Hakuna takwimu kuwa ukiachiwa wewe Ikulu nchi itakuwaje na wananchi watakuwaje. Tuambie hata kwa kutudanganya tu nini utafanya kwenye kilimo, ajira kwa vijana, uvuvi, elimu, afya, viwanda tofauti na anavyofanya CCM. Mfano, Trump yeye aliwaambia wapiga kura wake kama wakimchagua atafukuza wahamiaji haramu wote na kurejesha viwanda vilivyokuwa vimehamishiwa Asia virudi tena Amerika wakampa kura, na kweli alipopata urais akawatimua wahamiaji kama alivyosema na kujenga ukuta mpaka na mexco. Nyie sera zenu ni zipi ili tuwape kura au tusiwape kura? Hii ya kuikejeli CCM na viongozi wa serikali sio sera wananchi wanayoitaka, labda wananchi lakini wanaovuta bhangi.
kama huna sera zinazopimika ni heri tu ukazuiwa kwa nguvu zote usifike Ikulu, maana huna cha kufanya unataka ukapate cha kufanya utakapofika Ikulu. Hiyo inawezakuwa hatari kwa taifa. Wewe tuambie tu kuwa sisi tutakapofika Ikulu pale tutafanya yafuatayo kwenye Kilimo, kwenye umeme, kwenye usafiri, kwenye elimu, nk