Afrika hakuna nchi vyama vya upinzani vimeleta nafuu kwa wananchi vikifika Ikulu

Afrika hakuna nchi vyama vya upinzani vimeleta nafuu kwa wananchi vikifika Ikulu

Kubadi au kutokubadili is not an issue kwani kama nchi imeamua multiparty system basi pawepo transparency ili wananchi wenyewe wachague kwa uhuru chama wanachoamini ndiyo kinafaa kuwaongoza.
Kufanya hivyo ni sahihi kwenye mataifa ambayo wananchi wao wana uelewa mkubwa wa kusiliza sera na ahadi za mgombea na kuzichambua. Kufanya hivyo kwa mataifa haya ambayo bado mpaka leo kuna watu ambao wanajisaidia haja kubwa na kujitawaza kwa kusota chini kwenye mchanga sio sahihi. Hawana uwezo wa kujua nani muongo na nani mkweli, elimu bado. Utafika wakati vyama havitatumia nguvu kubwa kushinda na kushindwa uchaguzi. Sasa hivi bado kabisa
 
yaani mtu atumie hela zenu za mikopo na kodi zenu ndo mje mwite maendeleo,,,
mnahesabiwa shule, hospitali, madaraja na lami ila vitabu vya mahesabu mizani imeinama..
Afrika kuna madalali hakuna viongozi...
Angalau CCM imewezesha kila mtanzania kupata ardhi bila kujali wewe umetoka mkoa gani na dini gani. CCM watu wote ni sawa wanapofika madukani kununua bidhaa awe mwanaCCM au asiwe, wote mnahenya au kufurahi kwa uzito uleule. Ziko nchi zinazoangalia wewe ni chama gani, kabila gani, dini gani ndiyo upate huduma kwa bai yako. Angalau CCM kila mtu njia ya kwenda wilayani kwao kuna barabara ya lami, kila kijiji, kina umeme, shule na zahanati. nchi nyingine maendeleo yanaangalia mtawanyiko wa wanachama, kabila na dini (dhehebu).

Ndiyo maana CCM imechelewa kuangushwa na vyama vya upinzani.
 
Hayo ndio masharti ya ajira zao, kama hawataki waje huku nje tugombanie goli.
Ndiyo maana nakwambia sisi Afrika hatulipi kodi ipasavyo kama wanavyolipa wazungu. Hata mtu ana nyumba za kupangisha huko mitaani lakini halipi kodi kabisa kabisa. Ana mapaka, nguruwe, mbuzi lakini hawalipii kodi, ana kisima chake kachima anachota maji lakini halipi kodi, kwanza hajui kwamba hata maji ni madini.
 
Mpaka wananchi kufanya maamuzi ya kubadili chama tawala kuna mambo ya ovyo wamepitia mf,mfumuko wa bei,ufisadi,utekaji,huduma za kijamii duni,hakuna uwajibikaji,ilani isiyotekelezeka,haki jinai,ukosefu wa ajira na matumizi mabaya ya raslimali za umma,kumbuka vyma tawala vingi vimekaa madarakani muda mrefu halafu unataka mabadiliko ghafla within a short time,say one term pili vyama pinzani vinakumbana na vikwazo vya masalia kwenye mifumo ya utawala .
 
Naunga mkono kwa %100

Tanzania Wananchi wetu bado hawana uwelewa wa kujua msingi wa neno Demokrasia

Kwao wanaongozwa kutokea Misikitini na Makanisani kuchagua yupo ndio kiongozi mzuri au yupi ni m'baya

Demokrasia ya kuongozwa kutokea nyumba za Ibada❗️

Au Demokrasia yenye Ukanda kiongozi wa chama
anatokea wapi kina Bwashehe ❗️

CCM iendelee kutawala miaka mingi ijayo ili kuwakuza Wananchi wawe na uwelewa mpana wa Demokrasia
Wajue Demokrasia haitokei nyumba za Ibada
Kiongozi mzuri sio lazima hawe kwenye imani moja na wewe

Lkn kufikia uko Wananchi kuwa na uwelewa yumkin
Maisha ya Wananchi yataendana vizuri👈

kwani kipindi icho wagombea wetu watafanana na Wagombea wa Ulaya👈

Kule Ulaya mgombea yupo kuomba kura kwenye mambo tofauti na Shida za Msingi za Mwanadamu 👈

Sisi bado tupo kuomba kura kwa kutoa ahadi ya kujenga Barabara nzuri Uduma ya Afya Shule Maji

Wkt Ulaya uko wameshatoka
Miaka mingi nyuma✍️
Nikusema CCM iendelee kuijenga miundombinu mbalimbali
Ili tukifika uko👈

Nasisi sehemu sasa tunawaomba kura kwa vitu sio vya Msingi sio maitaji
ya lazima👈

Apo Wananchi watajua kiongozi bora anasifa zipi na zipi

Sio sasa Wananchi wanaongozwa kutokea nyumba za Ibada kumkataa kiongozi ✍️

japo hanatatizo lolote lkn utasikia tu hatumtaki hatumtaki

Kama wameambiwa kiongozi ni Mchumba wao😂😂

wao ndio wenye kuamua unamtaka au humtaki 😂

Demokrasia yasasa Samia must go Aleluyaaaaa Samia must go Aleluyaaaaa 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kuna pikindi nacho cha Benjamin William Mkapa

Waislamu waliongozwa kumchukia na kuambiwa kiongozi bora ni Profesa Haruna Lipumba

Mkapa tukaambiwa ni chinga wa Msumbiji must go

Demokrasia kutokea nyumba za Ibada ni upumbavu
mkubwa zaidi ✍️
 
Viongozi wa Dini wasasa na wale wapya uko mbele ya Safari ingependeza wabaki kwenye majukumu yao
ya kulea jamii kiroho basi wasijiingize kwenye Siasa👈

Siasa zibaki kwa wanasiasa wenyewe ✍️
 
Ndiyo maana nakwambia sisi Afrika hatulipi kodi ipasavyo kama wanavyolipa wazungu. Hata mtu ana nyumba za kupangisha huko mitaani lakini halipi kodi kabisa kabisa. Ana mapaka, nguruwe, mbuzi lakini hawalipii kodi, ana kisima chake kachima anachota maji lakini halipi kodi, kwanza hajui kwamba hata maji ni madini.
Kuna haja gani ya kulipa kodi inatofujwa? Ama huko Ulaya unaiga. ulipaji kodi tu, lakini hutazami nidhamu yao ya matumizi na mifumo yao ya uwajibikaji?
 
Mpaka wananchi kufanya maamuzi ya kubadili chama tawala kuna mambo ya ovyo wamepitia mf,mfumuko wa bei,ufisadi,utekaji,huduma za kijamii duni,hakuna uwajibikaji,ilani isiyotekelezeka,haki jinai,ukosefu wa ajira na matumizi mabaya ya raslimali za umma,kumbuka vyma tawala vingi vimekaa madarakani muda mrefu halafu unataka mabadiliko ghafla within a short time,say one term pili vyama pinzani vinakumbana na vikwazo vya masalia kwenye mifumo ya utawala .
Kama hayo yote yapo ni kazi ya chama cha upinzani kusema namna kitakomesha huo mfumko wa bei, ukosefu wa ajira, kupambana na vibaraka wa wazungu, kukabiliana na watakaotaka kuiangusha serikali yao, nk badala ya kusema hao wameshindwa tupeni tu sisi.

Chama ambacho kweli kinataka kukomesha umaskini wa wananchi hakiwezi kupanga kuwakosesha wananchi usafiri au kuwakata vidole raia ambao unataka kuwaongoza ukiwa Ikulu.
 
Kuna haja gani ya kulipa kodi inatofujwa? Ama huko Ulaya unaiga. ulipaji kodi tu, lakini hutazami nidhamu yao ya matumizi na mifumo yao ya uwajibikaji?
Kuna wakati hata sielewagi wanaosema hivyo wana maana gani. Yaani unataka kusema sio kodi zetu zinazotusambazia umeme na shule nchi nzima, kulipa majeshi na watumishi. Kama sio kodi zetu nani anatusaidia kuwalipa askari wanaotufanya tuwe salama, madakari, walimu, manesi, nk? Nani huyo ametujengea bwawa la umeme na madaraja marefu? Au hujui kodi ina kazi gani?

Unaposema kodi inaliwa ni kionyesha kuwa elimu yetu bado inahitaji CCM iendelee kutawala ili tuendelee kuiva na kukomaa kifikra.
 
Hizo kodi nyingi zinatoka kwenye indirect tax. Hata hivyo huwa mnajigamba kuwa tuna raslimali hadi wazungu wanatuonea wivu, uzeni hizo acheni kutukata kwenye pesa zetu za miamala ya simu.
 
Sikubishii, sasa wewe nionyeshe chama cha upinzani cha nchi gani Afrika ambacho kilibadilisha namna mambo yalivyokuwa huko nyuma na sasa vijana wanapiga vigelegele na vifijo kwa furaha ili nasisi tuseme naaam!! tufanye kama wale.

Tulichokiona sisi ni chama cha siasa kuchoma moto hata hiki kidogo tulichokidunduliza kwa taabu na mateso makubwa kwa miaka 64.
Vipo vingi sana. Sema wewe upo kwenye jela ya CCM ndio maana huoni. Hapo Kenya uchumi wa Kenya ulibadilishwa na Kibaki alipoingia madarakani. Nenda Kaangalie Botswana Wana mfumo wa uchumi mpya. Unajua hata Uganda Museveni alikuwa Mpinzani?
 
Kaakaa!! watu wenye uhakika wa kulipa kodi ya kipato ni waajiliwa tu. Wafanyabiashara wanakwepa kodi, unanunua hupewi risiti unauza hutoi risiti. Unaweza kupewa risiti yenye malipo pungufu au feki.
Hiyo ndio CCM Sasa haijali mambo ya msingi yenyewe ni kuteka na kuua raia wanao ikosoa.
 
Kama kwa mbali unaanza kuona baadhi ya vitabia vya hovyo walivyonavyo CCM na wapinzani nao wanavyo.

Basi unaweza kuthibitisha kabisa hata hawa nao wakiingia ikulu watafanya upuuzi wa CCM.

Kazi inabaki kwetu, tuwape ili kuwajaribisha?!

Kama unaona wanakosea lakini hawawezi kunyoosheana vidole waonyane, wao ni kuteteana tu kwa nguvu zote!.

Hivi kweli hawa nao wakipewa hii nchi watakuwa na tofauti gani na CCM wanaolea na kulinda mafisadi!

Siasa za hii nchi bado zina utoto mwingi sana, zimekaa kishabiki kama Simba na Yanga.
Bakini na CCM kwani shida ipo wapi. Niliwasifu CHADEMA waliposusia uchaguzi. Mmbaki mlichagur liccm lenu milele.
 
CCM imeshikilia kwa asilimia 98 vyombo vyote vya maamuzi.
1. Wenyeviti wa vijiji na mitaa
2. Madiwani
3. Halmashauri zote
4. Bunge
5 serikali
 
Bakini na CCM kwani shida ipo wapi. Niliwasifu CHADEMA waliposusia uchaguzi. Mmbaki mlichagur liccm lenu milele.
Aisee...

Naona umeshajikatia tamaa!

Safari bado ndefu sana hii, usikate moto mapema hivyo.
 
Mtazunguka sana ila uimara wa nchi unaanzia kwenye katiba yake na sio vyama vya upinzani.
Ccm inaogopa katiba imara inabaki na propaganda vyama vya upinzani vikiingia ikulu havitaweza kutawala.
Hakuna vyama pinzani ila kuna vyama mbadala.
 
Back
Top Bottom