Afrika hakuna nchi vyama vya upinzani vimeleta nafuu kwa wananchi vikifika Ikulu

Afrika hakuna nchi vyama vya upinzani vimeleta nafuu kwa wananchi vikifika Ikulu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Huwa nafuatilia sana siasa za dunia na Afrika. Afrika yote ni kama vile inaongozwa na Rais mmoja, bunge moja, mahakama moja na baraza la mawaziri moja. Hali yetu inafananafanana kwa kila kitu. kiuchumi, siasa, na huduma za jamii.

Huduma na maendeleo yetu yako chini relatively kulinganisha na zile za mabara mengine. Hii inaonyesha kuwa kuna common factors zinazolifanya bara lote liwe kwenye mstari mmoja kando na vyama vya siasa na viongozi wa nchi.

Vyama vya upinzani vya Afrika vinatumia hali hii mbaya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoa majibu ya uongo na laghai kwa wananchi wanaotamani hali bora zaidi kuliko waliyonayo chini ya vyama tawala. Vyama vya upinzani vinajenga hoja kuwa hali mbaya ya wananchi inatokana na uzembe wa vyama tawala na sio kingine chochote zaidi ya hapo. Hivyo, Wananchi wanapoamua kuvipa kura vya upinzani kushika dola wanajikuta hali yao inasalia ileile vilevile au wanaona afadhali ya zamani kule walikotoka kwa watawala wa zamani.

AFrika hakuna ushahidi kama nchi zilizobadilisha vyama vya siasa vinavyotawala wamepata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kuliko ilivyokuwa. Hakuna ushahidi kama wananchi wa Kenya, Malawi, Zambia, Libya, Sudani, Liberia ambako wamewahi kubadilisha vyama vyao tawala walipata nafuu kiichumi na kijamii kuliko wananchi wa Uganda, Tanzania, Rwanda, South Africa na Zimbambwe ambako vyama tawala viko kwa muda mrefu. Wala hakuna ushahidi kama maisha chini ya Uhuru Kenyatta yalikuwa mabaya kuliko maisha chini ya Willium Ruto. Walibya chini ya Gafaffi na chini ya watawala wa sasa. Wazamibia chini ya Kaunda na chini ya Chiluba, waliberia chini ya Sariff na choni ya George Wear, nk.

Afrika tunahitaji kuisaka hiyo common factor (x-factor) inayoliweka bara lote kwenye mstari mmoja wa maendeleo na ubora wa huduma badala ya kuwalaghai na kuwapa sababu za uongo wananchi wetu juu ya kwanini tuko hivi kiuchumi na kijamii.

Huwa nasikiliza na kufuatilia kampeni za vyama vya upinzani wanapokuwa wanaomba kura; hakuna chama kinachowaambia vijana ukweli kama vile sisi mkiituchagua tutahakikisha kuwa kila kijana anafanyakazi kwelikweli na kulipa kodi kwelikweli kwa ukamilifu, hakuna kijana kuzurura wakati na siku za kazi, hakuna kupanga bidhaa chini wala kuziba njia za waenda kwa miguu, tutahakikisha kuwa biashara ya ukahaba na madada poa inapigwa marufuku, hakuna kujenga nyumba kiholela na watu waliojenga mabondeni wataondolewa wote ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa.

Tuhakikisha kila kijana analima eka zake 2 za pamba ili kuinua hali zao za kiuchumi na taifa kupata fedha za kigeni. Hakuna anaewaambia vijana ukweli kuhusu kazi, kulipa kodi na utaratibu na siasa za dunia na hali ya masoko duniani badala yake wanawadanganya kwa ahadi laini kuwa wao kuna mahali watapatekenya ili maisha yao yawe bora kuliko sasa. Hii ni tofauti na wazungu ambao wanawaambia ukweli wapiga kura wao kwa kutumia sera zao safi au mbaya ili wananchi wachague wenyewe sera za chama gani ni bora.

Tunaweza kuuana bure wenyewe kwa wenyewe kwa sababu nyingine za uongo na kuficha sababu halisi za kuuana.
 
Huwa nafuatilia sana siasa za dunia na Afrika. Afrika yote ni kama vile inaongozwa na Rais mmoja, bunge moja, mahaka moja na baraza la mawaziri moja. Hali yetu inafananafanana kwa kila kitu. iuchumi, siasa, na huduma za jamii.

Huduma na maendeleo yetu yako chini relatively kulinganisha na zile za mabara mengine. Hii inaonyesha kuwa kuna common factors zinazolifa

Tunaweza kuuana bure wenyewe kwa wenyewe kwa sababu nyingine za uongo na kuficha sababu halisi za kuuana.

Hivi unajia bado kuna vyama vingapi vilivyopigania uhuru na bado vipo madakani? Kwa taarifa tu havizidi sita.

Sasa tuambambie hizo nchi zina maaendeleo gani kuzishinda nchi zinazoongozwa na vywama vya upinzani Kama unavyodai wewe....!!?
 
Huwa nafuatilia sana siasa za dunia na Afrika. Afrika yote ni kama vile inaongozwa na Rais mmoja, bunge moja, mahaka moja na baraza la mawaziri moja. Hali yetu inafananafanana kwa kila kitu. iuchumi, siasa, na huduma za jamii.

Huduma na

Tunaweza kuuana bure wenyewe kwa wenyewe kwa sababu nyingine za uongo na kuficha sababu halisi za kuuana.

Halafu itoe Uganda na Rwanda kwenye hiyo list yako. List yako ni Tanzania, South Africa. Namibia, Angola, Mozambique na Zimbabwe. Tuambie hizo nchi zinatofautianaje na nyingine.
 
Hivi unajia bado kuna vyama vingapi vilivyopigania uhuru na bado vipo madakani? Kwa taarifa tu havizidi sita.

Sasa tuambambie hizo nchi zina maaendeleo gani kuzishinda nchi zinazoongozwa na vywama vya upinzani Kama unavyodai wewe....!!?
Ndio maana nasema vyama vya upinzani havijaleta nafuu katika nchi zao hata kama vilipewa nafasi ya kuongoza. Walichofanya ni kupewa nafasi ili iwe zamu yao tu ya kufanya mambo yaleyale kwasababu kuna sababu nyingine za kwanini hali yetu Afrika iko hivi kando ya utawala.
 
Uko sahihi, basi ccm tokeni madarakani ili wananchi waamini hizo sababu unazosema. Sio uone huwezi kufanya maisha ya wananchi wainuke, lakini hutaki kutoka aingie mwingine ambaye unajua naye atashindwa.
 
Hakuna takwimu kuwa ukiachiwa wewe Ikulu nchi itakuwaje na wananchi watakuwaje. Tuambie hata kwa kutudanganya tu nini utafanya kwenye kilimo, ajira kwa vijana, uvuvi, elimu, afya, viwanda tofauti na anavyofanya CCM. Mfano, Trump yeye aliwaambia wapiga kura wake kama wakimchagua atafukuza wahamiaji haramu wote na kurejesha viwanda vilivyokuwa vimehamishiwa Asia virudi tena Amerika wakampa kura, na kweli alipopata urais akawatimua wahamiaji kama alivyosema na kujenga ukuta mpaka na mexco. Nyie sera zenu ni zipi ili tuwape kura au tusiwape kura? Hii ya kuikejeli CCM na viongozi wa serikali sio sera wananchi wanayoitaka, labda wananchi lakini wanaovuta bhangi.

kama huna sera zinazopimika ni heri tu ukazuiwa kwa nguvu zote usifike Ikulu, maana huna cha kufanya unataka ukapate cha kufanya utakapofika Ikulu. Hiyo inawezakuwa hatari kwa taifa. Wewe tuambie tu kuwa sisi tutakapofika Ikulu pale tutafanya yafuatayo kwenye Kilimo, kwenye umeme, kwenye usafiri, kwenye elimu, nk
 
Hata ASP na TANU vilikuwa vyama vya upinzani, vilipopewa madaraka vimebakia kuteka raia wake na kukopa pesa nje. Very stupid
Sikubishii, sasa wewe nionyeshe chama cha upinzani cha nchi gani Afrika ambacho kilibadilisha namna mambo yalivyokuwa huko nyuma na sasa vijana wanapiga vigelegele na vifijo kwa furaha ili nasisi tuseme naaam!! tufanye kama wale.

Tulichokiona sisi ni chama cha siasa kuchoma moto hata hiki kidogo tulichokidunduliza kwa taabu na mateso makubwa kwa miaka 64.
 
Ndiyo yale yale ya miaka ya Nyuma, kauli mbiu Yao ilikuwa: "Msichague upinzani, upinzani utaleta fujo katika nchi na hatimaye vita" .

October 29 riots zimetokea CCM bado ingali madarakani.
 
Huwa nafuatilia sana siasa za dunia na Afrika. Afrika yote ni kama vile inaongozwa na Rais mmoja, bunge moja, mahakama moja na baraza la mawaziri moja. Hali yetu inafananafanana kwa kila kitu. kiuchumi, siasa, na huduma za jkweli wapiga kura wao kwa kutumia sera zao safi au mbaya ili wananchi wachague wenyewe sera za chama gani ni bora.

Tunaweza kuuana bure wenyewe kwa wenyewe kwa sababu nyingine za uongo na kuficha sababu halisi za kuuana.
Hakuna nchi Africa iliyopata maendeleo kwa kuongozea na chama kilicholeta uhuru miaka ya 1960
 
Hakuna takwimu kuwa ukiachiwa wewe Ikulu nchi itakuwaje na wananchi watakuwaje. Tuambie hata kwa kutudanganya tu nini utafanya kwenye kilimo, ajira kwa vijana, uvuvi, elimu, afya, viwanda tofauti na anavyofanya CCM. Mfano, Trump yeye aliwaambia wapiga kura wake kama wakimchagua atafukuza wahamiaji haramu wote na kurejesha viwanda vilivyokuwa vimehamishiwa Asia virudi tena Amerika wakampa kura, na kweli alipopata urais akawatimua wahamiaji kama alivyosema na kujenga ukuta mpaka na mexco. Nyie sera zenu ni zipi ili tuwape kura au tusiwape kura? Hii ya kuikejeli CCM na viongozi wa serikali sio sera wananchi wanayoitaka, labda wananchi lakini wanaovuta bhangi.

kama huna sera zinazopimika ni heri tu ukazuiwa kwa nguvu zote usifike Ikulu, maana huna cha kufanya unataka ukapate cha kufanya utakapofika Ikulu. Hiyo inawezakuwa hatari kwa taifa. Wewe tuambie tu kuwa sisi tutakapofika Ikulu pale tutafanya yafuatayo kwenye Kilimo, kwenye umeme, kwenye usafiri, kwenye elimu, nk
Sera wanaambiwa wapiga kura, kisha wanaamua kupitia box la kura. Na wala sera sio hadi ziwaridhishe ccm.
 
Hakuna nchi Africa iliyopata maendeleo kwa kuongozea na chama kilicholeta uhuru miaka ya 1960
Kwako wewe maendeleo ni nini?

Mimi hapa ukiniuliza maendeleo nini nitakwambia idadi wa watu wanaokujua kusoma na kuandika, idadi ya watu wenye mahali pa kulala na chakula. Nitasema mafanikio kwenye sanaa na michezo, nitasema usambazaji wa huduma za afya, umeme, barabara, reli, shule na maji kwa watu, nitasema uhuru wa vyombo vya habari na kupata habari. Nitakuonyesha utawala wa sheria, nk. Sasa katika mambo hayo yote tanzania chini ya CCM inagonga vichwa vya habari Afrika.
 
Sera wanaambiwa wapiga kura, kisha wanaamua kupitia box la kura. Na wala sera sio hadi ziwaridhishe ccm.
CCM ina wajibu wa kukwambia wewe muongo unawalaghai watoto wasiokuwa na exposure kama yako. Ndiyo maana Nyerere ilimlazimu kutoka mafichoni na kwenda kumpigia kampeni Mkapa na kumwambia Mrema wewe muongo, na alikuwa muongo kweli. Asingefanya vile mrema angechukua nchi kwa uongo na asijue anaipeleka wapi.
 
Afrika watu wanabweteka ,kulaumu tu viongozi ,dini na ukoloni.

Wakati mpaka wazungu walifanyiwa ukoloni ,watakuambia china hakuna dini labda kama china ya sayari ya Pluto...Wanashikiwa akili na wanasiasa ambao wanatafuta unafuu wa maisha ,uliona wapi wanasiasa wakaleta maendeleo.
 
CCM ina wajibu wa kukwambia wewe muongo unawalaghai watoto wasiokuwa na exposure kama yako. Ndiyo maana Nyerere ilimlazimu kutoka mafichoni na kwenda kumpigia kampeni Mkapa na kumwambia Mrema wewe muongo, na alikuwa muongo kweli.
Zama za Nyerere zilishapita, kizazi hiki kinajitambua. Naona unadhani hiki ni kizazi cha kuchaguliwa mke/mume na wazazi. Usitake kufanya kuwa ccm ndio wana haki ya kufanyia wananchi maamuzi. Box la kura liheshimiwe, anayeshinda atangazwe sio hizi porojo zako za mbio za mwenge.
 
Hakuna nchi Africa iliyopata maendeleo kwa kuongozea na chama kilicholeta uhuru miaka ya 1960
Onyesha sasa nchi ya Afrika iliyoendelea kwa kukiangusha chama cha ukombozi. Simpo.

lazima tumsake na tumtaje hadharani adui yetu halisi Afrika badala ya kuparurana wenyewe huku adui yetu akiwa anachekelea pembeni anatuangalia.

Mtu ambae alikaribia kabisa kumkamata huyo adui alikuwa Magufuli.

Nadhani watu wote kufanyakazi na kulipa kodi sawasawa ndiyo adui yetu namba moja rahisi tunaemfahamu. Wazungu wanafanyakazi na wanalipa kodi kwa nguvu na kwa hiyari. Sisi hatufanyikazi na hatulipi kodi. Viongozi wetu wanaogopa kutoza kodi watu na kuwalazimisha watu wote wafanyekazi kwa kuogopa kukosa kura. Na mwasisi wa jambo hilo alikuwa Mwl. Nyerere. TANU ilipata wanachama wengi wakati wa ukoloni kwaahadi kuwa atafuta kodi kama tukipata Uhuru.
 
Ndio maana nasema vyama vya upinzani havijaleta nafuu katika nchi zao hata kama vilipewa nafasi ya kuongoza. Walichofanya ni kupewa nafasi ili iwe zamu yao tu ya kufanya mambo yaleyale kwasababu kuna sababu nyingine za kwanini hali yetu Afrika iko hivi kando ya utawala.
Watu weusi ni mifugo tu inayoweza kuongea, ila ubinadamu wao, bado muumbaji wao yuko maabara anawatengeneza akili ikae sawa.
 
Onyesha sasa nchi ya Afrika iliyoendelea kwa kukiangusha chama cha ukombozi. Simpo.

lazima tumsake na tumtaje hadharani adui yetu halisi Afrika badala ya kuparurana wenyewe huku adui yetu akiwa anachekelea pembeni anatuangalia.

Mtu ambae alikaribia kabisa kumkamata huyo adui alikuwa Magufuli.

Nadhani watu wote kufanyakazi na kulipa kodi sawasawa ndiyo adui yetu namba moja rahisi tunaemfahamu. Wazungu wanafanyakazi na wanalipa kodi kwa nguvu na kwa hiyari. Sisi hatufanyikazi na hatulipi kodi. Viongozi wetu wanaogopa kutoza kodi watu na kuwalazimisha watu wote wafanyekazi kwa kuogopa kukosa kura. Na mwasisi wa jambo hilo alikuwa Mwl. Nyerere. TANU ilipata wanachama wengi wakati wa ukoloni kwaahadi kuwa atafuta kodi kama tukipata Uhuru.
Nani halipi kodi nchi hii ww mfuata Mkumbo? Hizo bidhaa na huduma mlizojaza makodi inakuwaje? Ama hujui unaloongea?
 
Afrika watu wanabweteka ,kulaumu tu viongozi ,dini na ukoloni.

Wakati mpaka wazungu walifanyiwa ukoloni ,watakuambia china hakuna dini labda kama china ya sayari ya Pluto...Wanashikiwa akili na wanasiasa ambao wanatafuta unafuu wa maisha ,uliona wapi wanasiasa wakaleta maendeleo.
mtanga, wanasiasa wamefanya kenya kwenda kununua mahindi zambia huku TZ bei ikidorora
 
Back
Top Bottom