Acheni kumlaumu Rais Samia. Mafuta yamepanda bei katika soko la Dunia, ulizeni bei za mafuta Kenya, Uganda, Rwanda zipoje

Acheni kumlaumu Rais Samia. Mafuta yamepanda bei katika soko la Dunia, ulizeni bei za mafuta Kenya, Uganda, Rwanda zipoje

Nitajie nchi ambayo haitozi kodi katika bidhaa za mafuta.Nchi itajiendeshaje kama haikusanyi kodi? Mnataka kuja tena kumlaumu kuwa hospitalini hakuna madawa, wafanyakazi kutolipwa mishahara kwa wakati n.k
Inaonekana hata huelewi kitu juu ya mchakato wa uingizaji mafuta ulivyo na tozo kibao, kwa taarifa yako kuna tozo kama 19, sasa unapouliza eti kuna nchi gani haitozi kodi, kwenye mafuta ni ajabu.Inshu sio kuacha kutoza kodi bali ni kuondoa baadhi ya tozo ili kupunguza gharama ya mafuta!!
Mfano, kwenye mbolea Tz, mfuko mmoja uko kwenye 125, 000 lakini malawi mbolea hiyo hiyo inauzwa tsh.70, 000 na zote tuliambiwa kutokana na covid , kwenye soko la dunia imepanda sana!!wao wanapunguza tozo , na wakati mwingine wana weka ruzuku, ili kumsaidia mwananchi, lakini hapa kwetu wao ni siasa tu, wakisema ni bei imepanda kwenye soko la dunia wamemaliza!!!
 
Kwa hiyo? Zanzibar wameweka Kodi kama Bongo? Nani kakwambia mafuta ni jambo la Muungano?
Kwahiyo unakubali kuwa bei ya mafuta Zenji ni sh 2,600? Kama ndio, Znz wanachimba mafuta yao? Au wao hilo soko la Dunia haliwaathiri?

Na kwa kutumia mfano wa mama, bei ya lita moja huko USA ni sawa na huku? Utasingizia usafirishaji kana kwamba USA ndo nchi inayotoa mafuta. Vipi kuhusu bei ya mafuta kabla ya vita, ukilinganisha na nchi zote zilizotuzunguka, ilikuwaje? Kwanini?
 
Ahlan wa Sahlan

Habari zenu wana JF:

Kumekuwa na tabia ya upotoshaji inayoendelea hapa nchini kwa watu kumlaumu rais kwa hali ya kupanda kwa gharama za maisha inavyoendelea kila kukicha, kubwa ni hili la kupanda kwa gharama za mafuta ya petroleum, diesel na mafuta ya taa.

Bei ya mafuta kwa nchi zisizozalisha mafuta zimepanda kwa kiasi kikubwa duniani kote. Pigieni simu watu wa Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kampala , Lusaka, Kigali n.k muwaulize bei za mafuta zipoje.

Tembeleeni hii tovuti mjionee bei za mafuta duniani.

Zanzibar wao wananunua kutoka sayari gani?
 
Ni kweli bei imepanda duniani kote,,lakini serikali inafanya nini ili kudhibiti hiyo hali isiathiri sana maisha ya watu? kwa nini wasipunguze kodi na tozo kwenye mafuta ili kupunguza makali ya bei.? nini maana ya Rais kama hawezi kupambana na changamoto zinapojitokeza?
Zanzibar wao wananunua kutoka wapi?
 
Ndio maana nakwambia una akili ndogo afadhari na funza,unaweza Kuta na wewe ni msomi unauliza Kodi inaenda wapi [emoji1][emoji1]..

Nilitaka nisikujibu kwa sababu ntakuwa najichosha kujadiliana na mtu mwenye akili ndogo kiasi hiki..

Nchi zisizo na tozo,unajua uwezo wa kiuchumi wa hizo Nchi? Zinahudumia raia kiasi gani?

Yaani unauliza Kodi na mirahaba inakwenda wapi? Hapa sikujibu kwa sababu wewe ni mjinga,go find for yourself.

Royal tour unayoisemea ni nyenzo mojawapo ya kutafuta pesa Ili mke wako wewe mvivu akatibiwe,bil.9 hata mafuta ya nusu mwezi haitoshi.

Hujawahi msikia akikwambia anakopa kwa ajili ya miradi? Unapouliza inakwenda wapi wewe unaishi shimono?

Stupid monkey sikujibu tena upuuzi wako
Bunge limesitisha ratiba yake ili kupisha hoja ya dharula kupinga ongezeko la bei ya mafuta.

Je wabunge nao ni stupid Monkeys [emoji205] kama mimi?

Je wabunge nao ni akili za visoda?

Acha kuwa ukijiona mjuaji kwenye masuala kama haya ya kitaifa na yanayoigusa jamii kwa upana zaidi.

Wewe unaonekana kuwa mlala bure na familia ya walamba asali.
 
Ni porojo tuu huko Bungeni kwa sababu serikali itasema itakuja na majibu wakati wa kujadili bajeti ya Nishati wala hakuna jipya hapo.
 
Ni kweli bei imepanda duniani kote,,lakini serikali inafanya nini ili kudhibiti hiyo hali isiathiri sana maisha ya watu? kwa nini wasipunguze kodi na tozo kwenye mafuta ili kupunguza makali ya bei.? nini maana ya Rais kama hawezi kupambana na changamoto zinapojitokeza?
Na tatizo kubwa katika Nchi hii ni kwamba kila inapopanda bei ya nishati yeyote ile iwe ni umeme au mafuta basi hapo huwa ni neema kwa wafanyabiashara !! Kwa kupandisha bei za bidhaa kiholela kwa sababu huwa hakuna udhibiti katika kusimamia bei za bidhaa !! Wanasema ni soko huria, na kibaya zaidi ni kwamba hata hapo baadaye bei za nishati zikishuka bado zile bei zilizopanda kwa sababu ya kupanda bei ya nishati zitabaki huko huko juu na kuendelea kupandaZaidi na zaidi ! Hapo sasa ndipo Serikali inapolaumiwa kwa kushindwa kuwadhibiti wafanyabiashara wanaojipandishia bei za bidhaa kiholela !
 
Kwahiyo unakubali kuwa bei ya mafuta Zenji ni sh 2,600? Kama ndio, Znz wanachimba mafuta yao? Au wao hilo soko la Dunia haliwaathiri?

Na kwa kutumia mfano wa mama, bei ya lita moja huko USA ni sawa na huku? Utasingizia usafirishaji kana kwamba USA ndo nchi inayotoa mafuta. Vipi kuhusu bei ya mafuta kabla ya vita, ukilinganisha na nchi zote zilizotuzunguka, ilikuwaje? Kwanini?
Tzn time enjoy bei nafuu ya mafuta kuliko Nchi zote zinazotuzunguka except Zambia,kwa sasa hata huko Zambia bei hazikamatiki na hawana Kodi zozote..

Kuhusu Zanzibar,sio tuu mafuta ni nafuu lakini takribani vitu vyote kule ni nafuu kuliko Bara miaka yote hata kabla hujazaliwa wewe,huo unafuu haujaanza leo wala Jana..

Ni sawa ndio Kwa sababu mafuta yamepanda kote .
 
Mafuta yatapanda bei, Kila kitu kitapanda bei acheni malalamiko🐒
 
Ahlan wa Sahlan

Habari zenu wana JF:

Kumekuwa na tabia ya upotoshaji inayoendelea hapa nchini kwa watu kumlaumu rais kwa hali ya kupanda kwa gharama za maisha inavyoendelea kila kukicha, kubwa ni hili la kupanda kwa gharama za mafuta ya petroleum, diesel na mafuta ya taa.

Bei ya mafuta kwa nchi zisizozalisha mafuta zimepanda kwa kiasi kikubwa duniani kote. Pigieni simu watu wa Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kampala , Lusaka, Kigali n.k muwaulize bei za mafuta zipoje.

Tembeleeni hii tovuti mjionee bei za mafuta duniani.

znz je??
 
Kuhusu Zanzibar,sio tuu mafuta ni nafuu lakini takribani vitu vyote kule ni nafuu kuliko Bara miaka yote hata kabla hujazaliwa wewe,huo unafuu haujaanza leo wala Jana..
Yeah, nasikia hata gharama za kuunganishiwa umeme zimeshuka ilhali kwa Tanganyika imepanda, umeme huo huo unaotoka Tanganyika, ni kweli?

Kwanini sasa Znz bei iwe chini kwa vitu vingi ukilinganisha na huku Tanganyika? Wanapata feva kutoka wapi?
 
Huu ni ujinga wa Hali ya Juu,unaposema wafute hizi Kodi manake unasema madawa yapungue hospital,wasijenge barabara nk Ili watu wapumue sio?
Kabla ya kubishana na Zitto (ingawa Zitto huaga simkubali kwa mambo mengi sana but that doesn't mean kwamba HANA point, no ) ni vizuri kujiridhisha na wewe wenyewe kama umemuelewa Zitto na pia unajua idadi ya KODI zilizopo kwenye mafuta; maanake naona tayari umeisha potosha, mwenzio kasema punguza na wewe umesema WAFUTE, wapi Zitto kapendekeza KUFUTA!? So to me is either hujamuelewa Zitto na pendekezo lake au umeamua kupotosha makusudi or huelewi chochote kuhusu idadi ya kodi zilizopo kwenye mafuta. Again, remember hakuna anae ilaumu serikali/rais; watu wanakuja na mapendekezo ya nini kifanyike kuhusu hili sakata la mafuta
 
Rais nae amelegea legea kama mlenda tena anakomaa tegemeeni vitu kupanda zaidi.
 
Wanyonge hatawaki kujua sababu za huko nje, wanataka kuona Rais wetu anafanya nini kuwapunguzia ugumu wa maisha...
 
Bunge limesitisha ratiba yake ili kupisha hoja ya dharula kupinga ongezeko la bei ya mafuta.

Je wabunge nao ni stupid Monkeys [emoji205] kama mimi?

Je wabunge nao ni akili za visoda?

Acha kuwa ukijiona mjuaji kwenye masuala kama haya ya kitaifa na yanayoigusa jamii kwa upana zaidi.

Wewe unaonekana kuwa mlala bure na familia ya walamba asali.
Huyo ni mmoja ya wale wanaoishi kwa shemeji analala sebuleni kwa dada yake.
 
Ahlan wa Sahlan

Habari zenu wana JF:

Kumekuwa na tabia ya upotoshaji inayoendelea hapa nchini kwa watu kumlaumu rais kwa hali ya kupanda kwa gharama za maisha inavyoendelea kila kukicha, kubwa ni hili la kupanda kwa gharama za mafuta ya petroleum, diesel na mafuta ya taa.

Bei ya mafuta kwa nchi zisizozalisha mafuta zimepanda kwa kiasi kikubwa duniani kote. Pigieni simu watu wa Nairobi, Mombasa, Kisumu, Kampala , Lusaka, Kigali n.k muwaulize bei za mafuta zipoje.

Tembeleeni hii tovuti mjionee bei za mafuta duniani.

naomba kujua bei za mafuta zanziba zipoje kabla hatujaenda huko unapo tupeleka, tukumbuke tunapo fananisha hizi bei tusikimbilie kuchukua mifano ya bei ya juu tuu tuchukue na ya bei ya chini pia, lakini tunapofananisha pia tuangalie na kipoto cha chini cha kila mwananchi cha nchi husika tunazofananisha nazo.
pia tuanapo angalia pato la hao wananchi tuangalie na fursa zilizopo za kiuchumi kwa hizo nchi na tufananishe na fursa tanzania ilizo nazo.
Hebu fikiria je tz imeongeza asilimia yoyote ktkt siku ya may mosi kenya wameongezewa 12%, na nchi nyingine pia zimeongeza ila Tz lile jambo letu lipo palepale..... hebu rejea kauli ya nilikuwa marekani bei ya petrol hapa tz ni ndogo kuliko marekani, je wa tz wanafanana kipato na wamarekani nikukumbushe.
nikukumbushe pia kauli ya mama kila kitu kitapanda bei, kiongozi wa nchi alipaswa kuangalia ni namna gani na kwa mikakati ipi tutaepuka kupanda kwa bei ya vitu kutokana na vita ya Urusi na ukrein na si vinginevyo
 
Back
Top Bottom