One step at a time, it took ages and a lot of international pressure mpaka apartheid ikapigwa chini hivyo mapambano dhidi ya udhalimu unaofanywa na watawala wa TZ bado yana safari isiyo nyepesi ila gradually yanaendelea kukua, katika ya mapambano huwa kuna traitors, two headed serpents na sellouts na hao ndiyo hurudisha nyuma, huchelewesha na kupambana kukatisha tamaa harakati.
Mapambano ya October-29th-2025 dhidi ya udhalimu wa Samia ni mfano halisi kwani yale mauaji aliyoyatekeleza huyo Samia na genge ni sawa na mauaji yaliyofanywa na SA apartheid regime yale ya Sharpeville massacre ya 1960 na baadaye mapambano makubwa zaidi na mauaji makubwa zaidi ya Soweto massacre(Soweto uprising) ya 1976. Ukiangalia revolt growth ya 1960 ilikuwa ni ndogo lakini wakati oppression ikiongezeka na watu wanakuwa more determined tena hao watu ni teens si watu wazima ndipo 1976 revolt ikawa kubwa na mauaji yakawa makubwa zaidi huku good numbers za Wazulu(Kwazulu Natal natives) waki-support utawala huo dhalimu kwani chifu wao alikuwa ni chawa wa Makaburu. A lot of similarities with our current pathetic TZ scenarios.
Kuwaza kwa aina hii safari yetu ya maendeleo inaonekana bado ndefu sana wallah.
Tanzania iko huru tayari baada ya kuwafukuza wazungu wa Ulaya Magaribi ambao waliligawana bara letu tukiwemo sisi kwasabu ya kupata malighafi za bwerere kama madini, pamba, pembe za ndovu, nk, kupata wafanyakazi (nguvukazi) wa ujira mdogo (manamba, watumwa) na masoko ya kuuzia bidhaa zao walizozalisha kwenye viwanda vyao kama vile nguo, sukari, shanga, vioo, bunduki, sahani, nk. Mahitaji haya bado wanayo mpaka leo hii ninapoandika hapa hatabkama vyama vya ukombozi viliwafukuza physically kutoka Afrika na kupata huo wanaouita uhuru.
Kwa kuwafukuza wazungu kutoka Afrika vyama vya ukombozi vilikosana sana na wazungu maana ziko nchi kama tz ambazo zilikwenda mbali zaidi kwa kutaifisha "mali zao" kama vile ardhi, mashamba viwanda, mashule; na mbaya zaidi zilihamia upande wa Urusi na China kiitikadi. Ugomvi ulikuwa mkubwa kiasi kwamba viongozi wengi waliowafukuza wakoloni na kuonekana kuwakatia upatikanaji wa malighafi, nguvukazi na masoko ya bidhaa zao waliwaondoa au waliuliwa na kuweka watu wao (viongozi mataahila) ambao wangewahakikishia upatikaji wa zile rasilimali, nguvukazi na masoko ya bidhaa zao bila vikwazo. Nchi za magharibi haziwezi kusurvive bila kupata rasilimali/malighafi ya bure, nguvu kazi rahisi na masoko ya bidhaa zao.
Vyama vya upinzani vyooye 100% Afrika huwa vinapata msaada wa kujijenga, kujiendesha na kupambana na vyama vya ukombozi kutoka nchi zilezile zilizofukuzwa Afrika na vyama vya ukomnozi kama CCM, ANC, Frelimo, etc. Vyama vyote vya upinzani ni vyama rafiki na nchi za Magharibi, na sio rafiki wa nchi za Mashariki kama China, Urusi, Cuba au N.Korea. Jiulize ni kwanini chadema sio rafiki wa China au Urusi?. Maana yake ni nchi zilezile ambazo zilikuwa wakoloni wetu ndiyo zinakuwa nyuma ya vyama vyetu vya upinzani Afrika.
Na inafahamika agenda kuu ya nchi za Magharibi (wakoloni wetu) ni malighafi rahisi, nguvukazi rahisi na masoko rahisi ya bidhaa zao. Hivyo, tunaweza kusema moja kwamoja kuwa demokrasia safi kwa jicho la nchi za Magharibi ni vyama vya upinzani wanavyovilea na kuvipatia fedha zao kushinda uchaguzi, kinyume na hapo uchaguzi haukua huru na haki. Katika hali tu ya kawaida kama mwanafunzi wako akifeli na wewebmwalimu wake utahesabiwa umefeli, hivyo kushindwa kwa vyama vya upinzani Afrika ni kushindwa kwa wakoloni pia; comments zao lazima ziwe nyingi na negatives kuhusu chaguzi zetu. Na wakishindwa kwenye chaguzi wako tayari kusupport kijeshi, lengo likiwa kupata rasilimali rahisi, nguvukazi na masoko kutoka kwa wanaemsapoti.
CCM ni chama cha ukombozi kinachosambaza nchi nzima huduma za umeme, maji, elimu, afya, barabara, reli, pembejeo, ardhi kwa kila mtanzania na uchimbaji madini kwa kila mtanzania. Ubaya wa CCM uko wapi ili wote tuwe na ufahamu mmoja. Mpaka sasa vyama vya upinzani vinashindwa kuwashawishi watanzania ili nao wauone ubaya wa CCM na waunge mkono kile wanachokisema vyama vya upinzani.
Watanzania nao wana akili, macho, masikio na pua ya kunusa na mikono ya kupapasia. Wanaona wenyewe kwa macho yao:
1. Amani na utulivu
2. Mgawanyo wa ardhi yao, kila mtu ni rahisi kipata kipande
3. Huduma za usafiri
4. Huma za umeme
5. Elimu kila kijiji, kila kata
6. Afya kila kijiji, kila kata kila tarafa kila wilaya
7. Michezo, timu zetu zinafanya vizuri na ligi imejaa wachezaji wageni
8. Chakula kipo
9. Madini yanachimbwi
10. BANDARIA zinatema. Etc.
Watanzania hawa pia huwa wanatembea nchi nyingine za Afrika na kujifanyia benchmarking na wenzao, wanajiona ama wako sawa nao au wamewazidi mbali sana kwenye ardhi, amani, afya, etc.