikali pana bima ya afya pia.
Halafu mbona hakuna tofauti Kati ya hio 7 na 1.6.
Ingekuwa labda 7 m sawa.
Mwambie awahi haraka sana serikalini
 
Serikalini napo unaweza siku moja boooom uhamisho Bukoba
Na huko huko ndipo ukatobolea.
KWA SAsa tza yote unaishi na mambo YAKO unafanyia popote tu.Maisha sio Dar tu siku ukitoka Dar ndo utaelewa nilikuwa napoteza mda.
Mikoani saving ni kubwa kuliko dar.
Kodi nafuu, vyakula nafuu,huitaji bodaboda,hakuna presha za kuchelewa job,watu wanaupendo makazini,mnaishii kama ndugu haya yote Dar hayapo.
 
That's not the point...ni changamoto ya kuanza upya na kuhamisha familia yote , then mkeo au mumeo naye aache kazi yake akufuate, swali lake kila kitu ni risk tuu na hakuna guarantee kwa atakachofikiria , chochote kinaweza kutokea
Kama familia imeweka base sehemu moja uhitaji kuhamisha familia.
Utahamisha hadi wapi,Kazi ya utumishi ni mguu pande leo Bukoba kesho Mtwara,kesho kutwa Mbeya
 
Yah ila kwa baadhi ya vitengo unajua kabisa hapa pengo langu halina spea
Hiyo kauli iondoe kabisa ukiwa kwenye eneo la kazi.

Niliwahi kufanya kazi Bank fulani yule Head of Corporate and Banking Investment alikuwa anasema hivyo

Board of directors wakakaa wakaona hajafikia malengo kilichomkuta nafasi yake ilichukuliwa na akakiri aliyechukua nafasi yake anajua

Kuna watu wanajua na kazi zao zimeonekana
 
Hiyo kauli iondoe kabisa ukiwa kwenye eneo la kazi.

Niliwahi kufanya kazi Bank fulani yule Head of Corporate and Banking Investment alikuwa anasema hivyo

Board of directors wakakaa wakaona hajafikia malengo kilichomkuta nafasi yake ilichukuliwa na akakiri aliyechukua nafasi yake anajua

Kuna watu wanajua na kazi zao zimeonekana
Anyway mimi nafanya kazi mortuary
 
Mshahara wa miezi sita huku ni wa mwaka mzima

Fanya hapo private alafu kila mwezi weka milion moja usiiguse

Kazi ikija kubuma utakuwa tayar na mtaji mnene unakuwa tayar na pakuanzia.

Kuna watu bila ajira za serikalin wanachanganyikiwa kabisa

Wanaona kama ndio kila kitu


Job security ya mavi
 
Aende serikalini tu unless yeye ndo kichwa cha familia, lasivyo mkataba ukiisha au akifukuzwa atakuwa mzigo kwako
 
Nadhani angalia stability ya hapo anapofanya kazi saizi,kama panaweza kuwepo na kuwa imara kwa miaka 5 ijayo au zaidi haina haja,ila kama ni tiatia maji..........mjadili na mkeo
 
Mhasibu akienda Serikalini anaweza vuta hata M.3 kwa mwezi.
Yaani pamoja na poshoposho.

Aende Serikarini.
Kuna security kubwa na dhamana
 
Pressure ya ku-renew contract unaijua wewe?
aah sawa ila prior ukijua mkataba unakaribia kuisha unaanza kujipanga mapema na kama unafanya kazi vizuri basi hutokua na wasiwasi sana, unajua watarenew tu , pia unajua kuna makampuni private yenye permanent contracts?
 
Wife kapata kazi serikalini huko,mshahara ni TGS D ambayo ni sawa na laki 7.6, kwa sasa anafanya kazi private sector ambako mshahara ni 1.6m gross.

Kampuni anayofanyia ina pressure za hapa na pale ila kuna a lot of incentives kama bima ya afya ya Jubilee,holidays allowance na nyingine nyingi.

So right now yuko dilemma, aache hapo private au aende government?
1. Hawezi kuanzisha mradi na kuusimamia akiwa private tofauti na serikarini.

2. Serikalini atapata mkataba wa kudumu tofauti na private.

3. Serikalini mshahara ni kianzio wakati private ni kikomo

4. Serikalini anaweza kwenda kuongeza shule kwa kulipiwa tofauti na private ambapo hawezi ruhusiwa kwenda shule.

5. Serikalini anaweza kuomba likizo ya bila malipo ili akafanye mambo yake then anarudi tofauti na private.

6. Serikarini atalipwa mshahara wake kila mwezi hata kama Covid 23 iko inakuja tofauti na private ambapo mshahara unaweza sitishwa at any time.

Ninachoona ni kwamba BAADAYE ATAKUJA KUJUTA.

Naomba niishie hapo kwa leo.

Zingatia KUPANGA NI KUCHAGUA.
 
Back
Top Bottom