Afisa Elimu Jiji La Tanga, wazazi tunaomba ufafanuzi wa hii michango ya fedha

Hili hata mkoa wa pwani lipo,shule ya msingi misugusugu ushahidi wangu wa kwanza,ongezea na mchango wa msosi
Kwa hiyo mkuu unalalamikia hadi mchango wa msosi? Mbona haya masuala ya vyakula huwa yanaamuliwa kwenye vikao vya uongozi wa shule na wazazi? Au huko kwenu waliibuka tu?
 
Kwa hiyo mkuu unalalamikia hadi mchango wa msosi? Mbona haya masuala ya vyakula huwa yanaamuliwa kwenye vikao vya uongozi wa shule na wazazi? Au huko kwenu waliibuka tu?
Hakuna kitu sipendi Kama mtoto kushinda shule na kurudi nyumbani saa 12,Kisha kila jumamosi mitihani
 
Hii IPO kwenye manispaa zote walimu wa shule za msingi Wana ukwasi kuliko za sekondari
 


 
Mitoto ya siku hizi imekalia season tu basi bora muda mwingi ibanwe na ratiba nyingi za shuleni siku nzima ili irudipo majumbani iwe hoi ni kula na kupumzikia njozini
 

Wazazi wengi wanapambana kiuchumi kuliko malezi ya watoto!
Watoto wa siku hizi hawahitaji hata kanafasi kanachokosa uangalizi wa maana na usimamizi.
Akirudi mapema nyumbani na kukosa uangalizi wa michezo ya hapo nyumbani hatari sana kuliko unavyofikiria.
SHULE NI SOCIAL ORGANIZATION KUBWA AMBAPO KILA KITU KWA MTOTO ANAKIPATA kwani hata michezo ipo na inakuwa na uangalizi bora kutoka kwa walimu.
 
Stop that unsubstantiated statements! Kwa shule zipi? shule darasa lina watoto 200 kuna uangalizi hapo? Kuna kusoma hapo? Unaleta mzaha kenye maisha ya watoto
 
Stop that unsubstantiated statements! Kwa shule zipi? shule darasa lina watoto 200 kuna uangalizi hapo? Kuna kusoma hapo? Unaleta mzaha kenye maisha ya watoto
Kipi bora kwa mtazamo wako!
Ni bora hilo darasa lenye watoto 200 lenye uangalizi wa huyo mwalimu mmoja kuliko atoke mapema ili akalindwe na shamba boy.
 
Kipi bora kwa mtazamo wako!
Ni bora hilo darasa lenye watoto 200 lenye uangalizi wa huyo mwalimu mmoja kuliko atoke mapema ili akalindwe na shamba boy.
Mtot anayesoma darasa la watu 200, nyumbani hakuna shamba boy! shamba boy ni kwa matajiri watoto wao hawaendi huko1
 
Wazazi acheni lawama, mia 200 kwa mwezi ni elf 6 ukitoa weekends haifiki hata elf 5 kwa mwezi, kama unamjali mtoto unalia Lia elf 5 je vitabu mnanunua kweli???

Unapata kishipa mwalimu akipata hivo vi mia mbili mbili ilhali mtoto wako anapata msaada wa kuchangamsha akili kwa Kukutana na maswali Kila siku

Wakifeli mnawalaumu walimu, stupid!
 
Hakika wewe ni fala sana.
Inaelekea huna elimu yoyote ktk bichwa lako.
Shule kama hiyo na zingine za namna hiyo hakuna elimu yoyote wanayopata watoto hapo. Ni mateso na kukonda tu.
Sana sana wanakaririshwa maswali tu. Baada ya miezi 2 au 3 Kila kitu hakuna kichwani.
Walioweka mapumziko ya likizo Kwa ajili ya mtoto walikuwa na akili sanaaaa .
 
Watoto wenu vichwa vigumu sana
 
Haya yote yana sababishwa na wazazi pindi watoto wanapo feli. Pili ni makaripio ya viongozi wa juu wa elimu kwa waliopo chini Yao. Kwa ujumla viongozi hadi walimu wamekuwa wakifanya kazi kwa hofu ya kutumbuliwa iwapo matokeo ya mkoa au wilaya yako ni mabovu. Walimu nao wamekuwa wakiambiwa watahamishiwa vijijini km hawatafaulisha (utadhani wao ndiyo wanafanya mitihani). Ndio maana liliibuka suala la makambi kwa darasa 4 na kidato cha 4. Kitu ambacho utekelezaji wake basi tu.

Ila sisi wazazi nao vigeugeu, wanafunzi wakifeli maneno, wakifaulu sana eti mitihani ya siku hizi mirahisi sana wanafunzi wanakaririshwa tu lakini uwezo mdogo. Walimu wakitumia njia za kivita kufaulisha wazazi wanasema eti wanafunzi wananyanyasika. Sasa Walimu washike lipi. Acheni Walimu wapige kazi.
 
Hata kama iweje lakini sio kama muda wrote niwakusomatu.
Shuleni watoto hawafundishwi kupika,kuosha vyombo,kufua, no

Muda wa kupumzika na kufanya mambo yake binafsi nimuhim sana
 
ASANTE SANA UBARIKIWE.

Wazazi waliposikia elimu bure wakahisi serikali inawapenda sana mbona viongozi hawapeleki watoto wao kweny hio bure. Mzazi elimu ni haki ya msingi kwa mtoto kuchangia ni lazima kama hutaki michango ya 200 nenda private ukalipe 7m alafu unyooshe miguu hakuna vya bure. Alafu hata kama walimu wanakula hizo 200 mnalalamika kweli mbona viongozi wanakula bilioni za fedha hamlalamiki.
 
Kuna kitu hakiko sawa sehemu, serikali kwa sasa ni kama imeamua acha liwalo na liwe
 
Walimu ndo wanafundisha wanaelewa changamoto za watoto wanapojifunza kama hutaki mtoto wako afundishwe muda wa ziada wasiliana nao watamruhusu mapema arudi nyumbani apumzike kama unavyotaka usitafute justification kuharibu mipango mizuri ya walimu kwa hawa watoto.
 
[emoji1787][emoji1787]Kuna Shule moja mpaka mwalimu aliona Kuna kelele hizohizo akawa anawatangazia wale ambao wanaitaji kusoma muda wa ziada anawafundisha muda huo na hao wengine walikua wanakatazwa na wazazi wao aliachana nao wabaki na wazazi Hakua hata na muda wa kuwafatilia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…