Huwa nafuatilia sana siasa za dunia na Afrika. Afrika yote ni kama vile inaongozwa na Rais mmoja, bunge moja, mahakama moja na baraza la mawaziri moja. Hali yetu inafananafanana kwa kila kitu. kiuchumi, siasa, na huduma za jamii.
Huduma na maendeleo yetu yako chini relatively kulinganisha na zile za mabara mengine. Hii inaonyesha kuwa kuna common factors zinazolifanya bara lote liwe kwenye mstari mmoja kando na vyama vya siasa na viongozi wa nchi.
Vyama vya upinzani vya Afrika vinatumia hali hii mbaya ya kiuchumi, kisiasa na kijamii kutoa majibu ya uongo na laghai kwa wananchi wanaotamani hali bora zaidi kuliko waliyonayo chini ya vyama tawala. Vyama vya upinzani vinajenga hoja kuwa hali mbaya ya wananchi inatokana na uzembe wa vyama tawala na sio kingine chochote zaidi ya hapo. Hivyo, Wananchi wanapoamua kuvipa kura vya upinzani kushika dola wanajikuta hali yao inasalia ileile vilevile au wanaona afadhali ya zamani kule walikotoka kwa watawala wa zamani.
AFrika hakuna ushahidi kama nchi zilizobadilisha vyama vya siasa vinavyotawala wamepata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kuliko ilivyokuwa. Hakuna ushahidi kama wananchi wa Kenya, Malawi, Zambia, Libya, Sudani, Liberia ambako wamewahi kubadilisha vyama vyao tawala walipata nafuu kiichumi na kijamii kuliko wananchi wa Uganda, Tanzania, Rwanda, South Africa na Zimbambwe ambako vyama tawala viko kwa muda mrefu. Wala hakuna ushahidi kama maisha chini ya Uhuru Kenyatta yalikuwa mabaya kuliko maisha chini ya Willium Ruto. Walibya chini ya Gafaffi na chini ya watawala wa sasa. Wazamibia chini ya Kaunda na chini ya Chiluba, waliberia chini ya Sariff na choni ya George Wear, nk.
Afrika tunahitaji kuisaka hiyo common factor (x-factor) inayoliweka bara lote kwenye mstari mmoja wa maendeleo na ubora wa huduma badala ya kuwalaghai na kuwapa sababu za uongo wananchi wetu juu ya kwanini tuko hivi kiuchumi na kijamii.
Huwa nasikiliza na kufuatilia kampeni za vyama vya upinzani wanapokuwa wanaomba kura; hakuna chama kinachowaambia vijana ukweli kama vile sisi mkiituchagua tutahakikisha kuwa kila kijana anafanyakazi kwelikweli na kulipa kodi kwelikweli kwa ukamilifu, hakuna kijana kuzurura wakati na siku za kazi, hakuna kupanga bidhaa chini wala kuziba njia za waenda kwa miguu, tutahakikisha kuwa biashara ya ukahaba na madada poa inapigwa marufuku, hakuna kujenga nyumba kiholela na watu waliojenga mabondeni wataondolewa wote ndani ya siku 100 baada ya kuapishwa. Tuhakikisha kila kijana analima eka zake 2 za pamba ili kuinua hali zao za kiuchumi na taifa kupata fedha za kigeni. Hakuna anaewaambia vijana ukweli kuhusu kazi, kulipa kodi na utaratibu na siasa za dunia na hali ya masoko duniani badala yake wanawadanganya kwa ahadi laini kuwa wao kuna mahali watapatekenya ili maisha yao yawe bora kuliko sasa. Hii ni tofauti na wazungu ambao wanawaambia ukweli wapiga kura wao kwa kutumia sera zao safi au mbaya ili wananchi wachague wenyewe sera za chama gani ni bora.
Tunaweza kuuana bure wenyewe kwa wenyewe kwa sababu nyingine za uongo na kuficha sababu halisi za kuuana.